Usiku huu umeme umekatika zaidi ya Mara 5.
Unawaka unazima ,unawaka unazima,
Samia umezidi upole watu wa tanesco wanakuchezea
 
Najua Waziri husika huenda hata hajishughulishi na UMEME KUKATIKA ila tusaidieni jamani Umeme unakatika wiki YA Pili sasa mnarudisha masaa mawili tu samaki wanaharibika siwezi kuwasha Jenerator Usiku nikifunga ofisini angalau mchana naliwasha mtaji unapotea samaki wanaharibika kwenye friza jamani, biashara imekua ngumu hii bila Umeme najua waziri husika kauli zake ni "TUKO KWENYE MCHAKATO" mara "TUNAHANGAIKIA" ila hakuna lolote litafanyika ITAPITA MIAKA anasema ivo ivo, kwa mtazamo wangu tunaoteseka ni sisi wajasiriamali huenda waziri yeye hata hajui kama kuna mgao wa umeme na ajabu pengine nahisi anasema UPO WA KUTOSHA UMEME NA KUUZA NJE YA NCHI, nakumbuka Rais Magufuli alisema alimtoa nafasi yake kwa sababu alikuwa kila akimuagiza Azuie matumizi ya "RAMBO" alikuwa mzito kutoa uamuzi zaidi ya nusu mwaka Rais akawa anamkumbusha kuwa azuie mifuko ya RAMBO yeye akawa anasema Tunashughulikia tu mpaka Rais alipoamua Kuchukua hatua Mwenyewe.
 
Tulitegemea Bwawa la Nyerere, kwa ajili kufua umeme, lingejazwa maji mwezi huu wa 11/2021, haijawa hivyo ati hakuna winch ya kubeba milango ya kuziba mto uliochepusha maji. Kwa msingi huo hata mashine za kufua umeme hazitaweza kusimikwa!! Imekuaje kampuni isiyokuwa na winch ipewe kazi hiyo!!

TANESCO mtupe majibu yenye ukweli mtupu, la, tuamini ni mwelekeo wa kifisadi na hivi kuna ukame tutetegemee mgao wa umeme na biashara ya majenereta.

KAZI IENDELEE[emoji848]
 
Hivi huu umeme unaokatwa kutwa nzima nchi nzima tatizo ni nini na hali hii itaendelea mpaka lini
 
Tanesco achen kutuhujum mnakataje umeme usku ..?
Si mngekata mchana tu..! Usku Ni hatari Sana
 
Huku moshi kilema umeme umekatika tangu asubhi ukarudi saa 12 jioni na sasa HIV saa 7 umeshakatika
 
Kwa tuliopo hapa Dar hatuna umeme hatuna maji! Yaani uchumi wa kati sijui wa juu Serikali kweli hawalioni hili?

Kwanini kusiweko bajeti mkakati kukwamua hali hii. Wizara na waziri wahusika hebu mjitokeze mguambie bila kupepesa na kudanganya.

Vyanzo vya maji vipo hakuna utaalamu?

Joto litukaange hata kuoga iwe shida.
 
Ahsante mama SSH kweli Nchi imefunguliwa.

Tanesco sawa tumekubali kimya kimya kua Kuna mgao japo Makamba hutaki kulisemea hili.

Mnakataje umeme usku ?Kateni mchana Basi usku Ni hatari kabisa Mnatengeneza mabomu mtaani yanalipuka tu..vibaka tutakabwa sana ,uporaji ,wezi ,ujambazi ndo mda wake huu...!

Kuna jamaa mwezi wa tano aliniletea Generator kubwa analiuza laki mbili sikumzingatia ila tangu juzi namtafuta kwa namba yake hapatkani apa Ni kujipanga.

Viatu vya Kalemani Ni oversize Makamba vaa soksi nyingi.
 
Cjui munaona raha gani kuwatesa wananchi!!!! Yani ninyi dawa yenu rais dikteta labda mutajirekebisha,, lakini huyu mama kwa upole wake mtamsumbua mno.
 
Tuliandika barua na tukajiorodhesha wananchi zaidi ya kaya 130 kuomba kupatiwa huduma ya umeme tukaipeleka kwenye Ofisi ya TANESCO wilaya Missenyi mkoani Kagera lakini huu ni mwaka wa pili na miezi kadhaa hatujawahi kujibiwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…