MFUMO WA KUTUPATIA TAARIFA/LALAMIKOMnaboa sana yan...kwa kweli
TANESCO KAHAMA KWELI NI JIPUUU
MFUMO WA KUTUPATIA TAARIFA/LALAMIKONaomba kudaisiwa jaman tumeweka luku tangu tulipo unganisha tumenunua luku Mara moja tu! Ni mwaka Jana mwez wa kumi!
Nyumba iatumia taa tu
Afike ofisi ajaze fomuNaomba Ufafanuzi Kutoka Kwenu Tanesco
Mtu Aliyefungiwa Umeme December 27, 2016 Hadi December 27 , 2017 Ametumia Units 205 Kwa Matumizi Yake.
Je Anawekwa Kwenye Kundi Lipi La Watumiaji Umeme ? Yaani Anapaswa Kuja Mfano Ofisini Kwenu Ama Moja Kwa Moja Ninyi Tanesco Mnamweka Kwenye Kundi La Watumiaji Hao Wadogo
Mkuu unavyosema TANESCO inatupenda wateja wenu nashindwa kuwaelewa,, inbox tuliongea swala linalotaka kufanania ufisadi au wizi lakini hamtaki kushughulikia sijui mna maana gani angalieni Sana hii kitu nimesha lalamika Sana lakini hamfatilii kwa nini? Kuweni serious na kazi jamanTunawapendwa wateja wetu na tunapenda ushirikiano wenu ili kurahisisha kazi ya kuwahudumia
TUPATIE TAARIFA SAHIHI NA FASAHA KWA HUDUMA BORA.
NDUGU WAPENDWA WATEJA WETU MNAOTOA TAARIFA KUPITIA MITANDAO YETU YA KIJAMII TUNAWAOMBA MZINGATIE YAFUATAYO ILI KURAHISISHA UFAFANUZI NA UFUMBUZI WA TATIZO AU TAARIFA HUSIKA
1.ENEO HUSIKA
(Mnaweza kuwa eneo moja lakini mnahudumiwa na transfoma au njia ya kusambaza umeme (feeder) tofauti)
2.NAMBA YA SIMU
(Wakati mwingine umeme upo kote isipokuwa kwako hivyo na rahisi kuwasiliana na wewe)
3.KARIBU NA NINI
(Kuna alama vitu au watu mashuhuri karibu na eneo lako mfano ofisi ya Serikali ya Mtaa, Mahakama, Kituo cha Polisi nk)
4.JINSI YA KUFIKA MAKAZI YAKO
(Toa ufafanuzi wa jinsi ya kufika makazi yako,chukulia unamuelekeza mtu ambaya hajawahi kufika kabisa)
5.MKOA,WILAYA NA KITONGOJI/KIJIJI
(Taarifa hii ni muhimu sana kusaidia kubaini eneo husika lipo wapi kwani yapo maeneo yanayofanana kwa majina lakini yapo Mikoa tofauti mfano Magomeni ipo Dar es Salaam na Mkoa wa Mtwara pia.)
6.KAMA NI TATIZO LA MITA NINI KINATOKEA UKIWEKA UMEME
(Kila mita ina ujumbe wake unaoashiria kitu fulani hivyo kubainisha ujumbe kunamsaidia mpokea taarifa kukupatia maelezo sahihi mfano mita namba 24339173921 inaonyesha error 77)
7.KAMA NI KUSHINDWA KUNUNUNUA UMEME UNAPATA UJUMBE GANI NA UNANUNUA KWA NJIA GANI
(Ujumbe huu ni muhimu sana kuweza kubaini chanzo cha tatizo pamoja na njia iliyotumika kununulia umeme mfamo Mpesa, Tigopesa, Maxcom nk)
TUNAENDELEA KUWASIHII WATEJA WETU KUZINGATIA UTOAJI WA TAARIFA SAHIHI NA FASAHA KWA HUDUMA BORA ZAIDI KUTOKA TANESCO.
ENDELEA KUFURAHIA HUDUMA BORA KUTOKA TANESCO
Tunaomba namba yako ya simu na aneo lako mkuu tukuhudumieKuna maeneo hapa moshi umeme umekatika tangu saa moja na dakika tano, najaribu kupiga namba yao ya emergency 068771310 iko busy fo 45 minutes, sijui huyo ofisa aliyepo anaongea na nani muda wote, namba nyingine inaita tu haipokelewi 0765397925.
Hivi kama kuna moto au hatari yoyote ile, over 45 minutes kuna kitu kitaokolewa kweli
Naona mmekaa kimya wakati watu tumetumia pesa.Habari ya asubuhi nimenunua umeme kupitia MPesa kwa akaunti Namba 4311 5266 496
Umeme wa Tshs 20,000/= lakini nimepewa unit 22.5 badala ya unit 56
Naomba msaada kueleweshwa na mita hii haina deni lolote
Shukrani SanaAfike ofisi ajaze fomu
Tunaomba namba yako ya simu mkuuHabari
Mimi ni Mkazi wa Moshi Kilimanjaro Eneo la Bonite Kijiji cha Chekereni Kitongoji cha Miembeni
Kwa kweli tuna tatizo kubwa la umeme ni muda mrefu limekuwa likilalamikiwa kwa Uongozi wa Tanesco mkoa wa Kilimanjarao bila mafanikio. Tatizo liko hivi:
Umeme ni mdogo sana hasa saa za jioni na usiku unawaka kama kibatari huku ukichezacheza sana.
Wakati wa mvua kama jana unakatika mara kwa mara na kupungua sana; toka mvua inyeshe jana unakatika na kuja ukiwa na kiwango kidogo sana.
Tanessco walishalalamikia swala hili hadi kwenye vyombo vya habari lakini bado hawajalitatua; walileta nguzo wakasema wataweka nyaya mpya wauongeze lakini nguzo zimekaa hadi zinaoza sasa bila hata kuwekewa waya wowote.
Tusaidieni jamani tunateseka. Asante.