TANESCO tutangazieni kama kuna mgao wa umeme nchini

TANESCO tutangazieni kama kuna mgao wa umeme nchini

Ni shirika la hovyo sana halafu kuna watu kutwa kucha kusema tupo uchumi wa kati na kusema hii ni nchi ya viwanda.
Inasikisha sana kuona TANESCO wanaendesha shirika kama ghetto!
 
Maeneo ya Charambe Dar, ulikatwa tangu saa tango asubuhi hadi saa moja usiku..
 
TANESCO huu mgao eneo la Ubungo Riverside, Kibangu na maeneo ya karibu si mtutangazie tu mgao tujue moja?
 
Kwa siku kadhaa sasa, umeme umekuwa kikwazo kwa wakazi wa jiji la Mwanza. Sina hakika kama mamlaka zimetoa taarifa kwa uma. Kipindi cha nyuma tunaambiwa kabisa umeme hautakuwepo maeneo kadhaa kwa mda flani na kwa sababu flani.
Kuna ndugu yangu anafanya kazi TANESCO anasema kuna mtambo mbovu wa umeme ndo unasababisha mgao wa umeme na hii ni sehemu kubwa ya Tanzania.

Na amesema kwa hapa Mwanza wanasupply nusu tu ya demand ya umeme kwa siku yaani wanasupply 17MegaWatt kwa siku wakati mahitaji ya jiji la mwanza ni 38 MegaWatt, hivyo tutegemee kuumia haswa umeme unakua unakatwa kwa masaa 12 hadi 24 kwa siku hapa Mwanza
 
Uchumi wakati huku umeme hakuna hii nchi ina vituko.
 
Sasa ni kma wiki au zaidi umeme unazima kwa masaa kadhaa na kurudi baadaye sana. Jana kuna sehemu meneo yetu, walizimiwa umeme toka asubuhi na kuupata jioni. Sehemu iliyokuwa na umeme ilipofika saa moja jioni wakazimiwa mpaka saa tano usiku.

Kwa scenario kama hiyo ni wazi kuna mgao. Hakuna tatizo la kuwa na mgao, twambieni /tupe taarifa tujue ratiba ya mgao tujiandae kwa nishati mbadala hasa kupata mwanga usiku. Ni hilo tu!

Hii ni karibu nchi nzima kutokana na habari za mitandaoni zinazotoka sehemu mbalimbali za nchi ya uchumi wa kati.
 
Kama dk 5 zilizopita wamekata umeme.

Nikiripoti kutoka Arusha, Tengeru, ni mimi ripota wako Tall Guy Fam, wa JF
 
Kuna maneno kwamba kuna mgao wa umeme, je Ni kweli? Jana kutwa nzima niliambiwa kuwa nyumbani hakukuwa na umeme, majuzi rafiki yangu anayekaa eneo jingine alinambia hawakuwa na umeme, Leo sehemu ninayotafutia riziki pia hakuna umeme, Ni kweli mgao umerudi? Ule ugonjwa tuliambiwa haupo ila ni changamoto ya kupumua. Hii tutaiitaje? Nadhani hatuna mgao, ila tuna changamoto ya umeme.
 
Tukuyu leo toka asubuhi,simu hazina chaja,mawasiliano hakuna,tanesco hatari!.
 
Hii taasisi naomba iheshimu kazi za watu, sio kukata umeme ovyo wanavyojisikia.

Leo nimeshinda cetre huku mchana kutwa hakuna umeme, imefika saa 1 jioni umeme unarudi mie ndio naondoka,

Nafika mtaa wetu huku nakuta umeme hakuna ndio umekatika saa moja.

Kwahiyo naendeleza maisha ya msituni hakuna tofauti na kuishi kwenye kichaka.

Jamani tupeni taarifa umeme una matumizi Mengi.
 
Hawa MBWA wanatutia sana hasara, watatuozeshea friji zetu
 
Back
Top Bottom