Luku yangu nikinunua umeme napewa units ndogo tofauti na wenzangu msaada tafadhari
 
Lini mtaacha tabia yenu ya kuzima na kuwasha umeme kama Indicators za piki piki ya Sanlg?
 
TANESCO KIMARA MNAKERA KWA KWELI.....WIKI NZIMA MNAKATAKATA UMEME BILA HATA MAELEZO YA KURIDHISHA.....NAOMBA KUWASILISHA HILI KWENU KWA UFUATILIAJI.
 
Hivi mbona hatujapewa taalifa ya transformer zilizotolewa..kwamuda sasa haziludishwa kwanani transformer ya tuangoma na ya ponde zote zimetolewa sikumoja lakini muda haziludishwa
 
Hivi mmepeleka wapi transformer ya tuangoma na ponde pinda road..nakwanini hamtupi taalifa mmetuunga kwenye transformer zingine umeme unasinzia mufamwingine
 
Muwe mnatoa taarifa kwa umma juu ya kukatika Umeme, hili jambo siku hizi naona mmekuwa hamlijali kabisa....hivyo kutusababishia hasara kubwa....
 
Tumepokea taarifa kwa hatua zaidi mpendwa mteja
Rejea [HASHTAG]#4190[/HASHTAG] ya 20.4.2018
Update please maana sioni kama kuna kinachoendelea
Simu 0755759999
Magdalena Kaniki
Kongowe
Kibaha
Pwani
 
TANESCO Anagalieni hao wafanyakazi mlio waweka kwa ajili ya kupokea na kushughulika simu za wateja wamekuwa hawapokei simu kabisa simu mtu unapiga hadi mara tano lakini hakuna inayopokelewa sasa nini maana ya udharura hapo, kama mnavyosema dawati la dharura? Hii ni kwa dawati la Arusha.
 
Kabisa MKUU hasa wa Kigamboni ndio balaa.
 
Habari Tanesco.
Nguzo Hii iliyopo Kisukulu Banebane karibu na Mzee Masolwa imo hatarini kuanguka kutokana na udongo wake kuliwa na mafuriko ya mvua zinazoendelea.

Nimekupasheni, msiniulize tena.
 
Hivi huku songwe kuna shida gani mbona mnatukatia umeme kila jumamosi?
 
@TANESCO,leo maeneo ya uhasibu,mtoni kwa Aziz Ally uwanja waTaifa TEMEKE hakuna UMEME tangu asubuhi mpaka muda huu.
 
@TANESCO,leo maeneo ya uhasibu,mtoni kwa Aziz Ally uwanja waTaifa TEMEKE hakuna UMEME tangu asubuhi mpaka muda huu.
Tunawaomba radhi sana umeme utarejea hivi punde
 
Habari Tanesco.
Nguzo Hii iliyopo Kisukulu Banebane karibu na Mzee Masolwa imo hatarini kuanguka kutokana na udongo wake kuliwa na mafuriko ya mvua zinazoendelea.

Nimekupasheni, msiniulize tena.
Wilaya, eneo, namba ya simu na namba ya taarifa tafadhali
 
Tanesco hivi kigamboni tumewakosea nini?? Tangu asubuhi hadi sahii hakuna umeme!
 
Tanesco hebu acheni utaahira wenu jana mmetuweka bila umeme kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa saba usiku maeneo ya keko bora halafu saa 12 asubuhi mnatukatia umeme kwani huo umeme tunatumia bure
 
Mimi pia ni mmojawapo wa wanaoichukia hii huduma itolewayo na Tanesco kwa ujumla,hili la kujaza form ili kubadilishiwa Tariff jirani yangu kaijaza miaka mitatu sasa,bado anazungushwa na wenye kutakiwa kuhakiki,tumemshauri aachane nao aendelee na kazi ya kumzalishia kipato,suala la kukatika umeme ovyo siyo wakati wa mvua tu,kwa tafakari yangu ni kwamba mtu mmoja ndani ya shirika akiamua umeme ukatwe eneo fulani kama ana mamlaka utakatwa,pia kama wanakata matawi ya miti na kama wanabadilisha nguzo/waya umeme unakatwa,bado kubadilisha trasformer nao hukatwa,mnatuumiza kwa kweli,service charge iko palepale pamoja na aina hii ya huduma yenu,Tanesco ni shida,badilikeni,niko Vituka
 
Ukweli utawaweka huru, Mnaonaje endapo Mtatuweka wazi, Nikweli Mita za Njia Tatu, three phase hazipo kwenye bohari yenu au Management huku Mikoani ndohawataki kuagiza Mita kutoka Head quarter????????????! Manake imekuwa to much Sasa, Mita Miezi Miwili Kweli?????????????! Elezeni /Tangazeni kwenye Media tujue.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…