Nipo jirani na njia ya umeme ya kutoka Rusumo kwenda Nyakanazi.
Upana wa njia (line) ni mita 40.

Natamani kulima mazao mafupi kwenye eneo la njia hii ambalo ni mali ya Tanesco,

Napenda nilime
maboga,
mboga (bustanI),
maharage,
Kunde,
Nanasi,
Mihogo,
Mahindi,
Njegere.
Nifuate taratibu zipi kuomba kulima?
 
Mpnendwa mteja Ahsante kwa kuwasilaiana nasi kupitia ukurasa huu, hairuhusiwi kufanya shughuli yoyote kwenye maeneo ya maiundombinu ya Tanesco. Ahsante ^EB
 
TANESCO kwanini mnakatakata umeme ovyo hivi Kimara?hivi nyie mna shida gani haziishi daily miaka nenda miaka rudi?
Ndugu Mteja!

Tunafurahia kukuhudumia, tafadhali onesha taarifa kamili kwa huduma bora

Jina.

Namba ya simu

Mkoa

Wilaya

Eneo

Namba ya meter

Tatizo

Toka lini

makao makuu 0748550000^NM
 
TANESCO, hivi ni kweli kuwa siku hizi mnagoma kutuwekea mita kwenye kila nyumba kwenye apartment ? Juzi surveyor amenigomea kunikadiria malipo ya mita zaidi ya moja wakati apartments ziko zaidi ya moja at siku hizi hata nyumba zikiwa nyingi kwenye msingi mmoja (apartments) mnatoa mita moja tu! Yaani nyumba ziko 3 mnalazimisha iwe mita moja, hamuoni kuwa mnakwenda mwendo wa reverse, badala ya kusonga mbele mnarudi nyuma? Hamuoni kuwa mnajipunguzia mapato yatokanayo na kuunganisha umeme wateja wengi? Hamuoni kuwa mnaikosesha mapato ya kodi za majengo serikali?

TANESCO tupeni wateja wenu ufafanuzi kuhusu hili.

Vv
 
Ndugu Mteja!

Tunafurahia kukuhudumia, tafadhali onesha taarifa kamili kwa huduma bora

Jina.

Namba ya simu

Mkoa

Wilaya

Eneo

Namba ya meter

Tatizo

Toka lini

makao makuu 0748550000^NM
TANESCO sio shida ya mtu mmoja.Ni Kimara yote hapa Dar.Eneo lote la Kimara wilayani Ubungo tunaexperience ukatikaji wa umeme wa mara kwa mara siku hizi.Kama hapa Kimara mwisho line ya dawasco ndio kwa siku hata mara nne unakatika.
 
habari hivi nkitaka kubadilishiwa meter nafanyaje .... mi nlifungiwa meter ambayo haizimi ata umeme ukiisha inaandika negative tu .... ko kuna saa deni linakua kubwa napata shida kulipa .... kama nlipangishia watu nyumba nkakuta hawakulipa kabsa umeme deni limelimbikizwa unit za negative zenye thaman ya 200k
 
Mimi niwapongeze kwa kazi nzuri mnayofanya ya kuangaza maisha yetu watanzania,ila Kuna watu wachache wanakwamisha dira na maono ya shirika lenu.

Kwanza baadhi ya watumishi hasa mikoani mnamchonganisha mkuu na wapigakura wake wakati tunaona anavyoangaika kuiweka nchi kwenye mstari,mama anaupiga mwingi hadi raha.

Mfano hapa mkoani Geita ,wilayani katoro,eneo la Mjimwema Kuna hospital mpya na jirani Kuna taasisi za serikali,nguzo zimekuja Ili wakazi jirani na hizo taasisi pia wapate huo umeme, watumishi wachache walioko huku wanachukua rushwa na kupeleka umeme kwingine na kuacha majirani na hizo taasisi wakiwa gizani.

Nimesema kwa uchungu najua Kuna baadhi ya watanzania ambao pia wanadhurumiwa haki ya kupata umeme ila kwasababu ya watu wasio waaminifu wanakosa.

Mama ameweka kijana shupavu na makini January makamba Ili amsaidie kusambaza umeme nchi nzima ila anakwama.
Tafadhalini mama tunamkubali Sana na hatutaki mumfelishe, mama anastahili.

Mameneja wa kanda wasaidie kuweka utaratibu mzuri Ili wakazi majirani na taasisi za kiserikali wapate japo raha ya umeme Ili ndio ombi letu kwenu.

Poleni kama nimewakwaza.
 
Mimi nahitaji majibu ya kitengo cha emergency ktk mkoa wa Mara kutokupokea simu pindi tunapo katikiwa na umeme tatizo ni nini? Wanacho hiki kitengo au kimetutwa?
 
Naomba kujulishwa, hivi mtu akiongeza vyumba uani kwake haruhusiwi kufungiwa mita nyingine tofauti na ile ya nyumba kubwa? Nimnyimwa hiyo huduma huku Buza, sasa sijui ni kwa wote au huku kwetu tu?
 
Mpendwa mteja pole kwa changamoto kama umefika ofisi za Tanesco na meneja amekujibu hivyo ndio utaratibu ulivyo^NM
 
Mpendwa mteja pole kwa changamoto kama umefika ofisi za Tanesco na meneja amekujibu hivyo ndio utaratibu ulivyo^NM
Tatizo ni nini? Mbona mnajinyima fursa ya kuongeza mapato? Service line mpya hata ambayo haifiki mita 10 mnalipisha 320k, tena kila mita inalipa 1,000/= kila mwezi kama kodi ya jingo, hamuoni kuwa mnaikosesha serikali (mmiliki wenu fedha nyingi?

Vv
 
Semeni kama kuna mgao mbona mnakera sana, maisha magumu na umeme kero tu, semeni tuhamie burundi
Mpendwa mteja Ahsante kwa kuwasiliana nasi kupitia ukurasa huu,poleni sana kwa adha hio mnayopitia kwa sasa. tafadhali tunaomba kujua ni eneo gani mnakosa huduma kwa sasa ^EB
 
Habari za jioni Tanesco! Naomba kufahamishwa,Je kuna mgao wa umeme jijini Mwanza?
 
Habari za jioni Tanesco! Naomba kufahamishwa,Je kuna mgao wa umeme jijini Mwanza?
Mpendwa mteja ahsante kwa kuwasiliana nasi kupitia ukurasa huu, poleni sana kwa adha hio Tumepokea taarifa za changamoto ya umeme kwa baadhi ya maeneo ya mkoa wa mwanza , Tunawaomba radhi kwa adha yeyote mliyopitia wataalamu wetu wanaendelea na jitihada za kutatua tatizo
TANESCO Huduma Ndugu Mteja.kwa Wateja
0748550000^EB
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…