Gharama ya kulipia idadi ya nguzo inategemea na Survey iliyofanyika, kama kulikuwa na kutokuridhika ama dalili zozote za kuibiwa unatakiwa kutoa Taarifa TNESCO na namba za mawasiliano tumeweka za kila Mkoa
 
Asante kwa kitukatia umeme huku kijichi.
Ila leo mmekata mapema jamani saa moja

Kawaida ni saa mbili......

Kama kawaida

Leo sijui ndio itarudi saa saba au tisa??
 
Nimeanza kuwa na mashaka na haya mnayosema ya huduma bora hayapo kivitendo. Mtwara kuna eneo liko km 4 tu kutoka mjini njia ya kuelekea airport linaitwa Mangamba.

Nyumba zaidi ya 150 hazina umeme na wameomba kuletewa mradi wa umeme tangu mwaka 2015. Mwaka jana mwezi feb na march Tanesco walijenga line kwa kuweka nguzo na baadhi ya nyaya. Hadi sasa ni mwaka na mwezi hakuna umeme umewashwa kwa madai hakuna transfoma.

Wananchi wamefuatilia Tanesco mkoa hadi wamekata tamaa. January mwaka huu wameandika barua kwa mkurugenzi mkuu makao makuu bila kujibiwa lolote. Majibu ya mkoa hadi sasa hawajaletewaTransfoma. Inasikitisha ninaposikia TANESCO wanasema wanatoa huduma bora. Haiingii akilini.
 
Kuna nyumba mbafunga meter za matumizi ya biadhara wakati ni umeme hapi ni4 matumiz ya nyumban hakuna hata frame
 
Naomba kujua kama nina vigezo vya kupewa tarif, ili nisisumbuke kufuatilia maana nilipopeleka barua niliambiwa tarif imesitishwa kwa muda

Namba ya mita yangu ni
221 325 3284 1
 
Ahaaaaa kwa hiyo tarrif 1 ni wenye matumizi makubwa? Maana sisi kwa siku tu tunatumia units 42, so ukipiga kwa mwezi ni units 1260
Unaweza kutumia hata zaidi ya hizo.. kama vifaa vyako vinatumia umeme mwingi sishangai.

cha msingi ita fundi aangalie nini tatizo kama unahisi hakuna uhalisia.. ni PM kama unataka nikupigie hesabu vizuri wa wastani kwa siku unatakiwa kutumia Units ngapi na cha msingi uwe mkweli kunitajia vifaa unavyotumia...

huenda una Restaurant kubwa halafu unalalamika
 
Mbagala mnakata sana umeme
Leo kama nilivyosema awali umeme umekatika eneo la Mbagala Mgeni Nani toka saa 2 usiku mpaka muda huu hakuna umeme. Nyumba za mtaa wa pili umeme upo!!!
 
Tanesco anzisheni mfumo ambao unamwezesha Mteja akishanunua umeme uwe unaingia moja kwa moja kwenye meter badala ya kwenda tena kuanza kuingiza tokens kwenye meter (mfanye kama wateja wanavyolipia ving'amuzi). Hii italeta faida nyingi sana kwenu na wateja wenu.

Pia tengenezeni mfumo wa mteja kuangalia salio la umeme wake kwa kutumia simu ya mkononi (kama wafanyavyo wateja wa bank kwa kutumia sim banking)
Kwa ujumla badilisheni mifumo mnatumia mifumo ya kizamani sana ambayo inachosha.
 
Tumepokea ushauri wako mpendwa mteja tunashukuru sana

Sent from my SM-J200H using JamiiForums mobile app
 
Tumepokea taarifa yako tutaifanyia kazi mpendwa mteja

Sent from my SM-J200H using JamiiForums mobile app
 
Mimi niko tarrif 4 mwezi uliopita nili nunua umeme wa sh 9,500/- kwa M-pesa nika pata unit 73.6 mwezi huu nimenunua 9,500/-
nimepata 73.90 Units ina maana nitaamishwa kwenda tarrir 4
Mkuu tariff 4 ndo nini?na inawezekana vipi 9,500 upate units 73,wakati Mimi nanunua wa 20,000 napata units 56.
 
Mimi niko tarrif 4 mwezi uliopita nili nunua umeme wa sh 9,500/- kwa M-pesa nika pata unit 73.6 mwezi huu nimenunua 9,500/-<br />nimepata 75.90 Units ina maana nitaamishwa kwenda tarrir 4?
 
Kwanza niwapongeze kwa kujiunga na dunia ya digitali,
Pili nikushauri uongeze idadi ya watu wa kukusaidia kujibu matatizo ya wadau wako, ikiwezekana wawe wa kanda tofauti au mikoa husika pia,

Tatu na kuubwa kabisa ni kuwa mm nilikuwa mteja wa tarrif 4, ila nikawa nanunua umeme wa 10000Tsh, badala ya 9200. Ikawa matumizi yangu yalikuwa chini ya unit 75 lakini ilikuwa nanunua kila mwenzi na mabakia ya umeme wangu yakawa yanaongezeka kulimbikizana.
January niliponunua umeme nikakuta nimehamishiwa tarrif 1 automatic na kuanzia hapo nikazira kununua umeme nikawa natumia mabakia ya umeme wangu mpaka march hii ndo nimenunua tena umeme wa elf 10 nikapata unit 28.

Msaada ninaouhitaji n kurudisha kwenye tarrif 4 ila usumbufu wa kuanza kujaza yale maform ndo unanikwamisha, kama inawezekana ukaangalia details zangu na ukathibitisha hizo na kubadilisha kutokea ofisin kwako itasaidia sana. kuniondolea kero husika

Meter namba yangu ni 43001735406
 
Mwezi wa 10, 11 na 12 ulinunua wastani wa unit 77 kinyume na agizo la EWURA linalokutaka utumie chini ya unit 75 kwa wastani hivyo kwa kuzidi huko ndiko kumepelekea uwe kundi la matumizi ya wateja wa wa majumbani.Hivyo hautaweza kubadilishiwa baada ya kuvuka kiwango cha chini.


Sent from my SM-J200H using JamiiForums mobile app
 
Mimi swali langu ni moja tu linahusu treni ya umeme. Je tuna umeme wa kutosha watanzania wote na kuendeshea treni
 
Mimi niko tarrif 4 mwezi uliopita nili nunua umeme wa sh 9,500/- kwa M-pesa nika pata unit 73.6 mwezi huu nimenunua 9,500/-<br />nimepata 75.90 Units ina maana nitaamishwa kwenda tarrir 4?

habari loco tumeona swali lako, kumbuka kuwa utaratibu wa kubadilishwa tarrif ni wastani wa miezi 3 mfululizo kama ukizidi wastani wa unit 75 kwa miezi hio utabadilishwa mara, kwa hesabu hizo ulivyonunua mara 2 utakuwa na wastani wa unit 74.7 hivyo bado utabaki kwenye tarrif 4.

ushauri; ili kubaki kwenye kundi hili jitahidi kufuata masharti na vigezo vyake tafadhali kutoa usumbufu unaweza kujitokeza. pia hakikisha manunuzi yako hayazidi shilingi 9150 au unaweza kununua umeme wa shilingi 9000



TANESCO
 
Mbona mimi tangu nimeanza kutumia umeme (mita mpya, ina miezi 6/7 sasa hivi) sijawahi kuzidisha units 70 kwa mwezi na bado nalipa 10,000/- napata units 28 tu?

Hio tarrif 4 inapatikanaje?
 
Mbona mimi tangu nimeanza kutumia umeme (mita mpya, ina miezi 6/7 sasa hivi) sijawahi kuzidisha units 70 kwa mwezi na bado nalipa 10,000/- napata units 28 tu?

Hio tarrif 4 inapatikanaje?
Tunaomba namba yako ya mita
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…