Naambia hapa mkekuwa na Tabia ya kukata umeme katavi town bila kutoa taarifa tanesco katavi mungu anawaona
 
TANESCO, kwanini mnakatakata umeme sana huku Kigamboni mpaka nakosa raha ya kukaa huku? Mnatuchukuliaje hasa aisee? Mnakata as if hatustahili kupewa notisi kabla ya kukata umeme?
Kwa kweli huku Kigamboni wamezidi halafu ni kila siku.... imagine leo tu tangu asubuhi wameshakata mara tatu na hadi muda huu hakuna umeme wanaboa sana
 
Tokea tupate uhuru inakimbilia miaka sitini sasa,hivi kweli hadi leo hii mvua ikinyesha inakua shida ya umeme kasi hiki?
Naishi Kijichi tangu usiku wa jana hadi leo umeme unakatikakatika tumeshindwa hata kufanya shughuli zetu za kutuingizia pesa, leo tokea asubuhi ni hivyo hivyo nimetoka huko Kijichi nipo Mwananyamala jioni hii tunaangalia game ya simba kipindi cha mapumziko umeme umekatika!

Hivi shida ni uloa au tunatumia sola?ama ni hofu ya radi?kama hivyo ndivyo ilivyo kwanini hakutafutwi suluhisho?kwa hali inavyoendelea ni wazi hata mradi mkubwa wa nyerere utakapokamilika shida hii tutaendelea kua nayo

Ombi tu tunaomba kitengo cha habari maelezo TANESCO muwe mnatupa taarifa ya kinachoendelea na sababu na muda wa kurudi huduma.

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
TANESCO MOROGORO HAMUELEWEKI tumeomba kuingiziwa umeme zaidi ya mwaka sasa kila tukienda majibu ni yale yale hakuna nguzo na wako wengine wameomba kuingiziwa inakaribia miaka 2 sasa shirika linajiendeshaje kama watu wa kulifanya shirika liendelee hawapati huduma hiyo nyumba za jirani ziliingiziwa umeme zamani naulizia hata kuchukua umeme wa jirani kuleta ndani nasikia mmekataza sasa si mnapoteza hela wenyewe jamani kituo ni TANESCO Turiani wilaya ya Mvomero nshachoka kufuatilia kwa kweli nawekeza kwenye solar power tu
 
kuna mtu amejiunganishia umeme huku mtaani kinyume na taratibu.. jeh mnawezaje kumfikia lakini nisijulikane maana mi n mpangaji wake
 
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tafadhali tusaidia taarifa kamili ili tuweze kufanyia kazi taarifa zako

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja
 
kuna mtu amejiunganishia umeme huku mtaani kinyume na taratibu.. jeh mnawezaje kumfikia lakini nisijulikane maana mi n mpangaji wake
Tunashukuru kwa taarifa tafadhalo tupatia taarifa inbox ikiwemo namba yako ya simu mara baada ya kudhibitisha ipo zawadi
 
Kwa kweli huku Kigamboni wamezidi halafu ni kila siku.... imagine leo tu tangu asubuhi wameshakata mara tatu na hadi muda huu hakuna umeme wanaboa sana
Kigamboni tupo hatua nzuri ya ujenzi wa kituo cha kupoza umeme kikikamilika hivi karibuni huduma itaimarika
 
Tafadhali weka maelezo zaidi nini tatizo? Wilaya gani? Namba ya simu na ilikuwaje
 
Wakazi wa Tambani, Wilaya ya Mkuranga tunahitaji kuwekewa umeme

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tafadhali tusaidia taarifa kamili ili tuweze kufanyia kazi taarifa zako

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja
 
Tanesco Jamani hivi huku kukataa kuingia kwa units mpya baada ya kununua nini shida? yani unakuta unahangaika weeee ndo badae ushalala unaingia
 
Mzee wangu (baba) aliomba huduma ya kuunganishiwa umeme katika ofisi zenu za tabata liwiti-Dar es salaam tangu October mwaka jana 2020. Alijaza fomu na kuirejesha ofisini akaambiwa asubirie surveyor kufika site. Mpaka leo hajawahi kufika. Kwa sasa mzee anaumwa hawezi kufuatilia,juzi wiki moja iliyopita nilikuja dar kumsalimia mzee ikabidi niende kufuatilia,nikaambiwa tumeiweka kwenye list yetu, Jumamosi(tarehe 10/04/2021)tutakuja hapo. HAWAKUJA.

JINA: CHRISTIAN O.M
SIMU:+255744656545
SITE ILIPO: tabata-chang'ombe eneo la Mwembeni stand palepale.

Naomba msaada maana mzee hawezi kufuatilia kutokqna na afya yake. Hapo juu ni mawasiliano ya mzee na site ilipo.
 
TANESCO je, kunautaratibu wowote wa kufata ili kubadili matumizi ya umeme kutoka makubwa hadi madogo?.
Harafu je, kwa nini matumizi hayo hujibadili mfano kutoka matumizi madogo hadi makubwa pasipo taarifa?

Majibu tafadhali πŸ™πŸ™πŸ™
 
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tafadhali tusaidia taarifa kamili ili tuweze kufanyia kazi taarifa zako

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja
Habari,

Nipo Nyamongo wilaya ya Tarime Meter yetu Na 37210065324 inakula Sana umeme tofauti na matumizi yetu imagine umeme wa 5000 Tsh tunatumia kwa siku tatu umeisha na hamna friji,au vitu vinavyokula umeme Sana na Taarifa awali nishatoa Tanesco Tarime mwaka Jana wanakaniambia nirekebishe mfumo wa umeme yaani wiring fundi wao akaja akarekebisha mfumo wa umeme tukampatia Ela ya ufundi na kutuambia tujaze umeme tutumie ndani ya miezi mitatu matumizi yatabadilika Ila mpaka saivi hiyo miezi imepita hayajabadilika na badaye tulivyomwambia ndo akasema tulipie Ela sh 150,000/= kwa ajili ya kubadilishiwa hiyo mita labda tatizo litakuwa hilo Kuna shida gani hapa Kwan hizo mita mpaka utoe Ela kiasi hicho ndo unabadilishiwa mita?
 
Pole sana mpendwa mteja wetu tafadhali onyesha namba ya simu tukusikilize zaidi JM.
 
TANESCO je, kunautaratibu wowote wa kufata ili kubadili matumizi ya umeme kutoka makubwa hadi madogo?
Harafu je, kwa nini matumizi hayo hujibadili mfano kutoka matumizi madogo hadi makubwa pasipo taarifa?

Majibu tafadhali πŸ™πŸ™πŸ™
Pole sana mpendwa mteja wetu tafadhali onyesha namba ya simu tukusikilize zaidi JM
Pia na mimi naomba majibu hapo juu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…