TANESCO watoa ufafanuzi kuhusu Bwawa la kufua umeme la Mwl. Nyerere kuwa na nyufa

View attachment 2752996

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

HALI YA UBORA WA MRADI WA JNHPP NA UHIFADHI WA WANYAMA PORI

Jumapili, 10 Septemba 2023.
Kuna taarifa zinasambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mradi wetu wa Bwawa la Kufua Umeme la Mwalimu Nyerere (JNHPP). Taarifa hizo zinaelezea na kuleta hofu kuhusu Ubora wa Mradi, pamoja na Uhifadhi wa wanyama pori.

Taarifa sahihi kuhusu mradi wetu ni kwamba, mradi huu umesanifiwa kwa kuzingatia ubora wa hali ya juu na ujenzi wake unasimamiwa na wataalam walio bobea kwenye fani ya ujenzi(Civil Engineering) na Usimikaji Mitambo(Electromechanical Engineering) kutoka ndani na nje ya nchi ili kuhakikisha tunapata mradi ulio bora.

Kila hatua ya mradi hukaguliwa na kuhakikiwa kabla ya kwenda kwenye hatua nyingine, na pale ambapo hatua iliyotekelezwa inashindwa kufuzu ukaguzi na uhakiki basi marekebisho hufanyika kabla ya kuendelea hatua inayo fuata.

Bwawa letu ndani ya kuta zake limesimikwa vifaa vinavyo pima uimara kadri maji yanavyoingia kwenye bwawa, vifaa hivyo vina pima kama kuna hitilafu zozote zitakazo hatarisha ubora wa bwawa. Mpaka mwisho wa mwezi Agosti bwawa letu lina ujazo wa maji yalioingia wa mita za ujazo zaidi ya bilioni 14, na uzito wa maji unahimiliwa vizuri na bwawa letu kwani hakuna tatizo lolote la ubora au uimara linaloonekana kupitia vifaa vilivyosimikwa kwenye bwawa hilo.

Vilevile, uhifadhi wa wanyama pori na utunzaji wa mazingira unazingatiwa kama vile ilivyoainishwa katika mpango uliopitishwa wakati mradi huu unaanza kutekelezwa.

Mpaka mwezi Agosti 2023, Mradi mzima wa ujenzi umefikia asilimia 91.72%, na ni matarajio yetu mitambo yote itakuwa imefika nchini kabla ya mwisho wa mwezi Disemba 2023, na tutaanza kujaribu kupitisha maji kwenye mitambo mitatu ya kwanza mwezi Februari na tunategemea kupata Umeme wa kwanza mwezi Juni 2024 kama tulivyo ahidi.

Tunashukuru wananchi kwa kushirikiana nasi katika safari hii ya kujenga taifa letu, na hususan ufuatiliaji wa maendeleo ya mradi wetu huu mkubwa wenye manufaa makubwa kwa Taifa letu.

Imetolewa Na;
KURUGENZI YA MAWASILIANO NA UHUSIANO KWA UMMA TANESCO- MAKAO MAKUU.
DODOMA

Pia soma: Bwala la kufua umeme la Mwl. Nyerere, limeanza kutoa nyufa
Sasa hapo ndiyo wametoa majibu ya kutokea kwa nyufa? Stupid engineers!
 
Mbona hawajajibu hoja ya bwawa kuwa na nyufa?
 
Yule sijui anaitwa Lukasi nani nani ambaye huwa anaandika waraka mrefuuu wakumsifia mama mkwe wa Mchengerwa na mwishoni anaweka namba yuko wapi?
 
Hao wapiga porojo wa Makamba walipaswa wamfuate huko alikopelekwa hata kama ni wahandisi.

Hivyo vifaa vilivyosimikwa kubaini weakness vinaitwaje?

Kama kuna nyufa na vinasoma hakuna shida basi vyenyewe pia vibovu.
 
Jibuni swali letu sisi tunauliza nyufa nyie mnajibu vifaa vya vilivyosimikwa ndani ya bwawa. Haya achaneni na mavifaa yenu turudi kwenye nyufa nasema nyufa za bwawa alaaah.
Hao ndio ccm bhana wana majibu yote, si umeona hata ya yule kilaza wa HABARI
 
Hakuna lisilo na mwanzo likakosa mwisho,kulikuwa na Zanupf,Kanu, na wengine wengi leo wako wapi. Waache wajazane watoto wao, wake zao, wakwe zao, wadogo zao lakini ipo siku. Majibu ya hovyo hovyo kwenye maswali magumu yatatamalaki.
 
IMG_3158.jpg

Kama mambo yenyewe ndio hivi hatari sana
 
View attachment 2752996

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

HALI YA UBORA WA MRADI WA JNHPP NA UHIFADHI WA WANYAMA PORI

Jumapili, 10 Septemba 2023.
Kuna taarifa zinasambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mradi wetu wa Bwawa la Kufua Umeme la Mwalimu Nyerere (JNHPP). Taarifa hizo zinaelezea na kuleta hofu kuhusu Ubora wa Mradi, pamoja na Uhifadhi wa wanyama pori.

Taarifa sahihi kuhusu mradi wetu ni kwamba, mradi huu umesanifiwa kwa kuzingatia ubora wa hali ya juu na ujenzi wake unasimamiwa na wataalam walio bobea kwenye fani ya ujenzi(Civil Engineering) na Usimikaji Mitambo(Electromechanical Engineering) kutoka ndani na nje ya nchi ili kuhakikisha tunapata mradi ulio bora.

Kila hatua ya mradi hukaguliwa na kuhakikiwa kabla ya kwenda kwenye hatua nyingine, na pale ambapo hatua iliyotekelezwa inashindwa kufuzu ukaguzi na uhakiki basi marekebisho hufanyika kabla ya kuendelea hatua inayo fuata.

Bwawa letu ndani ya kuta zake limesimikwa vifaa vinavyo pima uimara kadri maji yanavyoingia kwenye bwawa, vifaa hivyo vina pima kama kuna hitilafu zozote zitakazo hatarisha ubora wa bwawa. Mpaka mwisho wa mwezi Agosti bwawa letu lina ujazo wa maji yalioingia wa mita za ujazo zaidi ya bilioni 14, na uzito wa maji unahimiliwa vizuri na bwawa letu kwani hakuna tatizo lolote la ubora au uimara linaloonekana kupitia vifaa vilivyosimikwa kwenye bwawa hilo.

Vilevile, uhifadhi wa wanyama pori na utunzaji wa mazingira unazingatiwa kama vile ilivyoainishwa katika mpango uliopitishwa wakati mradi huu unaanza kutekelezwa.

Mpaka mwezi Agosti 2023, Mradi mzima wa ujenzi umefikia asilimia 91.72%, na ni matarajio yetu mitambo yote itakuwa imefika nchini kabla ya mwisho wa mwezi Disemba 2023, na tutaanza kujaribu kupitisha maji kwenye mitambo mitatu ya kwanza mwezi Februari na tunategemea kupata Umeme wa kwanza mwezi Juni 2024 kama tulivyo ahidi.

Tunashukuru wananchi kwa kushirikiana nasi katika safari hii ya kujenga taifa letu, na hususan ufuatiliaji wa maendeleo ya mradi wetu huu mkubwa wenye manufaa makubwa kwa Taifa letu.

Imetolewa Na;
KURUGENZI YA MAWASILIANO NA UHUSIANO KWA UMMA TANESCO- MAKAO MAKUU.
DODOMA

Pia soma: Bwala la kufua umeme la Mwl. Nyerere, limeanza kutoa nyufa
Kwa nilivyo muelewa ni kwamba nyufa zipo ila hazina madhara na kuna vifaa wamefunga ili kuhakikisha madhara hakuna!

Shida kukiri kuna nyufa ndio shughuli.
 
Nadhani wananchi wanahoji kuhusu nyufa zilizokwisha jitokeza tayari hili ndio walipaswa Tanesco walijibu
Niliwaza sana baada ya Dam za Libya kupasuka nikajisemea tu baada ya kuona comments za watu wakifurahia maafa ya Morocco na Libya

Kama kuna nyufa bora wasitishe kama kupunguza maji sawa kuliko kusubiri vijiji visombwe
 
Back
Top Bottom