Tafadhali onyesha

Jina

Eneo

Wilaya

Simu

Tatizo

Toka lini

Kwa hatua zaidi
Ina maana nyie linapotokea katizo/kukatika kwa umeme kwa muda mrefu na mtu ametaja eneo ni Kimara Bucha/Baruti mnakuwa hamna taarifa za katizo hilo.....yaani system zenu za emergency zikoje....maana hata muda huu pia mmekata tena toka mida ya saa sita mapaka sasa saa nane hamajarudisha umeme na mnaona poa tu....wala taarifa ya kukatia hamjatoa maana kwa huku Kimara Bucha/Baruti ndo imekuwa michezo yenu mnakata na kurudisha pale mnapo jisikia.

Kama kuna mgao wa kisirisiri kwa maslahi yenu si mseme....maaana mnafelisha sana shughuli za kiuchumi😠😠😠😠😠😠😠😠😠😠😠
 
Yaani mkuu kweli kabisa nami niko Kimara na hakuna umeme muda mrefu kweli.....alafu majamaa yamekaaa tu kimya bila kutoa taarifa yoyote....wabaguzi kweli,mbona mitaa ya upanga na oysterbay wakitaka kukata umeme huwa wanawapa taarifa.

Acheni kutuchulia poa wakazi wa Kimara kwa kutukatia umeme hovyohovyo.
 
Nimefungiwa ni mita nadhani ni la mashine ya kiwandani,yani natumia umeme wa elfu 10 siku mbili jamani,nikifuatilia hakuna lolote
 
Nimefungiwa ni mita nadhani ni la mashine ya kiwandani,yani natumia umeme wa elfu 10 siku mbili jamani,nikifuatilia hakuna lolote
Tafadhali onyesha

Jina

Eneo

Wilaya

Simu

Tatizo

Toka lini

Kwa hatua zaidi
 
Mimi nadhani imefika mahali wakazi wa Kimara tutumie njia nyingine ili hawa jamaa watupe huduma endelevu kama kwingineko.
Kimara ina historia mbovu sana ya huduma ya umeme na sijui ni kwanini.Miaka ya nyuma tulisumbuliwa na tatizo la low voltage,tukapiga makelele sana hadi likatatuliwa baada ya miaka mingi sana.sasa tuna hili la kukatiwa umeme hovyo hovyo bila hata sababu.
Kwanini hamuwezi kutuliza mambo bila kupelekeshwa?Mpaka tuandikane humu?Dunia ya sasa kwenye metropolitan places kama Dar mtu akikukatia umeme anakuua kiuchumi.ila TANESCO mna mtazamo wa maisha ule wa miaka 50 iliyopita,even before you existed.ajabu!
 
Umenena vyema kabisa mkuu...Tanesco wanakera sana hasa kwa sisi wakazi wa Kimara.Hawana ubunifu na ufanisi katika utendaji wao kwa upande wa Kimara....tuko karne ya 21 lakini wao wanafanya kazi kama tuko karne ya 18.
 
Umenena vyema kabisa mkuu...Tanesco wanakera sana hasa kwa sisi wakazi wa Kimara.Hawana ubunifu na ufanisi katika utendaji wao kwa upande wa Kimara....tuko karne ya 21 lakini wao wanafanya kazi kama tuko karne ya 18.
Tafadhali onyesha

Jina

Eneo

Wilaya

Simu

Tatizo

Toka lini

Kwa hatua zaidi
 
TANESCO naomba muelewe kitu hiki,kumkatia mtu umeme hata kwa dk 20 tu kwenye dunia ya sasa na majiji kama haya ya Dar ni kuhujumu uchumi wa watu mmoja mmoja na uchumi wa nchi kwa ujumla.
Ifike mahali na nyinyi muone umuhimu wa kutokatia watu umeme hata kwa dk moja.Times have changed.Watu tumeamua kujikita katika shughuli halali za kujenga uchumi wa nchi,tumejiajiri,tunalipa kodi,hatuibi wala kufisadi mtu,kwa jasho jingi mkono unaenda kinywani,but you guys frustrate us.Mnaudhi sana,honestly let me tell you this.
Kama hii line ya Kimara mwisho,wewe TANESCO sema mwenyewe tangu lini tunakimbizana humu na kila baada yamda mfupi tunarudia topic ile ile upya?!uliniahidi almost 5 months ago kuwa mnaboresha huko ili tupate huduma bora,kiko wapi?
Wewe tuliza umeme wangu nnaoulipia kodi niupate,hutoniona nikikusumbua humu.
 
Tafadhali onyesha

Jina

Eneo

Wilaya

Simu

Tatizo

Toka lini

Kwa hatua zaidi
Nyie mnataka jina langu la nini wakati nimeshawatajia eneo na muda wa katizo na katizo bado mpaka sasa.Na mwenzagu wa Kimara pia amekiri kuwa umeme hakuna.Jina na number yangu ya simu ndo vitarudisha umeme au.....hebu acheni kufanya watu wajinga....ina maana hamna taarifa kuwa Kimara hakuna umeme au na baada ya kupewa taarifa mmefanya nini?.
 
Tafadhali onyesha

Jina

Eneo

Wilaya

Simu

Tatizo

Toka lini

Kwa hatua zaidi
 
Tafadhali onyesha

Jina

Eneo

Wilaya

Simu

Tatizo

Toka lini

Kwa hatua zaidi
Eneo ni Kimara Mwisho,ni eneo kubwa naamini haina haja ya kuandika sana,ukitaja Kimara mwisho basi mkazi yeyote wa Dar anapajua.ni Kimara yote haina umeme as we write here na tatizo hili la kukatika umeme ni sugu,kuna mda linatulia hata wiki mbili,then linarudi na kusumbua tena,na inaonekana huwa unatusaidia sana wewe maana tusipokuandikia tukakaa kimya huwa hali inazidi kuwa mbaya.Mientaendelea kukuandikia wewe hadi hukuground hali inabadilike na nakuahidi ikitokea nimekaa miezi miwili umeme haujakatika ntakuja kukuandikia pia huku na kuipongeza TANESCO kimara, i promise you that.
 
Tumepokea taarifa mkuu
 
Ni wiki tatu hadi sasa tangu nilipe gharama zote za kuwekewa umeme wa luku kwenye makazi mapya boma ng'ombe lakini hakuna kinachoendelea, na zaidi tunaambiwa eti kuna tatizo katika bohari kuu ya vifaa Kilimanjaro, na tatizo hilo litachukua wiki mbili, hivi kweli MTU utumie mwezi mzima kuwekewa umeme na umeshalipa kila kitu? Kuna shida gani? TANESCO
 
Taneeco Moshi mjini kitengo cha savey mnajiona kama shirika la baba yenu nimefungua malalamiko mpaka nimeamua kuweka sola kila siku mnadai hamna usafiri mnategemea wateja tufanye majukumu ya shirika au ndio mnasubiri magufuli aongee ndio muanze kumtafuta mchawi acheni kukwamisha juhudi za jpm mama mwenyew na hizi 0754343628 yuko mjini hapo savey anasema tanesco hamna usafiri wateja tugaramie hii ni sawa ?
 
Ukarabatr wa miondo mbinu mlioufanya huku maeneo ya Tandika Kilimahewa/Azimio takriban wiki 2 zilizopita umekuwa mwiba mchungu kwa wakazi wa maeneo hayo.TANESCO walipita kubadilisha nguzo na nyaya za umeme,ila baada ya maboresho hayo umeme umekuwa ukikatika mara kwa mara.Tena cha kushangaza utakuta katika mtaa/eneo kuna nyumba zinawaka umeme na nyingne hazina umeme.Kwa mtazamo wa haraka haraka unagundua walipobadilirsha hizo nguzo na nyaya wameunga laini nyingi pamoja ambazo hapo awali zilikuwa zinajitegemea na hivyo kusababisha njia hizo mpya kuzidiwa hali inayopelekea umeme kukatikakatika.Na pia hata zoezi la kubadilisha nguzo nalo wamelifanya kihuni, kwani wameacha nguzo nyingi mbovu zikiwa zimesimama jambo ambalo ni la hatari endapo zitaanguka maana zinshaoza ile sehemu iliyo chini ardhini.
 
Dah hivi tanesco mtaendelea kututesa mpaka lini huku kigamboni mikwambe kila siku naleta malalamiko hapa naambiwa tu lete taarifa kamili nawapa mnasema asante kisha zikipita tena wiki 2 hali ile ile

Jamani waendesha nchi si mmeshaona hamuwezi hata kuondoa kero ya umeme si muache jamani mbona mnakua ving’ang’anizi wa madaraka.

Hivi mimi nipo mjini tena kwenye population kubwa na miundo mbinu ipo ila umeme kwa siku unakatika mara 20 na kurudi kama vile switch amepewa mtoto achezee

Nchi yangu mwenyewe nina hela yangu niliotafuta kwa jasho langu halali nahitaji huduma tena ya muhimu kama umeme hamuwezi kunipatia

Tuna aina ya serikali ambayo haiwezi kuwajibisha wahusika tanesco kwa huduma mbovu ya kata zima umeme,

Tanesco inaongozwa na viongozi dhaifu ambao wanasimamiwa na viongozi vipofu wasioona umuhimu wa maendeleo ya wananchi kwa kukosa huduma muhimu kama umeme

Hata mufanye project muhimu kiasi gani katika nchii kama umeme ni kitendawili bado mpo hovuo sanna
 
Jana mita ilikuwa na unit 50,umeme ulikata na uliporudi mita ikaonesha hakuna umeme unit 0.
Ebu ni fafanulieni hii inshu,mnaweza rudisha hizo unit au ndo bye bye
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…