Ninashangaa sana umeme almost maeneo mengi hapa nchini unakatwa bila maelezo TANESCO imekaa kimya bila kutoa maelekezo sasa nyie ni shirika la vibatari au kandiri?

Sijapenda kwakweli hii tabia inakera na inaudhi. Hapa Dar es Salaam, nimekwenda Arusha, Moshi, Shinyanga, Dodoma, Mbeya, Mtwara hali ni ileile.

Jirekeibisheni hii si sawa.
 
Upungufu wa kina cha maji katika mabwawa ya uzalishaji umeme
 

Hiyo hali kitaalamu hua inaitwa "mgao wa umeme"
 
Habari wa Wahusika.

Kuna Jirani kaniomba nimsaidie kulifikisha hili lalamiko lake kwenu.

Anadai hili tatizo limetokea wiki sasa na akatoa ripoti Tanesco office Bagamoyo kwa namba hii 0682140405 na akapewa Namba ya Ripoti 890 na ikapita siku 2 ndio wakaja watu wa Emmergency na anadai walipofika waliangalia tu kwa mbali na wakasem hii sio kazi yao.

Wakasema hii sio Kazi yao ni kazi ya watu wa METER , wakasema na wao wataripoti kwa watu wa METER.

Wakaondoka bila kufanya chochote au kugusa chochote.

Sasa zimeshapita siku 4 kimya hakuna aliyekuja wala kupiga simu kwake.

Leo akapiga tena simu kuulizia nini kinachoendelea. Wakamjibu wako busy sana wakipata mda watakuja.

Ivi kweli wako busy wanashindwa hata kushughulikia hiyo meter inayoninginia na kutaka kuanguka ?

Huyu mama ni mtu mzima mwenye hiyo meter inayoninginia hana uwezo wa kutoa pesa kununua meter ingine kama hiyo ikija kuibiwa au kudondoka na kupasuka.

Naomba wahusik fuatilieni hili tatizo mtaliona lisharipotiwa na namba ya kuripoti na 890 nyumba ipo bagamoyo mjini karibia na soko la zamani.

Natumai huyu mama atasaidiwa.

Sikuelewa aliponiambia watu wa Emmergency wamesema kazi sio yao walikuwa wanamaanisha nini ?

Basi si ni bora wangeingoa na kuondoka nayo kama wanaona ipo katika mazingira HATARISHI.View attachment 1687632
 
Tafadhali onyesha

Jina

Eneo

Wilaya

Simu

Tatizo

Toka lini

Kwa hatua zaidi
TANESCO Nyakato Mwanza kuna shida sana yaan nimelipa gharama zote za kuunganishiwa umeme tangu mwezi wa kumi hadi leo hii hamna kitu ukiuliza unapewa majibu mepesi kabisa hawasemi tatizo ni nini.
 
TANESCO Nyakato Mwanza kuna shida sana yaan nimelipa gharama zote za kuunganishiwa umeme tangu mwezi wa kumi hadi leo hii hamna kitu ukiuliza unapewa majibu mepesi kabisa hawasemi tatizo ni nini.
Weka taarifa kamili tafadhali tuone kwenye mfumo wetu
 
Hongereni tanesco kahama mnafanya kazi nzuri sana!!!
Kahama manispaa
 
Tafadhali onyesha

Jina

Eneo

Wilaya

Simu

Tatizo

Toka lini

Kwa hatua zaidi

Tutumie taarifa hizo inbox
Nashukuru sana tatizo limetatuliwa kwa haraka,mbarikiwe sana,hii ilikuwa ni kero ya muda mrefu sana
 
Ahsante kwa taarifa iliyokamilika mpendwa mteja wetu tunaifatilia na mteja wetu atapata huduma mapema zaidi.

Kuhusu emergency kuondoka ni kweli wao wanawajibika kuondoka hatari kama ipo na kutatua kama tatizo lipo ndani ya majukumu waliopewa vinginevyo wanapeleka kwa vitengo vingine vilivyopewa jukumu la kugusa au kutengeza mita
 
Hii namba ya taarifa inaonekana ni ya Mlandizi tafadhali tusaidie namba ya mteja wetu au namba sahihi ya taarifa kwa hatua za haraka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…