TANESCO mbona kuna mgao lakini hamtangazi???
Kweli umeme huu ni wa gesi kweli? Waziri anajua kuna mgao kweli? Toka jana umeme unakatika kwanzia saa 3 asubuhi mpaka sàa 12 jioni,leo tena umekatika saa 3.

Kwanini mnafanya kimya kimya? Mnategemea wenye saluni watakula wap? Wauza barafu,lamba lamba watafanya nini?
TOENI TANGAZO KILA MTU AJUE AJIPANGE MAPEMA JINSI YA KUKABILIANA NA MGAO NA MSEME UTAKUWA WA MUDA GANI?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Asante sana kwa taarifa... Nzuri. Hivi mimewashinda nini kuautomate payment mtu akilipa umeme uwake palepale badala ya kuingiza kwenye meter zenu na nyingi mbovu?
 
Tanesco bora mtuambie kama kuna mgao tu maana sasa hivi maeneo ya Mbezi Beach kila siku mnazima umeme
 
Mimi nipo Arusha. Niliomba kuunganishiwa umeme na mwezi wa 11 na nililipia kama 175000 hivi. Wakaniiambia nisubiri ndani ya siku 30. Nilisubiri na baada ya kuona muda nilioambiwa umepita, nilirudi tena, wakaniambia watanujulisha maana wateja walikuwa wengi hivyo nisubiri hadi zamu yangu itakapofika.
Baada ya muda kidogo nikarudi tena TANESCO, wakaniambia inahitajika ngozo ndogo T-pole kitu ambacho sikuambiwa tokea mwanzoni,hivyo nisubiri hadi nguzo zipatikane. Nikawauliza nisubiri kwa muda gani? nikajibiwa mpaka sasa hatuna ngozo, na zilizopatikana tunawafungia mpaka mwezi wa nne 2018. kwa hiyo nisubiri mpaka watakapo nipigia simu.

Sasa nashindwa kuelewa kwa nini wasitoe majibu mapema ili kuepusha usumbufu wa wateja kwenda kuwaulizia ulizia?
 
Ulilipwa jina gani na namba yako ya simu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwenge,Mbezi,Ubungo na maeneo mengi ya Dar umeme unakatika sana sasa hivi.Mnaanza tabia yenu mdogo mdogo.Serikali ikikaa kimya mnatuzidishia maumivu.Nyie watu sijui mfanywe nini aisee!
Rais Magufuli tusaidie,fumua hili shirika linatuumiza watanzania.
 
Mwenge,Mbezi,Ubungo na maeneo mengi ya Dar umeme unakatika sana sasa hivi.Mnaanza tabia yenu mdogo mdogo.Serikali ikikaa kimya mnatuzidishia maumivu.Nyie watu sijui mfanywe nini aisee!
Rais Magufuli tusaidie,fumua hili shirika linatuumiza watanzania.
Tunafanyia kazi mpendwa mteja wetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunafanyia kazi mpendwa mteja wetu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mnafanyia kazi gani sasa maana imekuwa kama utaratibu kabisa. Bahati mbaya basi ingeishia siku moja. Lakini tangia wiki ianze hali ni ile ile, mnakata kuanzia saa 3 asubuhi mnarudisha saa 9 mchana! Ikifika saa 1 usiku tuu mnakata tena mnarudisha saa 6 usiku!

Sasa huko ndo kufanyia kazi?? Mnatutesa bhana! Au hayo marekebisho hayaishi? Au kila siku haya maeneo yanakuwa na hitilafu? Na kama yana hitilafu siku zote vipi kuhusu usalama wa watu na mali zao pindi mnapolejesha?

Kama kuna mgao seneni watu tujipange kivingine na ikibidi tubadili ratiba zetu za kazi!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi unit 50 mnazotowa mara baada ya kufungiwa umeme kwa mara ya kwanza ni hisani na kama hisani ni bora muitoe iliijulikane moja haipo

Tangu mwaka Jana mwezi wa 10 hadi leo nasumbukia unit 40 kweli

Kuweni waungwana tu

Namba ya luku ni 54183706958

Jina Rebeca Ruhunde Mahona

Mkoa Shinyanga
Wilaya Kahama
Mtaa MWENDAKULIMA KATI
 
Nnaishi nyumba yenye wapangaji wengi sana hivyo uchangishanaji na matumizi yake umekua ni changamoto sana kwangu.
Je, ninaweza kupata mita ya kwangu pekeangu nikafunga ndani kwangu? kama jibu ni ndio, Je ni gharama kiasi gani hiyo mita?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…