TANESCO kimara mwisho kote hakuna umeme usiku huu.
Nilisharipoti matatizo ya kukatika umeme humu nna post hata elfu moja kwamba Kimara kuna tatizo la kipekee la umeme kukatika na haswa line ya dawasco,matangini na tra na maeneo ya karibu.
Ni miaka sasa haipiti wiki bila umeme kukatika.
Tafadhali kama mnashindwa kutuwekea mtambo mpya utakaotupumzisha na madhila haya basi tuhamisheni line.
Lazima kuna shida huko ubungo sio bure.ni muda mrefu tunaripoti lakini miaka sasa!eneo kubwa kama kimara tunawalipa hela ya maana kununua umeme lakini mnakata halafu
ukienda vijijini huko kusikokuwa na matumizi makubwa ya umeme ndiko umeme uko stable.huku ambako tanesco inaingiza hela nyingi sababu ya wateja wenye matumizi makubwa ndio hamututhamini,hakuna huduma bora!
Jiji la dar na vitongoji vyake ndio linaongoza kwa matatizo ya umeme.and yet sisi ndio tunasababisha nyie muendeshe shirika lenu kwa mchango mkubwa kutokana na matumizi yetu.Msipoiweza Dar mtaweza wapi?!vipaumbele vyenu ni vipi?!mko bize kusambaza umeme vichochoroni huko lakini hapa penye uhitaji mkubwa wa umeme hapana huduma bora,mnaharibu kazi za watu kila siku!
Hivi nyinyi hamuishi huku mitaani?!hii kero hamuioni?!
Huu ni mchezo gani miaka tangu 2012 wimbo ni huu huu?!
Aliyeiroga hii nchi sijui katumia uchawi wa wapi!aibu na inasikitisha sana.
Sawa tanesco,mie ntafunga biashara zangu ntanunua costa niehamishie hela yangu kwenye petrol maisha yaendelee.sijui nyinyi mnafaidika nini na huu upuuzi mnaoendelea nao!huu ni upuuzi!ni umaskini wa kichwani mnao huko!kila siku tanesco tanesco tanesco!hovyo kabisa nyinyi!