TANESCO tutangazieni kama kuna mgao wa umeme nchini

TANESCO tutangazieni kama kuna mgao wa umeme nchini

Mwananyamala, Kariakoo, Ilala na Posta wanakata tu wakijiskia hawa watu.
 
Kuna watu wana ventilator majumbani, zinatumia umeme. Wana wagonjwa wa Corona wanaozitumia kuishi. Jitahidi msikate umeme maana mnaua wagonjwa majumbani. Tafadhali tafadhali.
 
Mgonjwa anakaaje nyumbani?.

Hospital zote zina electrical backup generators.
 
Kwa tunao ishi Arusha mgao umekuwa mkali sana, vipi nyie huko kwenu?
 
Ubungo jana na leo hawajatugusa. Ila Maji jana na juzi dry siku nzima..
 
Cha kusikitisha juzi kati tu waziri wa wizara husika alisema umeme upo wa kutosha.
 
Tunaona jitihada nyingi za serikali kujaribu kuwavutia wawekezaji Tanzania.

Sasa naomba kuwauliza hawa TANESCO ni Mwekezaji gani anayeweza kuwekeza mahali ambapo umeme unakatwa saa yeyote na bila hata taarifa?

Hivi kuna mtu yuko tayari kuja kupoteza mtaji wake kweli?

Hivi kwa nini TANESCO isiwekewe mshindani? Yawepo mashirika mengine yanayoweza kuzalisha umeme na kuwauzia wananchi?
Nadhani Serikali haitaki kuelewa hasara wanayopata Makampuni makubwa kwa kukatika umeme at the same time wanataka wauze bidhaa zao kwa bei ya chini ..mfano viwanda vya saruji ( cement)
 
Nilifikiri suala la Tanesco ni maeneo flani tu kumbe lila pembe ya nchi hii shida ni zilezile. Leo nipo Wilaya ya Songea, hatuna umeme toka jana majira ya saa 2 hivi ni karibu kata kama mbili hivi, ukipiga Emergency wanakuambia mafundi wapo wanafuatilia ila sema hii mvua inawasumbua.

Hivi mimi nataka niulize hii ni kwa sababu ya technology duni au uzembe wa watu tu? Inawezekanaje watu wakae na giza karibu masaa 24 kwa sababu tu ya uzembe wa mtu au watu wachache? Tanesco jirekebishe jamani hamuoni kwamba ni kero kubwa kulaumiwa kila kona?
 
Sikumbuki kama Tv au Radio au Magazeti yanahabarisha huu mgao wa umeme.

Huku Arusha imekuwa too much kabisa,

Hii ni moja ya Failure za Jiwe,
 
Hawana uthubutu huo,ugali kwanza mengine yatafuata.
 
Kuna mgao mkubwa wa umeme unaendelea kwa wiki ya tatu sasa katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha. Ratiba waliyotoa TANESCO ni kwamba umeme ungekuwa unakatwa siku za Jumapili tu kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 12 jioni na kumalizika jumapili ya mpaka tarehe 21/03/2021.

Mambo yamekuwa ni tofauti kabisa kwani hapa Arusha na sehemu nyingi za Kilimanjaro kama siyo zote umeme unakatwa kila siku mchana na usiku bila utaratibu wowote. Arusha umeme unakatika mchana kwa masaa kadhaa na kurudi kisha kukatwa tena kati ya saa 11 na 12 jioni hadi usiku wa manane.

Kwa ufupi huu mgao umeturudisha nyuma sana na inaondoa tumaini la hii nchi kuwa na umeme wa uhakika hata kama ule wa stigler utakamilika.

Kukata kata umeme ni tabia isiyo ya kistaarabu na inafifisha uchumi na kuwanyima watu confidence ya kuanzisha biashara kubwa.

TANESCO kuna watu wasomi kwa nini wasiweke ratiba inayoeleweka ya kukata umeme kuliko kufanya mambo kienyeji?

Hivi ninavyooandika hii post ninatumia jenerator na kwa siku 3 nimeshatumia karibu laki 1 ya mafuta ya generator.

Waziri anasema hatuna tatizo la umeme sasa hiki tunachokiona ni kitu gani
 
Kua mzalendo mkuu,sema hivi "KWA SASA KUNA MATENGENEZO YANAENDELEA KWA HIO UMEME UNACHEZA CHEZA KIDOGO TU"[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]

Mitano tena.
 
Back
Top Bottom