MAOMBI MAPYA YA UMEME YANAWAPA SURVEYORS NAFASI ZA KUOMBA RUSHWA
Niende moja kwa moja kwenye mada Tanesco Kibaha ambayo ndo inawakilisha Tenesco mkoa wa pwani, imejaa ubabaishaji na kuendekeza rushwa. Nasema HILI kwa sababu moja.

Mkoa wa Pwani ni mojawapo ya mikoa ambayo inakuwa kwa kasi sana, lakini pia ni mojawapo ya mikoa ambayo imepitiwa na miradi mbalimbali iliyo chini ya shirika la umeme.

Maeneo nilioko mimi ni maeneo yaliyopitiwa na mradi wa nguzo za zege, mradi umekamilika kabisa, shida ni Tanesco kuaunganishia wateja umeme. Unapopeleka maombi unaambia acha namba ya simu tutakupigia zamu yako ikifika, lakini wakati huo huo unafuatwa na mfanyakazi wa Tanesco na kukwambia kama unataka surveyor wa haraharaka toa laki moja, kinyume na hapo subiri zamu yako.

Kinachofuata hapa ni rushwa ilyogawanyika katika makundi tatu, kundi la kwanza ni laki moja kwa ajili ya Surveyor, kundi la pili ni kupewa mita na kundi la tatu nikuingiziwa umeme ndani.

Swali ni je ni mapato kiasi gani ambayo watumishi wa Tanesco Kibaha wanaikosesha Serikali kwa sababu ya kutaka rushwa ya laki moja?

Ukiachana na mimi nyumba kibao ambazo zimepitiwa na huo mradi hazina umeme na umeme upo, binafsi baada ya kukataa kutoa rushwa sijawahi muona surveyor tangu mwezi wa tisa mpaka leo hii.

Majirani zangu walioamua kutoa rushwa tayari wanao umeme. Mimi nimeapa sitotoa rushwa kwa kuwa ninayo solar yangu na pasi yangu ya mkaa kaeni na umeme wenu, manake hata tukija ofisni ni porojo tupu.
 
Tafadhali onyesha

Jina

Eneo

Wilaya

Simu

Tatizo

Toka lini

Kwa hatua zaidi

Tutumie inbox
 
Tafadhali onyesha

Jina

Eneo

Wilaya

Simu

Tatizo

Toka lini

Kwa hatua zaidi

Tutum
Eneo ni Kibaha, Kwa mfipa kata ya viziwaziwa
Wilaya Kibaha
Tatizo ni kucheleweshwa survey kwa makusudi ili nitoe rushwa.
Toka lini:- nimepeleka form yangu tangu mwezi wa tisa.
Mradi unafahamika make ni mradi wa kwanza wa nguzo za Zege eneo la kwa mfipa maarufu kama Shana Town, fuatilia ni wateja wangapi wameleta maombi na ni wangapi wamepatiwa umeme au kufanyiwa survey.
Jina na namba yangu ya simu siyo lazima, maombi yapo ofisini nirahisi sana kufaham ni mangapi yamefanyiwa kazi na mangapi hayajafanyiwa kazi na kwa nini.
 
Tafadhali onyesha namba ya simu ili tufanyie kazi swala lako?nani kakuomba rushwa?
 
Asante tunafuatilia kwa ukaribu sana swala hili ndugu mteja.




TANESCO Makao Makuu| 0768985100|customer.service@tanesco.co.tz
 
Jina: Shabani Kawina
Eneo: kata msongola, mtaa wa mvuleni
Namba ya simu: 0763531628/0783349834
Kero: Tanesco Emergency Kisarawe kutofika kurekebisha nguzo iliyochimbika chini kutokana na athari za mvua. Aidha, tangu mvua za mwezi oktoba, 2020 mpaka Desemba, 2020 kuna nguzo imechimbika na Hali ilivyo Sasa muda wowote inaweza kuanguka na kuleta athari kwa wananchi tunaotumia nguzo hiyo kupata huduma ya umeme. Kitengo Cha Tanesco Emergency Kisarawe wenye namba ya simu 0655989935 tumekula tukiwapigia simu Mara kwa Mara tangu mwezi oktoba mpaka Sasa Mara kadhaa wamekuwa hawapokei simu, na hata kipindi wanapopokea simu hutoa ahadi ya kuja wananchi tunawasubiri na hawatokei.

Tunaomba Tanesco mje kurekebisha nguzo hiyo Kama kuhamisha kwa kuweka sehemu isiyokuwa na athari na njia ya maji pindi mvua inaponyesha. Thanks.
 
Tumepokea kwa hatua zaidi
 
Naomba kutoa mrejesho. Wataalam wamefika leo hii na kuiweka nguzo sehemu salama tofauti na ilipokuwa awali. Asanteni kwa kutatua kero kwa wakati.
TANESCO makao makuu ndiyo wako serious na utoaji Huduma. Hawa wengine wa ngazi za chini wanahitaji wamulikwe. Yaani Hata maswala yaliyo chini ya mamlaka yao wanasuasua. Nimelipia umeme mwezi unaisha hawajaja kunifungia. Nasubiri ikifika katikati ya January niwashtaki kwa Waziri watumbuliwe kwa sababu wanatengeneza mianya ya rushwa. We are tired of this rotten system
 
Tafadhali onyesha

Jina

Eneo

Wilaya

Simu

Tatizo

Toka lini

Umelipa lini

Kwa hatua zaidi
 
 
Namba ya malipo: 991032233612
Nililipia Tangu tarehe 7 mwezi huu. Nataka itimie siku 30 Kulingana na mwongozo wa TANESCO, nimwage unga wa Watoto wao. Sina huruma nao kwa sababu Hata control number nimeisubiri Tangu mwezi June na wakanitumia mwezi huu baada ya kuomba msaada makao makuu. Wilaya Walinipigia na kunilaumu kwa Mimi kupiga simu makao makuu. Safari hii hatutapiga simu TANESCO makao makuu Bali ofisi ya Waziri wa nishati. Kufungiwa umeme sio hisani ya mtu Fulani Bali ni haki ya kiala Mtanzamia mwenye vigezo[/QUOTE]
 
[/QUOTE]Tafadhali tuma taarifa tulizoomba hata dm
 
@FURY BORN usijibu hili swali
Namba yangu siwezi kuwapa, niwape ya nini? nimeeleza kila kitu namba ya nini? Wampigie meneja wa Tanesco kibaha wamuulize ni kwa jinsi gani mradi wa nguzo za zege kibaha kwa mfipa unaendelea, wateja wangapi wameunganishiwa umeme au kufanyiwa survey, ni maombi mangapi yamechakatwa, na ni mangapi bado na kwa nini.
 
TANESCO naomba kufahamu inachukua mda gani kufungiwa umeme Tangu siku mteja amelipia. Binafsi wiki tatu zimepita toka nimelipia. Naomba kufahamu maximum huchukua mda gani kwa nyumba iliyopo ndani ya mita 20 kutoka kwenye nguzo
 
TANESCO siku tatu zilizopita niliripoti kukatika kwa umeme kila siku hapa Pugu Kigogo Fresh, kila siku lazima umeme ukatike. Jamani tuoneeni huruma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…