kwanza hakikisheni umeme haukati ovyo ovyo!
kwa wastani umeme hukatika mara 4 kwa wiki ni sawa na wastani wa masaa 16 kwa mwezi, unaweza kupata jawabu la hasara tunayopata haswa kwa wenye viwanda vidogo. tasco tanescoo!!!
 
kwanza hakikisheni umeme haukati ovyo ovyo!
kwa wastani umeme hukatika mara 4 kwa wiki ni sawa na wastani wa masaa 16 kwa mwezi, unaweza kupata jawabu la hasara tunayopata haswa kwa wenye viwanda vidogo. tasco tanescoo!!!
Eneo gani na namba yako ya simu mpendwa mteja,je huwa unapata taarifa zetu za kazi ya uboreshaji miundombinu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunaomba namba yako ya simu mpendwa mteja,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Personally I dont trust government institution in social network.
Why dont you launch your own websites
Are'nt you a threat posed by gov to threaten users?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
*TAARIFA KUHUSU DAWATI LA DHARURA MBAGALA*

Tunawaomba ndugu wateja wetu unapokuwa na suala la dharura, au kupata taarifa ya kukosekana kwa umeme, kutokea kwa hitilafu ya umeme katika eneo lako, na mengineyo.

Tafadhali usisite kuwasiliana na *Dawati la dharura TANESCO Mbagala* kwa namba za simu zifuatazo:
+255 714 073 588
+255 786 975 538
Au
Kituo cha miito ya simu TANESCO makao makuu:
+255 768 985 100
+255 22 219 4400

Tunawaomba mzingatie hilo ili muweze kupata taarifa kwa wakati kutokana na wakati mwingine kutokuwepo online kwa muda kutokana na mujukumu ya wakati huo.

*Imetolewa Na:*
Ofisi ya uhusiano
TANESCO Mbagala

TANESCO "Tunayaangaza maisha"
 
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani tarehe 20/8/2017 amefanya ziara katika Kituo cha Kupozea Umeme cha KIA mkoani Kilimanjaro kinachotoa Umeme wa kiasi cha megawati 18.

Kituo hicho kilijengwa chini ya Mradi wa TEDAP uliohusisha ujenzi wa Transfoma mbili zenye uwezo wa MVA 20 kila moja pamoja na jengo la kuendeshea mitambo ambapo Kituo kinasambaza umeme kwa wateja kupitia njia 6 za msongo wa kilovoti 33.

kituo hicho kilikamilika mwaka 2014 na kuimarisha upatikanaji wa umeme katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha.

Kwa kuwa utekelezaji wa Mradi huo wa KIA ulienda sambamba na ujenzi wa vituo vya kupozea umeme vya Mbagala na Kurasini, Dkt Kalemani aliwataka watendaji wa TANESCO kuhakikisha kuwa vituo hivyo navyo vinakamilika haraka ili kuboresha upatikanaji wa Umeme katika Jiji la Dar es Salaam.

Mradi wa TEDAP chini ya Wizara ya Nishati na Madini unahusisha Ujenzi wa njia za kusafirishia umeme wa msongo wa kilovolti 132, ujenzi wa vituo vitano vya kupozea umeme jijini Dar es salaam pamoja na Kituo cha kupozea Umeme cha KIA.

TANESCO "Tunayaangaza maisha"
 
Tarif 1 wanaotumia umeme chininya 75 unitd kwa mwezi na zaidinya hapo mpaka 7500 units ni tarif 1
Nilikuwa tarif 4,Julai mwaka jana nikarudishwa tarif 1 kwa kuwa nilikuwa nanunua umeme wa sh.10,000 kwa mwezi. Nilienda ofisi za TANESCO mkoa,nikaambiwa nitarudishwa tarif 4 na system. Lakini ni zaidi ya mwaka sasa sijarudishwa tarif 4 japo matumizi yangu kwa mwezi ni chini ya unit 75. Je,nifanye nini kurudishwa tarif 4?
 
Sheria inakutaka ununue umeme wa tsh 9150 ambao ninujit 75 kwa mwezi wewe ulikuwa unanunua unit 77 hivyo ulivuka takwa hilo na sasa upo tarif inayoendana na matumizi yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
habari za kazi
nina swali moja kidogo hivi nikitaka kuvuta umeme kwenye nyumba yangu nini haswa mnahitaji kutoka kwangu kama mteja mtarajiwa? mnafanya vipi na watu wa ardhi kuhusu kupeleka umeme sehemu zilizopimwa na ambazo hazijapimwa?

vipi kuhusu maeneo ambayo hayatakiwi kujengwa au yaliyojengwa kwenye hifadhi ya barabara,mito nakadhalika kwani ni mnapeleka umeme?
 
Ukitaka umeme kwanza hakikisha nguzo za kusambaza umeme zimefika eneo lako kisha mtafute mkandarasi aliyesajiliwa akufanyia kazi ya kutandaza nyaya ndani ya nyumba yako (wiring) kisha uje na kitambulisho utapewa fomu bure ofisi yeyote ile hapa nchini kisha tutakufanyia vipomo ( survey) na kukuambia kwa barua ulipe kiasi gani, ukilipa unafungiwa


Kuhusu maeneo yasiyopimwa , Utaratibu upo wazi kwa kuwa maeneo mengi nchini hayajapimwa tukisema hiki kiwe kigezo umeme utatembea maeneo machache sana utakubaliana nasisi hata hapa Dar es Salaam maeneo kama kimara na Mbezi Luis ndio yanapimwa saivi hivyo huduma inaenda kwa wateja huku upimaji ukiendelea.


Kuhusu maeneo yasiyotakiwa kujengwa, ikumbukwe kuwa maeneo ambayo hayajapimwa ni ngumu sana kusema hapa hapafai kujenga au laa na tungeongeza kigezo kuwa ukitaka umeme uende aridhi kwanza nadhani ungeona mlolongo wa malalamiko na ucheleweshaji wa huduma.aitha maeneo ambayo hayapaswi kujenga yakibainiswa na wahusika sisi tunaondoa miundombinu yetu mara moja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sheria inakutaka ununue umeme wa tsh 9150 ambao ninujit 75 kwa mwezi wewe ulikuwa unanunua unit 77 hivyo ulivuka takwa hilo na sasa upo tarif inayoendana na matumizi yako

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwahiyo natakiwa kufanya nini ili nirudi tarif 4? Maana matumizi yangu ni chini ya unit 75. Au ndo siwezi kurudishwa tena tarif 4?
 
Karibu TANESCO Masasi mkoa wa Mtwara kwa msaada wa dharura wasiliana nasi kwa namba 0789999924 tutakuhudumia



TANESCO "Tunayaangaza maisha"
 
Uzinduzi wa miradi ya REA III mkoa wa Mtwara wilaya Namyumbu


 
Tanesco, kiukweli nimefadhaika sana baada ya kufata process zote za kufungiwa umeme na baadae kukamilisha malipo
Baada ya kutajiwa gharama na kukamilisha malipo ndani ya siku iyo iyo na kungojea kufunguwa umeme ndani ya siku 30 za kazi badala yake imegeuka kuwa kero tu,

badala ya kupewa huduma yangu stahiki naambiwa nisubiri mpaka pale vitu vitakapopatikana wakati siku 30 zimeshayoyoma mnanitumia sms za kukatisha tamaa kabisa

Mbona wakati mnachukua pesa yangu imeingia faster kwenye account yenu ila umeme kwangu ndo imekuwa kero kiasi ichi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ndio sms yenu mmenitumia kwenye simu yangu

HABARI NDUGU MTEJA TUNAOMBA RADHI KWA KUKUCHELEWESHEA KUPATA HUDUMA YA KUUNGANISHIWA UMEME, KUTOKANA NA UHABA WA VIFAA. TUNAFANYIA KAZI SUALA HILI PINDI TUTAKAPO PATA VIFAA TUTAKUPIGIA SIMU KWA AJILI YA KUKUJENGEA! ASANTE KWA KUWA MILIVU.. NI SHIRIKA LA UMEME TANESCO KINONDONI KUSINI [MBEZI].

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Si ushukuru hata umepewa taarifa mkuu? Wangekaa kimya je
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…