Mbona mimi nimejaza form toka tar 5 September mpaka leo hata control namba sijapata kwa ajili ya kulipia na nipo ya mita 30. Kuna nini hapaTunaposema ndani ya siku kadhaa haina maana mpaka zifike hii ni kuruhusu waliolipa mbele yako kupatiwa huduma ndio tukufikie wewe
Ahsante kwa taarifa tumepokea kwa hatua zaidiTanesco transfoma lenu linawaka moto kwenye bush kila siku mafundi wanakuja wanazima na mchanga na kuondoka lakini tatizo haliishi tumechoka inahatarisha usalama wetu kila leo.wahusika ni Tanesco Chanika
Eneo ni majohe bwera transfoma njia panda ya merlin sina haja ya kuandika maelezo mengine tunaomba lifanyiwe kazi 0625556661
Ahsante kwa taarifa tumepokea kwa hatua zaidiJina Henry Juma lusoba
Eneo Tegeta Boko Chasimba
Wilaya Kinondoni
Namba ya simu
0687 482196
Tatizo ni kutokufungiwa umeme kwa muda tumekamilisha malipo toka Julai 02 lakini mpaka leo bado hatujafungiwa umeme kila mara tunaambiwa wiki hii haishi,naomba msaada tafadhali tumechoka maanà ni miezi mitatu sasa inaenda kukamilika toka tumelipia.
Kwanini mnapokea tu lakini hamtupi mrejesho? Maana hapa majibu kama haya yanatolewa lakini tatizo lako huambiwi limefikia wapi na linatarajiwa kufanyiwa kazi lini.Ahsante kwa taarifa tumepokea kwa hatua zaidi
Utaupata usiwe na shaka ndio kwanza tumepokea lazima tutakupigia simu na kufanyia kazi taarifa zakoKwanini mnapokea tu lakini hamtupi mrejesho? Maana hapa majibu kama haya yanatolewa lakini tatizo lako huambiwi limefikia wapi na linatarajiwa kufanyiwa kazi lini.
Ahsante sanaUtaupata usiwe na shaka ndio kwanza tumepokea lazima tutakupigia simu na kufanyia kazi taarifa zako
Jaribu kuzima Fridge siku moja uone kama ndio inashida. Angalia pia vifaa kama pasi, mara nyingine husahaulika kuzimwaNaomba mawazo yenu kwa tatizo hili: natumia unit 8 kutwa.
Nina frigdge moja ndogo, taa energy saver kama 5 zinawaka saa 12 a day, tv mbili zinatumika kama saa 5 a day, . Nadhani unit 8 a day huu ni umeme mwingi ninao tumia.
Tatizo linaweza likawa wapi? Nimeleta fundi akacheki wiring akasema iko vizuri.
Ushauri tafadhali.
Asante
Mimi kwangu surveyor alikuja toka 28/04/2021 nipo ndani ya mita 45 panahitaji nguzo moja ila mpaka leo TANESCO hawataki kunipa control number, sasa sijui hizo siku 60 zinaanza kuhesabiwa kuanzia kwa surveyor au kuanzia siku uliyopewa control number.Kwa mujibu wa mkataba wa huduma kwa wateja mteja aliyepo ndani ya mita 30 kutoka kwenye nguzo itakayomuunganishia umeme anapaswa kufungiwa umeme ndani ya siku 30 za kazi, mita zaidi ya 30 hadi 100 ndani ya siku 60 za kazi na zaidi ya mita 100 ni ndani ya siku 90 za kazi
Kazi iendeleeTANESCO MPYA IMEZALIWA LEO, TUNATAKA IENDESHWE KIBIASHARA- Waziri Makamba
Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba amesema ni wakati sasa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO kuanza kujiendesha kibiashara, kwa ufanisi ili kuchangia uchumi wa Taifa.
Mhe. Makamba amesema hayo leo Septemba 26, 2021 wakati akizungumza na Mameneja wa TANESCO wa ngazi ya Kanda, Mikoa, Wilaya na Makao Makuu.
Aidha Mhe. Makamba amewatambulisha Wajumbe wa Bodi ya TANESCO wakiogozwa na Mwenyeki, Bw. Omari Issa, pamoja na Mkurugenzi Mtendaji, Bw. Maharage Chande, walioteuliwa Septemba 25, 2021 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Wajumbe wa Bodi ya TANESCO waliotambulishwa ni pamoja na Bw. Nehemia Mchechu, Bi. Zawadia Nanyaro, Bw. Lawrence Mafuru, Mhandisi Cosmas Masawe, Balozi Mwanaidi Maajar, Mhandisi Abdallah Hashim, Bw. Abubakar Bakhresa na Bw. Christopher Gachuma.
Mhe. Makamba amesema Bodi iliyochaguliwa ina wajumbe kutoka nyanja mbalimbali na watasaidia Shirika kufikia malengo.
"Tunataka baada ya miaka mitatu Shirika liingie katika orodha ya mashirika bora, yenye thamani na yanayoheshimika Afrika" alisema Mhe. January Makamba
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO, Bw. Omari Issa, amesema atahakikisha Bodi inafanya kazi na kutimiza malengo yake kwa kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa malengo na uwajibikaji.
Mkurugenzi Mtendaji, Bw. Maharage Chande, ameeleza vipaumbele ambavyo ni masilahi ya rasilimaliwatu, Wateja wa Shirika na utekelezaji wa mipango, hivyo ameomba ushirikiano kutoka kwa wafanyakazi wa TANESCO.
"Nimhakikishie Mhe. Waziri tutahakikisha tunarudisha heshima ya Shirika na ufanisi kupitia ushirikiano wenu, hakuna Shirika lolote linalotoa huduma ya umeme zaidi yetu sisi, yamkini tuwape wateja wetu huduma wanayostahili", " alisema Bw. Maharage Chande
Meneja Mwandamizi Rasilimaliwatu, Bw. Francis Sangunaa, aliwahakikishia viongozi ushirikiano kwa niaba ya wafanyakazi wa TANESCO.View attachment 1954139View attachment 1954141View attachment 1954142
Ndugu mteja,Habari ndugu Admin naomba kujuzwa gharama zaku ongeza meter ya luku katika nyumba ambayo tayari ina meter, Nipo Ilala bungoni vilevile naomba kujuzwa taratibu gani ni fwate na kipi na kipi kina hitajika ili kukamilisha mchako na itachukua siku ngapi mpaka kua tayari?
Sent from my SM-G9550 using JamiiForums mobile app