TANESCO watoa ufafanuzi kuhusu Bwawa la kufua umeme la Mwl. Nyerere kuwa na nyufa

TANESCO watoa ufafanuzi kuhusu Bwawa la kufua umeme la Mwl. Nyerere kuwa na nyufa

Msijali Watanganyika, likibomoka ntawaletea Jenereta, naamini serikali itanifutia kodi ili nije kuwauzia kwa bei nafuu.
Cracking-Control-in-Dam.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
View attachment 2752996

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

HALI YA UBORA WA MRADI WA JNHPP NA UHIFADHI WA WANYAMA PORI

Jumapili, 10 Septemba 2023.
Kuna taarifa zinasambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mradi wetu wa Bwawa la Kufua Umeme la Mwalimu Nyerere (JNHPP). Taarifa hizo zinaelezea na kuleta hofu kuhusu Ubora wa Mradi, pamoja na Uhifadhi wa wanyama pori.

Taarifa sahihi kuhusu mradi wetu ni kwamba, mradi huu umesanifiwa kwa kuzingatia ubora wa hali ya juu na ujenzi wake unasimamiwa na wataalam walio bobea kwenye fani ya ujenzi(Civil Engineering) na Usimikaji Mitambo(Electromechanical Engineering) kutoka ndani na nje ya nchi ili kuhakikisha tunapata mradi ulio bora.

Kila hatua ya mradi hukaguliwa na kuhakikiwa kabla ya kwenda kwenye hatua nyingine, na pale ambapo hatua iliyotekelezwa inashindwa kufuzu ukaguzi na uhakiki basi marekebisho hufanyika kabla ya kuendelea hatua inayo fuata.

Bwawa letu ndani ya kuta zake limesimikwa vifaa vinavyo pima uimara kadri maji yanavyoingia kwenye bwawa, vifaa hivyo vina pima kama kuna hitilafu zozote zitakazo hatarisha ubora wa bwawa. Mpaka mwisho wa mwezi Agosti bwawa letu lina ujazo wa maji yalioingia wa mita za ujazo zaidi ya bilioni 14, na uzito wa maji unahimiliwa vizuri na bwawa letu kwani hakuna tatizo lolote la ubora au uimara linaloonekana kupitia vifaa vilivyosimikwa kwenye bwawa hilo.

Vilevile, uhifadhi wa wanyama pori na utunzaji wa mazingira unazingatiwa kama vile ilivyoainishwa katika mpango uliopitishwa wakati mradi huu unaanza kutekelezwa.

Mpaka mwezi Agosti 2023, Mradi mzima wa ujenzi umefikia asilimia 91.72%, na ni matarajio yetu mitambo yote itakuwa imefika nchini kabla ya mwisho wa mwezi Disemba 2023, na tutaanza kujaribu kupitisha maji kwenye mitambo mitatu ya kwanza mwezi Februari na tunategemea kupata Umeme wa kwanza mwezi Juni 2024 kama tulivyo ahidi.

Tunashukuru wananchi kwa kushirikiana nasi katika safari hii ya kujenga taifa letu, na hususan ufuatiliaji wa maendeleo ya mradi wetu huu mkubwa wenye manufaa makubwa kwa Taifa letu.

Imetolewa Na;
KURUGENZI YA MAWASILIANO NA UHUSIANO KWA UMMA TANESCO- MAKAO MAKUU.
DODOMA

Pia soma: Bwala la kufua umeme la Mwl. Nyerere, limeanza kutoa nyufa
Mbona hajauzungumzia huo ufa ambao kila mmoja ameuona?
 
Narudia tena... Hii kitu sidhan kama kutakua na suluhisho la matatizo ya umeme hata uzalishaj ukianza!! Tupo hapa kikubwa uzima tu!!
 
TANESCO mnacheza na maisha ya watanzania!
Jifunzeni kutoka Derna huko Libya kuhusu madhara ya bwawa kupasuka!
Maelfu kwa maelfu wamesombwa na Mafuriko yaliyotokana na mguvu ya maji toka kwenye Mabwawa.tena yale hayakuwa na ukubwa kama wa JNHP !

Lakini Je!
TANESCO mnataka kutuambia kwamba Naibu waziri mkuu amepotosha Umma na kuleta hofu kwa wananchi.?
Je!
Waziri wa Nishati Biteko alipoongelea Nyufa kwenye Bwawa la Nyerere ameudanganya umma na hivyo TANESCO kupitia huu waraka wenu mnakanusha taarifa ya waziri wenu?

Ukwelo mchungu......
Ili Biteko aweze kufanikiwa lazima achukuwe Maamuzi magumu....afagie mabaki yote ya Kipara ...kuanzia Bodi mpaka management.

Vinginevyo atabaki kubeba jumba bovu la Makamba na wenzake.
Sijui nianzie wapi yarabi toba!! Ee mola wetu tunusuru na yajayo. Mheshimiwa Naibu Waziri Mkuu katueleza wananchi kuwa kuna nyufa.Mainginia wakatoa ufafanuzi wa namna ya kushughulikia hizo nyufa.Tanesco mnasema kuna jambo linaleta taharuki isiyo ya lazima lakini hamuisemi ni tararuki gani , ninyi mbazungumzia mitambo na muda wa kujaza maji na kuanza majaribio.Sasa nani anadanganya!! Aaah nimeishiwa cha kuandika
 
taarifa haijagusia hata kiduchu kuhusu nyufa
Hapo ujue tayari wameshapiga tukio. Tayari hela zimekwapuliwa,likapigwa chini ya kiwango. Hasa tukio limeanzia baada ya mwenda zake kuondoka. Hii nchi kwa sasa tutaona kila aina ya ufisadi na wizi. Kwa sasa taasisi za Umma zinapigwa milioooo ambayo haijawahi kutokea tokea dunia iumbwe
 
Mtoa taarifa amekurupuka na ana hasira, wananchi wanahoji nyufa sio kuanza kufanya kazi.
 
Kwa hiyo hizo nyufa zinazosemwa zipo au hazipo maana taarifa haijazigusia hizo na ndiyo concern ya watu
Ahsante, mkuu '3Angels', umegonga penyewe hasa.

Ukitaka kujua ubabaishaji, huo ndio mfano mzuri. Hawataki kujibu swali rahisi, badala yake wanaeleza mengine kabisa ya kuwachanganya watu akili.
 
Mbwembwe za Marope hizo alikuwa anataka bwawa lijae kwa sifa tu alifikiri anajaza pipa la maji
Angalia Ethiopia imewachukua miaka mingapi

Kama ni hela wamepiga sana bila kujali uimara wake
Aisee hao ni wa kufungwa tu
Msimsingizie Marope, ... waziri wa nishati sio Engineer wa huo mradi! Tafuteni watu sahihi wa kuwajibishwa!
 
wataalamu waliobobea kwenye fani ya ujenzi (CIVIL ENGINEERING) na waliobobea kwenye fani ya mitambo (ELECTRO MECHANICAL ENGINEERING)

wallah hapo kuna ukakasi
 
Back
Top Bottom