TANESCO watoa ufafanuzi kuhusu Bwawa la kufua umeme la Mwl. Nyerere kuwa na nyufa

TANESCO watoa ufafanuzi kuhusu Bwawa la kufua umeme la Mwl. Nyerere kuwa na nyufa

Niliwaza sana baada ya Dam za Libya kupasuka nikajisemea tu baada ya kuona comments za watu wakifurahia maafa ya Morocco na Libya

Kama kuna nyufa bora wasitishe kama kupungunguza maji sawa kuliko kusubiri vijiji visombwe
Haya ni makosa makubwa ya mkandarasi lakini pia wakaguzi wa wizara husika wanawajibika kwenye hili pia.. Kuna maswali muhimu ya kujiuliza hapa
Je hizi nyufa husika
Zimeanzia chini?
Zimeanzia katikati?
Zimeanzia juu?
Kila moja hapo lina madhara yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
... KWAKWELI kabisa suala la nyufa halijajibiwa!
TUNAOMBA SANA, CHONDE CHONDE, uchunguzi ukamilike mapema ili, kama kuna hatari, watu wa mabondeni, 'downstream', wahame haraka kabla ya hatari!
USALAMA WA RAIA KWANZA!
 
Haya ni makosa makubwa ya mkandarasi lakini pia wakaguzi wa wizara husika wanawajibika kwenye hili pia.. Kuna maswali muhimu ya kujiuliza hapa
Je hizi nyufa husika
Zimeanzia chini?
Zimeanzia katikati?
Zimeanzia juu?
Kila moja hapo lina madhara yake

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbwembwe za Marope hizo alikuwa anataka bwawa lijae kwa sifa tu alifikiri anajaza pipa la maji
Angalia Ethiopia imewachukua miaka mingapi

Kama ni hela wamepiga sana bila kujali uimara wake
Aisee hao ni wa kufungwa tu
 
Haya ni makosa makubwa ya mkandarasi lakini pia wakaguzi wa wizara husika wanawajibika kwenye hili pia.. Kuna maswali muhimu ya kujiuliza hapa
Je hizi nyufa husika
Zimeanzia chini?
Zimeanzia katikati?
Zimeanzia juu?
Kila moja hapo lina madhara yake

Sent using Jamii Forums mobile app
Inawezekana Ufa umeanzia chini na sio juu.
Ni janga hili
 
Kwahiyo hapo nilipoedit na rangi ya njano ndio wamedhibiti hizo nyufa?![emoji848][emoji849]
20230918_094008.jpg
JamiiForums-69498884.jpg
 
Lilivyojaa likipasuka wataokutwa njiani hawatapona.

NB: Tulikosea kujenga hilo bwawa
 
Hizo kitaalam si ndio wasema sijui kitugani jointi!

Hivyo sizani kama zinatabu sana, kadri tutakavyo kuwa tuna endelea kulitumi litazoea na hizo jointi zitajiziba

Pia nazani zitakuwa zieacha kwa sababu za kitaalam zaidi ili ukuta uweze kupumua kabla maji hayajaanza kujazwa na kuanza kutumika na baada ya hapo zitajiziba zenyewe hivyo tusiwe na wasi ndugu zangu


Makofi tafadhari
 
View attachment 2752996

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

HALI YA UBORA WA MRADI WA JNHPP NA UHIFADHI WA WANYAMA PORI

Jumapili, 10 Septemba 2023.
Kuna taarifa zinasambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mradi wetu wa Bwawa la Kufua Umeme la Mwalimu Nyerere (JNHPP). Taarifa hizo zinaelezea na kuleta hofu kuhusu Ubora wa Mradi, pamoja na Uhifadhi wa wanyama pori.

Taarifa sahihi kuhusu mradi wetu ni kwamba, mradi huu umesanifiwa kwa kuzingatia ubora wa hali ya juu na ujenzi wake unasimamiwa na wataalam walio bobea kwenye fani ya ujenzi(Civil Engineering) na Usimikaji Mitambo(Electromechanical Engineering) kutoka ndani na nje ya nchi ili kuhakikisha tunapata mradi ulio bora.

Kila hatua ya mradi hukaguliwa na kuhakikiwa kabla ya kwenda kwenye hatua nyingine, na pale ambapo hatua iliyotekelezwa inashindwa kufuzu ukaguzi na uhakiki basi marekebisho hufanyika kabla ya kuendelea hatua inayo fuata.

Bwawa letu ndani ya kuta zake limesimikwa vifaa vinavyo pima uimara kadri maji yanavyoingia kwenye bwawa, vifaa hivyo vina pima kama kuna hitilafu zozote zitakazo hatarisha ubora wa bwawa. Mpaka mwisho wa mwezi Agosti bwawa letu lina ujazo wa maji yalioingia wa mita za ujazo zaidi ya bilioni 14, na uzito wa maji unahimiliwa vizuri na bwawa letu kwani hakuna tatizo lolote la ubora au uimara linaloonekana kupitia vifaa vilivyosimikwa kwenye bwawa hilo.

Vilevile, uhifadhi wa wanyama pori na utunzaji wa mazingira unazingatiwa kama vile ilivyoainishwa katika mpango uliopitishwa wakati mradi huu unaanza kutekelezwa.

Mpaka mwezi Agosti 2023, Mradi mzima wa ujenzi umefikia asilimia 91.72%, na ni matarajio yetu mitambo yote itakuwa imefika nchini kabla ya mwisho wa mwezi Disemba 2023, na tutaanza kujaribu kupitisha maji kwenye mitambo mitatu ya kwanza mwezi Februari na tunategemea kupata Umeme wa kwanza mwezi Juni 2024 kama tulivyo ahidi.

Tunashukuru wananchi kwa kushirikiana nasi katika safari hii ya kujenga taifa letu, na hususan ufuatiliaji wa maendeleo ya mradi wetu huu mkubwa wenye manufaa makubwa kwa Taifa letu.

Imetolewa Na;
KURUGENZI YA MAWASILIANO NA UHUSIANO KWA UMMA TANESCO- MAKAO MAKUU.
DODOMA

Pia soma: Bwala la kufua umeme la Mwl. Nyerere, limeanza kutoa nyufa
Katika taarifa yenye maneno 299 sijaona hata neno moja lililotaja nyufa,
 
Kwa hiyo hizo nyufa zinazosemwa zipo au hazipo maana taarifa haijazigusia hizo na ndiyo concern ya watu
Walio stable kichwani jibu limeeleweka tu na lipo wazi. Kiufupi wamejibiwa wenye akili, wanaojielewa ili waendelee na shughuli za ujenzi wa taifa. Misukule inaweza kuendelea na uzushi wao kama kawaida......haina athari; kuwepo au kutokuwepo kwao makes no difference.
 
Walio stable kichwani jibu limeeleweka tu na lipo wazi. Kiufupi wamejibiwa wenye akili, wanaojielewa ili waendelee na shughuli za ujenzi wa taifa. Misukule inaweza kuendelea na uzushi wao kama kawaida......haina athari; kuwepo au kutokuwepo kwao makes no difference.
Hivi na wewe upo stable kichwani?Vituko haviishi duniani!😂😂😂😂
 
Muwe makini msije mkawa mnajitengenezea majanga, taifa litachekwa kama kawaida yetu
 
Na hapo kwenye wataalamu wetu walio bobea ndipo ukakasi mkubwa sana ulipoko, wanaleta siasa kwenye mradi mkubwa kama huo? miradi mingi ya Tanesco nimefanya nao waache uongo wanakodishaga wataalamu hata kusimika transformer, Tanga pale Pongwe na Mazinde ni moja kati ya ushaidi nilio nao. Waache tu Muda uta waumbuwa.
Chuo cha tanesco wameviua , huko Moro wamekigeuza kuwa cha Islamic sharia
 
Back
Top Bottom