ndugu mteja, ukisoma vizuri post yake aliiuliza swali ndio akamalizia kutupa maelezo, sisi tumjibu kwanza swali lake kuwa hakuna kitu kama hicho maana yake survey ni BUREE!!!, katika kuhusu kuhakikisha tumelipokea kwa hatua zaidi, tukaomba mtu ambae anafanya hivyo kinyume na utaratibu wa shirika
 
Ndugu TANESCO nina Shida ya kubadilishiwa Luku yangu, sehemu iliyowekwa kuna walakini mvua ikinyesha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari za siku ya leo
Hongereni na kazi mnazoendelea nazo mwaka huu


Naomba kujua Ni lini mtasambaza nguzo za umeme na kuwasha umeme KWENYE Kijiji Cha Lwamgasa kitongoji Cha majengo
Kata Rwamgasa, wilaya Geita, mkoani Geita

Maana TUNAHITAJI umeme
Lakini Tanesco hamjatufikia
Tunaomba nasi maana Ni haki yetu kupata nishati hiyo

Natanguliza shukrani Kama mtalifanyia kazi
Asante.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wapi nguzo bure?Hapo moro ndani ya manispaa hawana umeme na wameambiwa walipie nguzo.Shame

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niko Kibaha Pwani,sio siri vifaa vyetu vingi vimeshaungua kwa huu upumbavu wa kukata umeme bila taarifa. Tunajiuliza kwani mgao wa umeme umeanza? kama sivyo kwa nini kuwe na double standard Kibaha Picha ya Ndege umeme unawaka, lakini kuanzia Gereza la Mkuza hadi Sofu umeme hakuna.Mfano leo umeme umekatwa majira ya 1000hrs ukarudi 1900hrs lakini kufikia 2000hrs umeme umekatwa tena,hivi ninavyoandika niko kwenye giza zito,kwa nini TANESCO Pwani ni wababaishaj? Sisi wateja tunanunua umeme lakini haturidhishwi kabisa na huduma inayotolewa.Tunamuomba Mh. Kalemani Waziri mwenye dhamana aje Kibaha Pwani ajionee utendaji mbovu wa TANESCO Pwani. Yaani huku kwetu umeme kukatika bila utaratibu tumeshaona ni kitu cha kawaida. Awamu hii ya tano inayoongozwa na Mh. Rais John Joseph Pombe Magufuli sera yake ni kuona umeme unakwenda hadi vijijini kwa mpango wa REA lakini kuna watendaji wanataka kukwamisha jitihada za Mh. Rais. Ikiwa hapa Kibaha kuanzia Gereza la Mkuza hadi Sofu umeme unasumbua watamudu kufikisha vijijini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
KUNA MRADI WA REA HAPA KIBAHA KATA YA VISIGA MIWALENI, TANESCO WALIKUJA KUPIMA WAKAWEKA ALAMA ZA NGUZO MIEZI MITATU ILIYOPITA HADI LEO HAWAJARUDI.
TUNAOMBA KUFAHAMISHWA WALIPOFIKIA HADI SASA.

0718505991

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanesco mnatutesa Sana na policy zenu sisi wafanyabiashara tunakamatia fursa popote ninaposhindwa huku nafanya plan B nnapotaka kuhama na mita yangu ya 3phase kwenye eneo jingine mnakataa kwa hyo nichome laki tisa nyingine ya kununua meter ilihali ipo na eneo lenyewe ni ndani ya mkoa husika fikirie kuhusu hilo

Sent from my TECNO LC6 using Tapatalk
 
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO) MKOA WA PWANI. linawataarifu wateja wake kuwa kutakuwa na katizo la umeme kama ifuatavyo:

MUDA: SAA 4:00 HADI 11:00 jioni
SIKU: JUMAPILI 05/01/2020

SABABU: Matengenezo katika laini zetu ili kuboresha upatikanaji wa umeme wa uhakika.

MAENEO YATAKAYOKOSA UMEME NI:
Mlandizi yote, Misugusugu, Boko, Mwendapole, na Tumbi.

Tafadhali usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka toa taarifa kupitia namba za simu zifuatazo: - KIBAHA 0657108782, 0739108732

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbe mna uwezo wa kuutangazia umma kuhusu katizo la umeme,sasa mbona mwanzo mlikuwa mnakata bila kutoa taarifa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanesco kwakweli mnatufanya tuichukie CCM bila sababu. Sasa kutokea Vingunguti hadi Chanika mmekata Umeme bila kutoa taarifa tangu saa moja asubuhi kweli ni halali?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni wiki sasa kuna jirani yangu kwake umeme hakuna mita imeungua! Anafanya biashara sasa watu wakamshauri awaambie TANESCO wamfungie umeme kwa njia ya one way au direct.

Je, hii one way au direct ndiyo inafanyaje kazi?

Je, kuna madhara yoyote kwa kutumia njia hii ya upitishaji umeme?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mm ni mteja wenu wa Tanesco nipo Manzese karibu na uwanja wa Fisi
Number mita yangu ni 54151453237
hii mita ninashindwa kuielewa inapata sasa mwezi sasa haionyeshi umeme kuisha wala kuzima
Naweka umeme hata sh 3000 naweza kutumia week nzima, kitu ambacho huko nyuma haikuwa hivyo, nyumba ina wapangaji zaid ya Tisa
Nimetoa ripoti Tanesco Magomeni tokea tarehe 30- 12 - 2019 mwaka jana mbaka leo awajafika kuja kuchek tatizo
Msije baadae mkaja kutustaki ohho mita imechezewa sijui mita inajikopesha
Mje mcheki tatizo jamani kama mita ni mbovu nijue moja nyumba zenyewe hizi ni za urithi.. Tanesco mnakwama wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…