Ebu nipeni moyo kidogo, nimepimiwa kuna kama mita 150 nguzo 2 ya tatu ntatumia ile ya msongo mkubwa ivi gharama inaweza kuwa kama kiasi gani maana ni kimya sijapata bado mrejesho
aliyekupimia ndo mwenye majibu sahihi, ushauri wangu; nenda kituo kilichokaribu na wewe watakupa makadirio sahihi;
Mimi kwangu ilikuwa kama yako nililipaga 1.2mil yaani nguzo tatu, hata kama hiyo ya msongo Mkubwa IPO lakini lazima ulipie nguzo tatu na waya zake
 
Tanesco mie tatizo ni kua napata ile error 77 ingawa luku inakua ina umeme fresh na umeme unakatika kwangu tuuu almost kila baada ya cku mbili na kwa wengne unakwepo had baada ya muda sanaa ndo unarudi nimejaribu kuweka ile 0 mbele na namba za mita ila hakuna kitu ata nikiconnect kweny switch ili kipokeo kiwez kuwasiliana hakuna kitu.Hii ishakua kero kwa kweli!!..?
 
Shukran kwa idea ila kwako ilikuwa mita ngap?
 
Walipita kuchukua Ramani mtaani kwetu kata ya mbondole ktk mtaa wa kurutini wakafika mpaka kwangu ambapo bi nyumba ya Tatu kutoka barabarani na ni mtaa kabisa pia niliwaonyesha pakuweka nguzo na alama ikawekwa cha ajabu siku wakipokuja kusimika nguzo hawakuweka badala Yake waliwawekea mtaa wa pili yaani nyuma ya nyumba yangu nyumba moja kabla nilipowauliza wakasema Ramani haionyeshi kama hapo nguzo inahitajika wakaniambia niende ofisi na malalamiko yako

NIKAONA SIWEZI KUMLIPIA MWANAMKE MAHALI ASIYENIPENDA.

Nikaingia dukani nikalichafua bati langu KWA sorala za kufa mtu
Sasa kwangu ni kama tansco org

Kwao unakatika kwangu upo
Kwao wanalipia luku kwangu no
Kwao wanatumia friji kwangu natumia friji
Tuko sambamba ila Mimi nawazidi

Badilikeni kila mtu atumie umeme wenu
 
Yani pamoja na Waziri kutishia kutumbua watu,lakini bado mnakata tu umeme,kweli nyie vichwa vyenu havieleweki
 
WAKAZI WA KMR HILI GRP LINA MSAADA SANA LA TANESCO

TANESCO HUDUMA KIMARA
 
Pamoja na kupigwa mkwara na waziri wa nishati,jana mwenge umeme wamekata na muda huu wamekata tena,
 
Tanesco naanza kuwapongeza kwa majukum yenu ya kila siku.
Mm niko mbeya nzovwe mtaa wa halengo kuna transformer inasumbua Tunaenda week sasa hatuna Umeme.
Tunaomba msaada
 
Inawezekana naogopa tu kuhusu solar, nipe mwangaza ni uekezaji wa aina gani unahitajika kupata umeme ambao naweza run fridge masaa 24 bila shida
 
Kuna shida umeme ukiangalia unit zipo lakin haufiki ndani na kuna alama ya kiswitch katika remote namba za meter ni
24214371965
 
Tanesco kuna Mgao? Tumechoka kukatiwa umeme kila siku jamani na huu ni msimu wa sikukuu muda mwingi tupo majumbani...mnatutesa
 
Eti likizo [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]tanesco ukiwafikiri unaweza pata presha
 
"Mradi wa gas kutoka Mtwara utakapokamilika , tatizo la umeme kwa Tanzania litakuwa historia maana tutakuwa na umeme wa uhakika inchi nzima" Prof Muhongo enzi zake akiwa waziri wa nishati na madini
 
Baada ya kukamilika,tatizo lipo palepale na suala la gas halizungumziwi tena. Sasa tumehamia Stiglers gorge
"Mradi wa gas kutoka Mtwara utakapokamilika , tatizo la umeme kwa Tanzania litakuwa historia maana tutakuwa na umeme wa uhakika inchi nzima" Prof Muhongo enzi zake akiwa waziri wa nishati na madini
 
Hawa Tanesco hawapo siriazi kabisaa...wanaubabaishaji wa kiwango cha lami..haiwezekani leo siku ya tatu hatuna umeme hapa kwetu eneo Mlalakuwa Mwenge, yaan tatizo Luku meter inasoma CONNECT muda wote. Inagoma kuingiza token kabisaa.... cha ajabu tumewafikishia malalamiko yetu pale ofisi zao mikochen wametujibu majibu mepesi sanaa...eti turudi nyumbani mafundi watakuja kurekebisa mchana.. leo siku ya tatu kila tukiwapigia simu wanajifanya eti wanashangaa...so sad.. Tanzania ya viwanda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…