Haya ni maajabu ya awamu ya tano ya chuma (Rais Magufuli).

- Zamani Shirika letu la Umeme Tanzania (TANESCO) lilikuwa linawauzia Watanzania nguzo za umeme 1 kwa Tsh. 1,000,000/- (Milioni moja). Awamu ya tano ya Mh. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, nguzo za umeme zinatolewa bure bila malipo yoyote (haziuzwi).

- Zamani Shirika letu la Umeme Tanzania (TANESCO) lilikuwa linajiendesha kihasara. Sasa hivi, TANESCO inajiendesha kwa faida maradufu na wanatoa gawio kwa serikali kuu kupitia hazina.

- Zamani umeme ulikuwa unakatika katika hovyo hovyo Ssaa 24, wiki nzima. Na sababu kuu iliyokuwa inatolewa au kusemwa ni "Bwawa la Mtera kukauka maji mara kwa mara."

- Lakini awamu ya tano ya Mh. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, umeme unawaka saa 24, Wiki nzima katika Vijiji, Vitongoji na Mitaa yote nchini. Na siku hizi Bwawa la Mtera halikauki maji tena.

Hongera sana Mh Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa Kazi Nzuri iliyotukuka.

2020

#MagufuliTena
 
Hongera sana RAIS, we real appreciate; Ila bado awanyooshe kabisaaa maana bado usumbufu kwenye kuungiwa umeme mjini 321,000/- bila nguzo hata moja kuhitajika, ni mita tu na kasha mita ni yao, japo wao kumiliki hizi mita ni sawa kabisaaa maana huduma ni zao, isije mtu akabidhiwa mita iwe yake halafu aka ichezea apendavyo maana ni yake
 
Nguzo bure wapi wakati bado Tanesco wanawauzia hizo nguzo wananchi??????? Matamko ya viongozi na watendaji wa Tanesco ni vitu viwili tofauti.
 
*Zamani Shirika letu la Umeme Tanzania (TANESCO) lilikuwa linajiendesha Kihasara,
Sasahivi, TANESCO inajiendesha kwa Faida Maradufu na Wanatoa Gawio kwa Serikali Kuu kupitia Hazina.
mkuu, una uhakika? kutoa fungu la kumi kanisani haimaanishi huna madeni mtaani kaka!!
 
Acha uongo wapuuzi (Tanesco ) wa Dodoma wamenipigia gharama za nguzo karibu 4, 000,000/-
 
habari ndugu mteja,
tunaomba kujua hio nguzo; eneo, wilaya, mkoa na namba yako ya simu
Hizi nguzo zipo mkoa wa Dar es salaaam wilaya ya Ubungo kata ya Goba Mtaa wa Muungano/Marobo Kisiwani,hii ni barabara inakarabatiwa pamoja na kuwekwa daraja(Biluku Road and Bridge),huku tunahudumiwa na Tanesco Tegeta Kibaoni,na mkandarasi yupo katika za mwisho za mradi kwa hyo hizi nguzo kachimba mitaro kaziacha katikati,namba yangu ni 0756666890/0719180972
 
Tunashukuru kwa taarifa tunaifanyia kazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…