Habari, hatujapata muongozo kuhusu umeme wa 9,150 baada ya kuingiza Kodi ya majengo. Kwa Sasa ukinunua tunapata unit pungufu ya 75. Tununue umeme wa shilingi ngapi bila kuathiri masharti ya units 75 kwa 9,150
 
TANESCO hebu angalia wewe mwenyewe frequency yangu ya kuja humu kuripoti matatizo ya kukatika umeme Kimara Mwisho.

Hii iwatambulishe mlioko makao makuu ukubwa wa tatizo la umeme Kimara. Kila baada ya siku moja mbili niko humu!Hebu vaa viatu vya raia wa Kimara uone jinsi wanavyoharibikiwa shughuli zao za uzalishaji mali kwa kadhia hii.

Ni nini hiki mnachofanya kisichoisha miaka na miaka kila siku?
Laini inayotoka Ubungo kuja Kimara upande wa Dawasco na TRA ndio worse kabisa.

Hebu niambie hii line ina tatizo gani kwani lisiloisha?
 
Kila nikinunua umeme unagoma kuingia,CIU inaandika sleep, nikiingiza 0/namba ya mita/0/namba ya mita inaandika good halafu nikiingiza token inaandika error 77 tatizo mini?
 
Kila nikinunua umeme unagoma kuingia,CIU inaandika sleep, nikiingiza 0/namba ya mita/0/namba ya mita inaandika good halafu nikiingiza token inaandika error 77 tatizo mini?
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tafadhali tusaidia taarifa kamili ili tuweze kufanyia kazi taarifa zako

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo
Namba ya Mita
Toka lini

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja, JM
 
Soma PM yangu ndugu Tanesco unipe msaada kwa haraka. Nashukuru sana ndugu TANESCO.
 
Kuna kijiji kinaitwa Nyakunguru, wilaya ya tarime vijijini mmeweka umeme kwenye kitongoji kimoja tu ,vitongoji vingine vitano vilivyobaki vipo gizani . mpango kazi upoje
 
Habari, hatujapata muongozo kuhusu umeme wa 9,150 baada ya kuingiza Kodi ya majengo. Kwa Sasa ukinunua tunapata unit pungufu ya 75. Tununue umeme wa shilingi ngapi bila kuathiri masharti ya units 75 kwa 9,150
Walinipa muongozo, kwenye hiyo 9150 unaongeza na kodi ya nyumba 1000 au kama unadaiwa zaidi unaweka kiasi ambacho unadaiwa ili kusudi wakishakata madeni yao wewe ubaki na kiasi kisichozidi 9150.
 
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tafadhali tusaidia taarifa kamili ili tuweze kufanyia kazi taarifa zako

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo
Namba ya Mita
Toka lini

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja, JM
Acheni uhuni nyie Tanesco!
Kwani hamnaga system inayowaonyesha matatizo! Na kama sivyo hamumuamini mteja anapotoa taarifa. Je mnajua huu ni moto sasa msipochukua hatua mkisubiria taarifa ya majina ya Wadena na simu zao huu ni kutukuwajibika!. Je kama kuna hitilafu mahali mitambo haitoa taarifa!?
Acheni hizo!
 
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tafadhali tusaidia taarifa kamili ili tuweze kufanyia kazi taarifa zako

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo
Namba ya Mita
Toka lini

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja, JM
Malalamiko ya huku tabata mwananchi mnayo lakini? je, mnataka kutuunguzia vitu au mnataka kutuunguza wananchi?, Umeme unasumbua Kutoka ahsubh Umeme inapungua na kuongezeka, Umeme hauwezi kawasha hata redio, Hivi ni kweli kwamba sasahivi mmekuwa na kazi ya kuboa wananchi Kila secta? Mmetoka kuweka tozo kwenye kulipia Umeme kwa njia ya luku basi tuacheni tupate huduma Bora, Kwanini mnatufanyia hivi?
 
Walinipa muongozo, kwenye hiyo 9150 unaongeza na kodi ya nyumba 1000 au kama unadaiwa zaidi unaweka kiasi ambacho unadaiwa ili kusudi wakishakata madeni yao wewe ubaki na kiasi kisichozidi 9150.
Nashukuru kwa ufahamu,

Tanesco hoja inhitaji hitimisho lenu. Mbona hoja zingine mmejibu? Au hii Haina mashiko
 
Habari Tanesco.

Mkoa-Morogoro
Wilaya - Morogoro mjini
Kata -Mkundi

Tatizo
Zima washa zima washa wa umeme takribani wiki nzima, iwe usiku iwe mchana.

Hatari na madhara
Kuunguza vitu
Kutokufanya biashara

Ombi
Shughulikieni tafadhalini.
 
Hali hii huku kwetu imekuwa ya kutisha yaani umeme unakatika zaidi ya mara Tatu kwa siku na hakuna taarifa yoyote tunayopatiwa

Sielewi tatizo ni Nini huko tanesko, bora watangaze kuwa Kuna mgao wa umeme tujue moja kuliko kurushana roho, huku wakijua kwamba umeme ndio kila kitu

Kwa kweli hali hii ikiendelea hivi uchumi wetu utakuwa katika hali tete Sasa

Nahisi tunarudi zama za jk.
 
Jana huku tabata utasema kulikua na mtoto wa manager wa tanseco amepelekwa akachezee zile switch maana umeme ulikua unawaka dk tano ya sita umezimwa, unawaka unazimwa kwa siku nzima mpk jioni ndio ukatulia. Mtu unaona uzime vitu vyako visije ungua
 
Sehemu Pekee Inayopata Pata Cha Mtema Kuni Ni Morogoro.

Kila Siku Giza Tangu Kituo Cha Msamvu Haa Hawasemi Watakamilisha Lini Ukarabati
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…