Wametuunguzia vifaa vya umeme huku mkoa mmoja wa Nyanda za juu kusini, Sabufa zote zimenyauka taa chaja za simu ,Kisimbuzi...nimewahi kuzima Tv tu nayo ingeenda na maji.
 
Wakuu: Nina swali kuhusu mita za LUKU. Zipo mita za kuweka ukutani na za kwenye nguzo. Nini tofauti yake? Na je mita za LUKU za ukutani zimesitishwa au zinafungwa bado majumbani kwa sasa?
Hakuna tofauti katika kupima matumizi bali tofauti ipo kwenye technologia iliyotumika.
 
Upo ofisi ipi ndugu mteja. Umienda kufanya malipo.
Tunaomba kujua upo ofisi wilaya na mkoa tuweze kukusaidia
 
Endelea kufurahia huduma za TANESCO kwenye simu yako ya kijanjani. Sasa unaweza kulipia huduma za shirika kwa kupitia simu cha kufanya fuata maelekezo haya.

TANESCO TUNAYAANGAZA MAISHA YAKO
 
Huduma zenu za matandao ni hovyo nipo Tanesco nimepoteza muda kusubiria matandao nipewe risiti nikalipe bank lakini mtandao hakuna. Mbona kwenye mitandao ya simu kuna mtandao ninyi mna shida gani na mkongo wa taifa, mmevurugwa nini?
Upo ofisi ipi ndugu mteja. Umienda kufanya malipo.
Tunaomba kujua upo ofisi wilaya na mkoa tuweze kukusaidia

Haya ongeeni sasa, sisi tunawaangalia msipigane ngumi na kutoana ngeu
 
Mmetuunguzia vifaa Iringa sijui umeme mmezidisha sio mimi tu hata majirani.
 
Fire-Sinoni/Lemara Mitimirefu ( Karibu na kituo cha Watoto Yatima). Umeme unawaka na kuzima ( kama indicator ya Gari) Kila ifikapo saa 12 Jioni. Na hufanya hivyo siku nzima siku za Weekend.
 
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA
TAARIFA KWA UMMA
KATIZO LA UMEME- KINONDONI KASKAZINI

Shirika la umeme Tanzania Tanesco Mkoa wa Kinondoni Kaskazini linawataarifu wateja wake kutakuwa na katizo la dharura katika Laini yetu ya Masaki 3 kama ifuatavyo:-

*Tarehe* 07/11/2018 Jumatano

*MUDA*: Saa 01:00 Usiku hadi saa 02:00 Usiku
SABABU; Kubadilisha cable iliyoungua katika Kijiji cha Warusi.
Maeneo yatakayoathirika ni; Parts of Mwaya and Chole road, UNDP quorters,IFM flats, muhimbili MUHAS university hostels, double tree hotel, Mitaa ya bakhhresa masaki, kijiji cha warusi, Marry brown,kahama mining,Shule ya Kimataifa ya Tanganyika na maeneo ya jirani.

*MAWASILIANO*:
Dawati la dharura Mkoa wa Kinondoni Kaskazini 0784768584, 0716768584 au Kituo cha miito ya simu Makao Makuu 2194400 na 0768985100

*Tovuti*: www.tanesco.co.tz

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza
 
Kukatika kwa umeme huku yombo Buza kila Jumanne na Jumatano kutaisha lini? Mnatukwamisha mambo hayaendi
 
Yan nipo huku kigamboni kibugumo..tumelipia mita 2 za umeme, ni miezi miwili imekatika twafatilia mita bila mafanikio, hatujui ni nini tatizo.
 
Nimelipia umeme kupitia wakala selcom ni zaidi ya masaa 10 sijapata token namba ya mita ni 22118109044 naomben msaada wenu
 
TANESCO MAKAO Makuu hamlioni lalamiko langu kwa Tanesco Kigamboni au tatizo liko kwenu kwa kushindwa kupeleka vifaa kazi; kupeleka magari pamoja ukarabatii wa magari yaliopo ili kuboresha huduma maana Tanesco Kigamboni wanna visababu vyao eti magari Ni machache na mabovu.
 
Shirika la umeme TANESCO wilaya ya SONGEA mkoani RUVUMA...mmezidi kukatakata umeme bila utaratibu maalumu, bila taarifa kwa wananchi. Tunajua kunachangamoto kubwa katika huduma ya umeme nchini kwetu, lakin huku SONGEA kuna balaa. Ukikaa masaa mawili bila umeme kukatika mpaka unashangaa. Wilaya imeinganisha katika Grid ya Taifa lakin mizengwe ndi inazidiiii.
TANESCO SONGEA MNANINIIIIIIIIIII....
 
Umeme umekatika kwenye nyumba yetu yenye meter nunber 37154698759..naa huu Hapa chini ndio muonekano wa meter
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…