Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tunakata miti.Tanesco Wanasemaje?
Soma namba mliipenda wenyeweKuna mgao mkubwa wa umeme unaendelea kwa wiki ya tatu sasa katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha. Ratiba waliyotoa TANESCO ni kwamba umeme ungekuwa unakatwa siku za Jumapili tu kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 12 jioni na kumalizika jumapili ya mpaka tarehe 21/03/2021...
Huu mgao so utakupa hasara ya hao sato.Hiyo kitu sehemu nyingi
Haha kabisa mzee bora ingekua kambale.Huu mgao so utakupa hasara ya hao sato.
Kuna mgao mkubwa wa umeme unaendelea kwa wiki ya tatu sasa katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha. Ratiba waliyotoa TANESCO ni kwamba umeme ungekuwa unakatwa siku za Jumapili tu kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 12 jioni na kumalizika jumapili ya mpaka tarehe 21/03/2021.
Mambo yamekuwa ni tofauti kabisa kwani hapa Arusha na sehemu nyingi za Kilimanjaro kama siyo zote umeme unakatwa kila siku mchana na usiku bila utaratibu wowote. Arusha umeme unakatika mchana kwa masaa kadhaa na kurudi kisha kukatwa tena kati ya saa 11 na 12 jioni hadi usiku wa manane.
Kwa ufupi huu mgao umeturudisha nyuma sana na inaondoa tumaini la hii nchi kuwa na umeme wa uhakika hata kama ule wa stigler utakamilika.
Kukata kata umeme ni tabia isiyo ya kistaarabu na inafifisha uchumi na kuwanyima watu confidence ya kuanzisha biashara kubwa.
TANESCO kuna watu wasomi kwa nini wasiweke ratiba inayoeleweka ya kukata umeme kuliko kufanya mambo kienyeji?
Hivi ninavyooandika hii post ninatumia jenerator na kwa siku 3 nimeshatumia karibu laki 1 ya mafuta ya generator.
Waziri anasema hatuna tatizo la umeme sasa hiki tunachokiona ni kitu gani
HeheheheMnyonge mnyongeni haki yake mpeni....kweli JPM aliwanyoosha......Mimi sijawahi kuwa mshabiki wa JPM.. na tangu aingie madarakani sijawahi kukaa gizani kiasi hiki.....huku mitaa ya Dodoma sehemu kubwa hakuna umeme na sasa yameshapita masaa matatu....eti kisingizio mvua iinyesha kidogo mara ukakatika....haijawahi kutokea for 5 years naapa...... sasa wameanza kabla hata hajazikwa .... naona wanaturudisha zama za wataalam wa kutapisha maji mtera