TANESCO tutangazieni kama kuna mgao wa umeme nchini

TANESCO tutangazieni kama kuna mgao wa umeme nchini

Waswahili bado hatujang'amua umuhimu wa kutoa taarifa rasmi za changamoto hasa kwny issue nyeti kama nishati, watu wanategemea nishati kuendesha maisha ya kila siku....*****
 
Waswahili bado hatujang'amua umuhimu wa kutoa taarifa rasmi za changamoto hasa kwny issue nyeti kama nishati, watu wanategemea nishati kuendesha maisha ya kila siku....*****
Bila nishati hasa umeme wa uhakika na kutosha hakuna maisha wala maendeleo.
 
Hata Arusha nako umeme unasumbua sana, hasa maeneo ya unga Ltd na soko mjinga.
 
Haya mamiradi ndio yanapelekea umeme kua pungufu, sijui kwnn tunatesana hivi?
 
Kariakoo leo umeme wamekata siku nzim.

Kariakoo sehemu ya uzalishaji na wanakata umeme.. halafu wanataka kodi
Unataka manager atangaze mgao then appteze kibarua chake?

Yajayo yana furahisha
 
Hii ndo Tanzania ya viwanda bwana umeme wenyewe umekata tamaa kama watanzania tulivyokata tamaa
 
Huu mshirika umekuwa wa kifamba sana....yaani yanakata kata umeme hovyohovyo kama yana tumbo la kuhara.

Yatakuwa hayana pesa ya kujiendesha so yanaibia kwa kukata umeme ili gharama za uendeshaji ziwe nafuu.

Kubababake mitano tena na bado.
 
Kumbe tunashindana na rwanda kununua ndege cash, kujenga reli mpya na kujenga jiji jipya hapa burigi wakati hatuja fix maswala ya nishati....mitano tena..
 
Kwa siku kadhaa sasa, umeme umekuwa kikwazo kwa wakazi wa jiji la Mwanza. Sina hakika kama mamlaka zimetoa taarifa kwa uma. Kipindi cha nyuma tunaambiwa kabisa umeme hautakuwepo maeneo kadhaa kwa mda flani na kwa sababu flani.
 
Wang'oe engine za Bombardier na Dreamliners zikaboost megawatts huko
 
Yani siku hizi umeme haupiti siku bila kukatika sasa hivi wamekata kutoka saa kumi na moja jioni mpaka sasa, jana walikata toka asubuhi mpaka saa kumi na moja jioni.

Naona wati sehemu mbalimbali wanalalamika.

Jamani kama kuna mgao ni afadhali mtueleze tujipange mbona tushazoea tu watanzania. Nashangaaa waziri juzi anasema tuna umeme wa kutosha kuliko mahitaji yetu sasa huo umeme kama watumiaji hatuna uhakika nao una maana gani.

Kuweni serious tafadhali walau muwe mwatwambia kama mtakata tujipange.
 
Naunga mkono hoja.... Kuna mgao wa kimyakimya hata hapa Morogoro....
 
Wapinzani walituchelewesha sana! Mitano 5 uchumi wakati sisi tunazalisha umeme na kuwauzia majirani...

Wao wamejifungia lockdown sisi tunalima tuje tuwauzie chakula!

Nasema uongo ndugu zangu?
 
Back
Top Bottom