TANESCO mimi niko Wazohill sio mbali sana na Twiga cement Wilaya ya kinondoni, nipo kwenye tarrif 4 kwa kawaida nikinunua umeme wa 5000 huwa napata units 41 ila muda mwingine wananipa units 36 sijajua tofauti hii inasababishwa na nini kama naibiwa au kuna ndio utaratibu!

Naomba msaada wenu mnieleweshe katika hili.
 
TANESCO
Majibu yanatakiwa waje watu wao wakina Public Relations Officers {PRO} Badra Masoud.
Na wengineo wengi waliopo mikoani na wenyewe waje wajibu majibu ya wananchi, kwanza tunashukuru kwa kuondoa Services Charges iliyokuwa inakatwa kila mwezi.

Swali langu je? Naweza kununua umeme wa mwaka mzima kama matumizi yangu ni Units 56.2 kwa mwezi, naweza nunua Units
56.2*12=674.4
Maana kipindi cha services charges siku ukilipia unakuwa na faini fulani nijulishe apo wadau wenzangu wa Luku Tanesco
 
NMECHOKAAA NMEUMIZWA SANA NA KADHIA HIII


Tanesco sasa yapita miezi6 toka nmelipa gharama za kuunganishiwa umeme. Naombeni ajibu.

Nmelipia tare16/10/2016 mkaniambia ndani ya siku 90 sasa hivi sijui niwaeleweje. Nmeshaenda TANESCO Himo mara10 wananizungusha, like kama wanatengeneza mazingira ya kupewa rushwa na mimi sio MTU wakutoa rushwa kwenye huduma inayostahili kupewa
 
Asante kwa kuanzisha Uzi huu ili tuwafikishie malalamiko na matatizo yetu.

Mimi naishi kitongoji cha Kapugi kilichopo Wilaya ya Rungwe. Ili uweze kufika huku unafuata njia ya Ndembela kuelekea kisumba, kagwina, masebe then kapugi. Katika njia hii tunashukuru mmetuwekea nguzo za umeme phase 3 lakini tangu mziweke tumekuwa tukisubiri kuwekewa nguzo ndogo kwa ajili ya kuunganisha umeme majumbani lakini kumekuwa kimya kwa muda mrefu sasa.

Kuna tatizo gani? Ina maana hamkujipanga kuleta umeme huku hadi sasa tumeanza kuumizwa na matumaini. Tafadhali twaomba mkamilishe zoezi zuri na muhimu kwa maendeleo katika eneo hili.
 
Mkuu pole sana najua kadhia unayopitia ila naamini suala lako limeshafika kunakohusika
Inakatisha tamaa sana
Bado hizi Enzi za JPM, kunataasisi zinatumia lugha zile za kuzungushana tu. Ingekuwa kunakurushiwa hela ningeenda kuchukua hela yangu
 
Mimi niko kwenye nyumba ya kupanga, tunatumia units 42 kwa saa 24 hivi hii iko sawa kweli? Au Kuna shida mahali sisi hatuujui, matumizi ni ya Kawaida tu ya majumbani
 
Mimi niko tarrif 4 mwezi uliopita nili nunua umeme wa sh 9,500/- kwa M-pesa nika pata unit 73.6 mwezi huu nimenunua 9,500/-
nimepata 73.90 Units ina maana nitaamishwa kwenda tarrir 4
Mkuu mbona mimi 10000 napata units 28 tu wewe unafanyaje unapewa units nyingi hivyo? Kwa 9500 tu
 
Mimi niko kwenye nyumba ya kupanga, tunatumia units 42 kwa saa 24 hivi hii iko sawa kweli? Au Kuna shida mahali sisi hatuujui, matumizi ni ya Kawaida tu ya majumbani
Duuh pole mkuu kuna mtu atakua na mashine kubwa kubwa ndani kwake.

Fanyeni msako nyumba hadi nyumba
 
Duuh pole mkuu kuna mtu atakua na mashine kubwa kubwa ndani kwake.

Fanyeni msako nyumba hadi nyumba
Mpaka nataka kuhama mkuu maana Kuna changamoto ya umeme vibaya, yaani unatoa 15k kwa mwezi alafu umeme wenyewe bado wamashaka
 
Mkuu mbona mimi 10000 napata units 28 tu wewe unafanyaje unapewa units nyingi hivyo? Kwa 9500 tu
Wewe upo Tariff 1 ndio maana. Kama matumizi yako hayazidi 75 Units kwa mwezi nenda TANESCO uhudumiwe.

Lakini hayo matumizi lazima iwe ni kila mwezi ukizidisha tu hapo Automatically unarudishwa T1
 
Mpaka nataka kuhama mkuu maana Kuna changamoto ya umeme vibaya, yaani unatoa 15k kwa mwezi alafu umeme wenyewe bado wamashaka
Mkuu nishawai kukutana na hili tatizo mwanzo nilikua natoa elf 10 kwa mwezi maana nilikua naondoka asbh narudi jioni weekend nilikua nakaa muda mchache sana home baada ya muda ikafikia natoa elf 25 hadi 30.

Tukamuomba mwenye nyumba akafunga vimita vidogo kwa kila chumba, kuna watu walikua na rice cooker, wengine majiko wanachemsha maharage mbaya na mafreezer ndo waliokua wanatuliza.

Hata hapo kwako kutakua na watu wanamajikoya umeme au wanagandisha barafu
 
Ref 4C16HQI03W
04140663875
Rcpt MAXCO33EMDB20244131
Units 28.1KWH



Cost TZS 8196.73
Serv Charge TZS 0.00
Tax TZS 1803.27
Total TZS 10000
eSign. hii mita ni kwa ajili ya matumizi ya nyumbani au kiwandani?. Kwani hii ndo natumia nyumbani na huwa napata units hizo,
 
Wewe upo Tariff 1 ndio maana. Kama matumizi yako hayazidi 75 Units kwa mwezi nenda TANESCO uhudumiwe...
Lakini hayo matumizi lazima iwe ni kila mwezi ukizidisha tu hapo Automatically unarudishwa T1
Ahaaaaa kwa hiyo tarrif 1 ni wenye matumizi makubwa? Maana sisi kwa siku tu tunatumia units 42, so ukipiga kwa mwezi ni units 1260
 
Mkuu mbona mimi 10000 napata units 28 tu wewe unafanyaje unapewa units nyingi hivyo? Kwa 9500 tu. huyu yuko kwenye umeme wa rea
 
Ndugu utakuwa umezidi kiwango cha 75KW kwa mwezi ndio maana ukawekwa tarifu T1 na sio T4
Jaribu kutumia zosizozidi Units 70KW kwa miezi ndani ya miezi3 automatically utapelekwa kwa watumiaji wadogo
 
Mkuu pole sana najua kadhia unayopitia ila naamini suala lako limeshafika kunakohusika
Limefikaje kama hawa TANESCO hawajauliza details zangu? Ndio limeishia hapa hapa mkuu.

(Au unaonaje
Niandike barua kwa katibu mkuu wa Nishati na Madini)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…