granitized
JF-Expert Member
- Jul 5, 2016
- 3,249
- 7,948
aliyeandika hii taarifa ni kiazi, na kama md wa tanesco naye kaipitia kabla haijatolewa, md naye ni kiazi++
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Taarifa haijitoshelezi...wamejibu kisiasaView attachment 2752996
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
HALI YA UBORA WA MRADI WA JNHPP NA UHIFADHI WA WANYAMA PORI
Jumapili, 10 Septemba 2023.
Kuna taarifa zinasambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mradi wetu wa Bwawa la Kufua Umeme la Mwalimu Nyerere (JNHPP). Taarifa hizo zinaelezea na kuleta hofu kuhusu Ubora wa Mradi, pamoja na Uhifadhi wa wanyama pori.
Taarifa sahihi kuhusu mradi wetu ni kwamba, mradi huu umesanifiwa kwa kuzingatia ubora wa hali ya juu na ujenzi wake unasimamiwa na wataalam walio bobea kwenye fani ya ujenzi(Civil Engineering) na Usimikaji Mitambo(Electromechanical Engineering) kutoka ndani na nje ya nchi ili kuhakikisha tunapata mradi ulio bora.
Kila hatua ya mradi hukaguliwa na kuhakikiwa kabla ya kwenda kwenye hatua nyingine, na pale ambapo hatua iliyotekelezwa inashindwa kufuzu ukaguzi na uhakiki basi marekebisho hufanyika kabla ya kuendelea hatua inayo fuata.
Bwawa letu ndani ya kuta zake limesimikwa vifaa vinavyo pima uimara kadri maji yanavyoingia kwenye bwawa, vifaa hivyo vina pima kama kuna hitilafu zozote zitakazo hatarisha ubora wa bwawa. Mpaka mwisho wa mwezi Agosti bwawa letu lina ujazo wa maji yalioingia wa mita za ujazo zaidi ya bilioni 14, na uzito wa maji unahimiliwa vizuri na bwawa letu kwani hakuna tatizo lolote la ubora au uimara linaloonekana kupitia vifaa vilivyosimikwa kwenye bwawa hilo.
Vilevile, uhifadhi wa wanyama pori na utunzaji wa mazingira unazingatiwa kama vile ilivyoainishwa katika mpango uliopitishwa wakati mradi huu unaanza kutekelezwa.
Mpaka mwezi Agosti 2023, Mradi mzima wa ujenzi umefikia asilimia 91.72%, na ni matarajio yetu mitambo yote itakuwa imefika nchini kabla ya mwisho wa mwezi Disemba 2023, na tutaanza kujaribu kupitisha maji kwenye mitambo mitatu ya kwanza mwezi Februari na tunategemea kupata Umeme wa kwanza mwezi Juni 2024 kama tulivyo ahidi.
Tunashukuru wananchi kwa kushirikiana nasi katika safari hii ya kujenga taifa letu, na hususan ufuatiliaji wa maendeleo ya mradi wetu huu mkubwa wenye manufaa makubwa kwa Taifa letu.
Imetolewa Na;
KURUGENZI YA MAWASILIANO NA UHUSIANO KWA UMMA TANESCO- MAKAO MAKUU.
DODOMA
Pia soma: Bwala la kufua umeme la Mwl. Nyerere, limeanza kutoa nyufa
JF 'mtaua watu kwa pressure''. Jumapili wamekaa kikao wakiwa wamechanganyikiwa
Hawajakanusha kuhusu nyufa, wanatueleza kuhusu watalaam. Kwani nani alisema watalaam ni 'mama ntilie''
JokaKuu
Exactly..contractor na consultant wa mradi wanatakiwa kutoa maelezo.
Tanesco wanasema kuna watalaam kutoka ndani na nje ya nchi waliobobea! Hili linatusaidiaje kujibu swali.
Mradi umefikia 92 %, hivi hizi si namba tu mtu anaweza kusema, je zinaeleza ubora wa kazi
Ukisoma barua nzima, kwanza imeandika katika ubora hafifu sana
Maudhui ya barua anaonyesha kuna kitu kinafichwa! na swali linabaki pale pale, je kuna nyufa?
Ili kufanya damage control iliyotokana na barua , mkurugenzi akiwa na contractor na consultant wafanye press conference. Kuna tatizo ima la nyufa aua mawasiliano lakini kuna tatizo linafichwa.
Kuna tatizo linafichwa
Pascal Mayalla JokaKuu
Kwa maana kilichobaki ni kuangalia mifumo kama ya maji taka, maji safi, umeme, barabara za kuzunguka mradi n.k...Na mradi ukifika 92% maana yake kazi zote kubwa zimeshafanyika, kilichobaki ni marekebisho ya hapa na pale.
Yaani kuwe na nyufa na lita bilioni 14 nyufa zihimili??? huo ni uzito mkubwa sana kama nyufa zingekuwepo ni dhahiri lingepasuka....Kwa hiyo hizo nyufa zinazosemwa zipo au hazipo maana taarifa haijazigusia hizo na ndiyo concern ya watu
Mkuu achana na hao matade wameshavimbiwa na asali ndio sababu wanaropoka ovyoDalili za mvua ni mawingu.. Hao wanaoitwa watalam nawafahamu vilivyo
Labda uniambie kama hizo nyufa zipo kama sehemu ya ujenzi ama kuna tatizo mahali?
Kumbuka kabla ya kujazwa maji hakukuwa na ufa wowote.. Hizi nyufa zilizoanza kuonekana je zitaishia hapo? Na zikiendelea je? Unayajua madhara yake!?
Daily tuna watu wako site na wanatueleza yanayoendelea huko! Hivi hujiulizi ni nani kavujisha hili la nyufa? Unadhani ni mtu wa kutoka nje?
Na je unajua kuna nyufa za aina ngapi? Mradi haujaanza tayari kuna tatizo limeonekana na bado baadhi yenu mnashupaza shingo kulitetea.. [emoji848][emoji2827]
Sent using Jamii Forums mobile app