Napatikana mbagala kongowe A mzinga tatizo langu siku ya tatu leo nalal giza umeme auwaki luku inasoma hipo lakini umeme auwaki tatizo ni nini arafu nilikuwa naongeza luku nikajua imeisha inasomaa arafu aimarizi inazima leotena nimejaribu ile tokeni naambiwa umeshatumika tumika lakini umeme auwaki
 
TANESCO nimenunua umeme wa laki moja badala wa elfu 10,je naweza kurudishiwa fedha , naomba msaada wa haraka,
 
TANESCO naomba kujua hatma ya tokeni tulizonunua ktk mita ya zamani ambayo iliharibika, baada ya batani zake kugoma kubonyezeka. Sasa imefungwa mpya.

Inamaana tokeni zilizonunuliwa ktk mita ya zamani hazitatumika tena?
 
Umeme unakatika sana siku hizi hatujui shida ni nini. Ni maeneo ya Tabata karibia yote kuanzia Bima hadi Segerea na Kinyerezi. Mchana kutwa hamna umeme. Pia usiku angalau kila siku hukatika na kurudi baada ya saa1, masaa 2 nk. Kuna shida yoyote?
 
Inaelekea Kuna mnachokitaka kingine sio kutukatia umeme tu. Semeni tuwape. Tanesco ya magufuli vs Samia
 
NI UMBALI KIASI GANI (metre) MNASHAURI UJENZI WA NYUMBA UANZIE HAPO TOKA KWENYE NGUZO KUU (LAINI YA TRANSFOMA)?
 
TANESCO leo jpili watu wako ibadani mmekata umeme Kimara mwisho!
Hivi haya malalamiko mengi nnayosoma humu hasa ya wakazi wa Dar hamuyaoni?

Niliwauliza kuwa kama hamuwezi kuihudumia Dar es salaam vizuri, legitimacy yenu kuitwa shirika la umeme Tanzania iko wapi then? maana huu ndio mji wa mfano.

Huwezi kushindwa kuihudumia Dar ukatudanganya unaweza kuihudumia Kigoma.Hamna kitu hicho.
Ilipaswa kuwa kosa la jinai umeme kukatika Dar.Lakini soma malalamiko humu,majority ni sisi wakazi wa Dar!

Ndio watumiaji wakubwa zaidi wa umeme,tena tunautumia kuzalisha mali, iwe jtano iwe jpili, lakini hamtuheshimu, mnakatakata umeme hovyo hovyo na mko consistent kwenye hilo!mko imara katika jambo lililo kinyume na kazi yenu. Huu ni uhalifu.

Mimi pekee soma post zangu kuhusu ukatikaji wa umeme kimara mwisho pekee, ni miaka na miaka nalalamika, lakini hadi leo nipo hapa bado natoa taarifa kila baada yamda mfupi.siwezi kukaa wiki mbili kabla ya kukerwa na umeme na kuja humu.Inashangaza sana.
 
Tumepokea taarifa wataalamu wetu wanaendelea kufanyia kazi tatizo lilitokea eneo la Mbezi na Kimara huduma itarejea.Tunawaomba radhi sana
 
Dah mbona haya makato yamezidi leo nimenunua umeme wa 10000 matokeo yake nimepata unit 22 tu na mwanzo ilikuwa 28 unit,
Na Tanesco naomba ufafanuzi jinsi gani nitarudishwa kwenye Tarifu 0 maana hii imekuwa too much nahapa ni kijijini mnatuuzia umeme zaidi ya sh. 300 kwa unit
 
Ndugu mpendwa Mteja wetu!

Kama ambavyo Serikali ilivyotangaza kuwa kodi ya majengo italipwa kupitia manunuzi ya umeme hivyo basi kwa sasa wateja wanalipia kodi ya Mwezi wa Saba (Tsh 1000) na Mwezi wa nane (Tsh 1000) sawa na kiasi cha Tsh 2000 kwa mwezi huu, baada ya mwezi huu wateja wetu wataendelea kukatwa Tsh 1000 tu kwa kulila malipo ya kwanza ya mwanzo wa mwezi

TANESCO HUDUMA KWA WATEJA

Makao Makuu
 
Na hilo la kurudishwa tarifu 0 maana umeme tunanunua bei juu na hapa ni kijijini naomba ufumbuzi wa hili maana nilimsikia hata waziri akisema umeme usiuzwe zaidi ya sh. 100 kwa 1 unit
 
TANESCO haraka sana eneo la Kijichi mwanamtoti karibu na msikiti wa isticama kuna transfoma inaungua taratibu. Umeme eneo hilo unawaka na kuzima unaweza kusababisha hasara kwa watumiaji. Maarufu kama kwenye "matenk"
Your browser is not able to display this video.
 
SHIKRIKA LA UMEME TANZANIA TANESCO MKOA WA MOROGORO.

TAARIFA YA KUOMBA RADHI KUKOSEKANA KWA HUDUMA YA UMEME BAADHI YA MAENEO YA MKOA WA MOROGORO.

Shirika la umeme Tanesco linaomba radhi wateja wetu wanaotumia laini ya Tungia,Mzinga,Kilosa,Mikese kwa kukosa huduma ya Umeme usiku wa kuamkia leo kutokana na changamoto zilizojitokza:

Siku :Jumanne.
Tarehe 31/08/2021.

Sababu :hitilafu iliyosababisha kosekana kwa huduma ya Umeme Usiku wa kuamkia leo kutokana na changamoto iliyojitokeza wakati wa kuunga trasfoma kubwa la Msamvu.

Maeneo yanayokosa umeme ni Tungi,Mikese,Mzinga,Mkambarani,Mgeta,Mlali,Tandali,Maguruwe,Area 5&6,Kola A&B,Wilaya yote ya Kilosa yote Kilosa ,Wilaya ya Morogoro vijijini.

Juhudi zilizofanyika team imeanza kurejesha huduma ya iii meme baadhi ya Maeneo mengi ya Mji kupitia transfoma hilo na sasa Tunaendelea na kuunga laini zilizokosa umeme usiku wa kuamkia leo .

Tunaomba radhi sana kwa usumbufbcu utakao kuwasa umejitokeza.

Tahadhari usishike wala kukanyaga nyaya zilizolala chini yoa taarifa Emergency Tanesco Morogoro kipitia namba 06770630010684>89272 tutakufikia .


imetolewa na :
Ofisi ya Uhusiano huduma kwa wateja Tanesco Morogoro.

31/08/2021.
 
Ni mwezi mzima sasa Morogoro tunashida ya umem na hakuna taarifa kwa umma
 
Tanesco mtuoe muongozo tafadhali, surveyor kaja site MLANDIZI KIBAHA 12/7/2021. Mpaka leo sijapata control no nikimuuliza anasema wanasubiri budget ndio watoe control no. Je huu ndio utaratibu na lini hiyo budget inategemewa kupitishwa?
INAUMA SANA UNA HELA MFUKONI HALAFU UNALALA GIZANI
 
Tafadhali onyesha namba ya simu kwa hatua zaidi
 
Nimeuliza swali ya tatu hii na hakuna majibu. Je kweli mmesoma mkakausha.

Niliuliza ensapo nina mita 3 za luku kwa jengo /plot moja ninalipiaje? Kwa kuchagua mita mojawapo au ni zote?

Kitu ambacho kitakuwa kulipia mara 3 jengo moja!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…