Napenda kufahamu kama TANESCO wana utaratibu wa kumwezesha mtu mwenye uhitaji wa umeme ambaye ili umeme ufike kwake itamlazimu pengine nguzo sita hadi nane, na yupo katika eneo ambalo jirani kuna mradi wa REA uliokamilika,ila makazi husika hayajajumuishwa kwenye mpango REA japo ni kijijini.je kama mhusika anaweza kulipia nusu ya gharama fedha ya nguzo zinazohitajika na gharama inayobakia ikafidiwa kwa wahitaji wengine watakaokuja kuomba huduma siku zijazo,na kama haiwezekani ni kwa nini?
 



Safi sana Tanesco.
 
 

Attachments

  • Screenshot_20190729-195741.png
    47.1 KB · Views: 14
Jina: Shabani Mtonga
Eneo: Mtaa wa Mvuleni, kata ya Kitonga, Wilaya ya Ilala Mkoani Dar es Salaam
Tatizo: Nililipia UMEME tarehe 18.03.2019, wiki mbili zilizopita nimeletewa nguzo 2 na kuahidiwa mnamo tarehe 27.07.2019 ningeletewa mita na kufungiwa nyaya za UMEME lakini mpaka Sasa bado huduma haijakuja.
Simu: current phone number0763531628/ Namba ya awali niliyoandika Tanesco KISARAWE wakati wa kulipia ni 0713673276 ambayo kwa Sasa haipo hewani. Thanks.
 
TANESCO nasikitika sana. Yaani muda wote tulikosa umeme kwa sababu za watu binafsi.


Leo waziri kasema hakuna kulipia nguzo. Na familia ya nyumbani wakati nikiwa chuo walitaka kuunganisha umeme wa REA ila.mradi ulikuwa unasua sua mwezi wa kumi na moja ndo wakakumbuka na baadhi ya wateja kulipia alafu wakakaa muda mrefu hadi wa 3 mwaka huu wakaunga chapchap na kukabidhi TANESCO mapema mwezi wa tano.

Nyumbani walikuwa wamefanya taratibu za REA ila ikakabidhiwa so gharama tukaambiwa ni laki 5 wakihesabu nguzo mbili na mita.

Tunaomba mmlike hili suala ikiwa waziri amesema hatulipii nguzo basi fatilia tulipie vinavyotakiwa kulipiwa. Mtuondolee kero.


Location:

Mkoa Mara
Wilaya-Tarime
Kata-Kemambo
Kijiji-Kewanja
Kitongoji-Kemambo
 
Nina makaazi yangu pia sehemu fulani (kijijini) kutoka kwenye chanzo cha umeme zinahitajika nguzo 10 (yaani nahitaji umeme wa matumizi ya kawaida) hapa nitapaswa kugharimika kiasi gani hadi nawashiwe umeme?
 
Nimelipa 320960 ili nivutiwe umeme..nimelipa toka ijumaa mpaka leo sioni kuungiwa umeme
Mkoa : dodoma
Mahali:kikuyu
 
Tamko la kutolipia Nguzo ni vijijini tu au hata mjini?
 
TANESCO na REA naombeni mnijibu...... mradi wa umeme vijijini mmepitisha nguzo ya umeme katikati ya shamba langu je nifanyeje?.... nahitaji zitoke ziwekwe pembeni mwa mpaka sababu wakati wanapitisha nguzo mimi sikuwepo .. je nifanyeje
 

TANESCO
 
Ndugu wanabodi, naombeni msaada nataka nipate namba ya Manager wa TANESCO KASULU KIGOMA. Please naombeni msaada sana TANESCO Kasulu nipate Namba ya Manager, nisaidieni. Wasalaam, Kidudu
 
TANESCO KIMARA KWA MARA NYINGINE HAKIKA MNAKERA.HII NI MARA YA PILI MNAKATA UMEME MIDA YA ALFAJIRI SANA BILA TAARIFA YOYOTE KWA WAKAAZI WA KIMARA.MNATEGEMEA FAMILIA ZITAJIANDAA VIPI NA MASWALA YA ASUBUHI KABLA YA KUANZA PILIKAPILIKA.

NAOMBA NIWASISITIZE TENA KUZINGATIA KUFANYA KAZI KWA KUTOA TAARIFA NA UWELEDI.

ASUBUHI HII YOTE MNATAKA TUKANYOOSHE NGUO WAPI NA KWA NN KWA SIKU HIZI MBILI UMEME UKATIKE ASUBUHI TU.
 
kwa nn watu masikini wote tunaokaa vijijini na hatuna matumizi makubwa ya fridge, cooker, wala heater tumetolewa kwenye tariff 0 na kupandishwa tariff 1?
Tanesco tunaomba kuwapa taarifa kuwa huku Moshi umeme umekatika too saa 12 asb haujarudi. Tusaidie.
 
Nina tatizo la LUKU naingiza token results inakuja ERROR 75, shida nini naomba msaada wa haraka
 
Habari za sahizi wakuu, nina tatizo la luku naingiza token results inaleta Error 75, ni siku pili sasa bila majibu tanesco hawajanibu mpaka sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…