TANESCO tutangazieni kama kuna mgao wa umeme nchini

TANESCO tutangazieni kama kuna mgao wa umeme nchini

chapachapa

Member
Joined
Jan 14, 2013
Posts
93
Reaction score
21
Kwa siku tano mfululizo maeneo haya umeme ifikapo jioni unakatwana bila taarifa kwa sisi wateja labda Kama tangazo Hilo sijalisikia.

Maeneo ya ubungo Mandela Rd kuanzia external, maziwa, hadi darajani unaotazamana na rivaside.

Pamoja na kuwa jirani kabisa na mitambo ya umeme ya ubungo tunakutana na adha hii.

Leo tarehe 26/02/2021 umeme haukarudi mpaka saa 5 za usiku niandikapo taarifa hii na hatujui utarudi saa ngapi.

Tunaomba tutangaziwe kama ni mgao au uzembe au hitilafu.
 
Daaaah aseee nimerud kutoka mishe mishe umeme hakuna hivi kwa joto hili la dar tunalalaje jmn??????? Tanesco mnatukwazaa sanaa aseeee TANESCO
 
Cha ajabu na huku wanakata saa 1 usiku hadi saa 5 huko
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Wahusika mtupe majibu haraka. Na kuna baadhi ya sehemu wanakata na kurudisha ndani ya dakika moja, tena ni mara kwa mara, tatizo linakuwa ni nini?. Mkisababisha kuunguza mali zetu muwe tayari kutulipa.
 
Huku Mbeya siku ya pili umeme unakatika asubuhi unarudi usiku saa nne
 
  • Thanks
Reactions: _ly
Habari wana jamvi,

Siku za hivi karibuni sisi wakazi wa Dar tumeshuhudia kukatika kwa umeme sehemu tofauti tofuati kwa muda mrefu na kila siku.

Kwangu uwelewa wangu na uzoefu wangu naona kama mgao wa umeme umeanza kinyemela humu jamvini tuko watu wa aina mbali na nyadhifa tofauti, ni ombi langu tupeane taarifa kama kuna mgao ili kusudi tuanze kujipanga namna ya kukabiliana na mgao kama upo.

Natambua kwa asilimia kubwa wakazi wa jijini shughuli zetu zinategemea uwepo wa nishati hii. Ni mategemeo yangu tutapata majibu ya uhakika kwny uzi huu.

Ninawasilisha
 
Pia naona kuna nguzo nyingi mpya zinabadilishwa mtaani hasa njia kubwa. kuna nguzo za cement zimesimama huenda wanabadili nguzo.
 
Mimi sio msemaji wa TANESCO wala EWURA lakini haiitaji degree mbili kupata jibu la swali lako. Lakini kama nilivosema hapo hawali, ngoja wasemaji wenyewe waje. TANESCO
 
Kuna mtambo mbovu kidatu unasubiriwa kufanyiwa marekebisho . Jana Waziri kalemani kawasimamisha kazi baadhi ya viongozi kwa suala hilo maana mtambo uliharibika toka Septemba mwaka jana haukuwa umefanyiwa matengenezo mpaka sasa
 
Pia naona kuna nguzo nyingi mpya zinabadilishwa mtaani hasa njia kubwa. kuna nguzo za cement zimesimama huenda wanabadili nguzo
"Huenda" zimekuwa nyingi ni vyema wakatoa tamko ijulikane.
 
Back
Top Bottom