TANESCO watoa ufafanuzi kuhusu Bwawa la kufua umeme la Mwl. Nyerere kuwa na nyufa

TANESCO watoa ufafanuzi kuhusu Bwawa la kufua umeme la Mwl. Nyerere kuwa na nyufa

Sijui kama hili bwawa litahimili miaka 10 kabla halijapasuka na kuleta madhara makubwa kwa watu, mazingira, na viumbe hai wengine

[mention]Mshana Jr [/mention] punguza kuwa Hussein Yahaya mkuu. Sorry, unautaalamu wowote wa mambo ya Uhandis lakin? Umewahi tembelea ule mradi walau kujua Kazi zinaendeleaje pale? Kwa iyo leo TANESCO haina wahandis mpk nyie ndo mtoe utaalam wa kitaa? Mradi ule unakila security za kuusecure mkuu, otherwise kwa nguvu ya maji yake izo nyufa zingeshapasua zile monolithic concrete walls kitambo sana, maji hayazuiliki kizembe!
 
Hii ndio ile inaitwa professional rubbish

Sent using Jamii Forums mobile app
Na kwa kukazia iitwe professerial rubbish!
[mention]Mshana Jr [/mention] punguza kuwa Hussein Yahaya mkuu. Sorry, unautaalamu wowote wa mambo ya Uhandis lakin? Umewahi tembelea ule mradi walau kujua Kazi zinaendeleaje pale? Kwa iyo leo TANESCO haina wahandis mpk nyie ndo mtoe utaalam wa kitaa? Mradi ule unakila security za kuusecure mkuu, otherwise kwa nguvu ya maji yake izo nyufa zingeshapasua zile monolithic concrete walls kitambo sana, maji hayazuiliki kizembe!
Miaka kumi imefika?Tulia na utunze maneno yako.
 
TANESCO nashauri mtafute AFISA MAHUSIANO kwa Umma mwenye weledi na kuelewa namna ya kujibu Hoja zinazoibuliwa na Jamii. Huyu aliyeandika huu Waraka wa kujibu Hoja za Nyufa sio PUBLIC RELATION OFFICER labda kama amesoma saaana ni Arts and Work yaaani ni msanii wa Maigizo au kudance sasa nyie mmempa cheo kisichomfaa. Kwa kifupi ni Kilaza maaana majibu yake yanazusha taharruki zaidi ya ile ya awali.
Tutawasilisha huuu Upuuzi wake kwa NAIBU WAZIRI MKUU huyu mtu aende KAKONKO DC huko labda panamfaa lakini siyo TANESCO.
 
[mention]Mshana Jr [/mention] punguza kuwa Hussein Yahaya mkuu. Sorry, unautaalamu wowote wa mambo ya Uhandis lakin? Umewahi tembelea ule mradi walau kujua Kazi zinaendeleaje pale? Kwa iyo leo TANESCO haina wahandis mpk nyie ndo mtoe utaalam wa kitaa? Mradi ule unakila security za kuusecure mkuu, otherwise kwa nguvu ya maji yake izo nyufa zingeshapasua zile monolithic concrete walls kitambo sana, maji hayazuiliki kizembe!
Dalili za mvua ni mawingu.. Hao wanaoitwa watalam nawafahamu vilivyo
Labda uniambie kama hizo nyufa zipo kama sehemu ya ujenzi ama kuna tatizo mahali?
Kumbuka kabla ya kujazwa maji hakukuwa na ufa wowote.. Hizi nyufa zilizoanza kuonekana je zitaishia hapo? Na zikiendelea je? Unayajua madhara yake!?
Daily tuna watu wako site na wanatueleza yanayoendelea huko! Hivi hujiulizi ni nani kavujisha hili la nyufa? Unadhani ni mtu wa kutoka nje?
Na je unajua kuna nyufa za aina ngapi? Mradi haujaanza tayari kuna tatizo limeonekana na bado baadhi yenu mnashupaza shingo kulitetea.. [emoji848][emoji2827]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
View attachment 2752996

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

HALI YA UBORA WA MRADI WA JNHPP NA UHIFADHI WA WANYAMA PORI

Jumapili, 10 Septemba 2023.
Kuna taarifa zinasambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mradi wetu wa Bwawa la Kufua Umeme la Mwalimu Nyerere (JNHPP). Taarifa hizo zinaelezea na kuleta hofu kuhusu Ubora wa Mradi, pamoja na Uhifadhi wa wanyama pori.

Taarifa sahihi kuhusu mradi wetu ni kwamba, mradi huu umesanifiwa kwa kuzingatia ubora wa hali ya juu na ujenzi wake unasimamiwa na wataalam walio bobea kwenye fani ya ujenzi(Civil Engineering) na Usimikaji Mitambo(Electromechanical Engineering) kutoka ndani na nje ya nchi ili kuhakikisha tunapata mradi ulio bora.

Kila hatua ya mradi hukaguliwa na kuhakikiwa kabla ya kwenda kwenye hatua nyingine, na pale ambapo hatua iliyotekelezwa inashindwa kufuzu ukaguzi na uhakiki basi marekebisho hufanyika kabla ya kuendelea hatua inayo fuata.

Bwawa letu ndani ya kuta zake limesimikwa vifaa vinavyo pima uimara kadri maji yanavyoingia kwenye bwawa, vifaa hivyo vina pima kama kuna hitilafu zozote zitakazo hatarisha ubora wa bwawa. Mpaka mwisho wa mwezi Agosti bwawa letu lina ujazo wa maji yalioingia wa mita za ujazo zaidi ya bilioni 14, na uzito wa maji unahimiliwa vizuri na bwawa letu kwani hakuna tatizo lolote la ubora au uimara linaloonekana kupitia vifaa vilivyosimikwa kwenye bwawa hilo.

Vilevile, uhifadhi wa wanyama pori na utunzaji wa mazingira unazingatiwa kama vile ilivyoainishwa katika mpango uliopitishwa wakati mradi huu unaanza kutekelezwa.

Mpaka mwezi Agosti 2023, Mradi mzima wa ujenzi umefikia asilimia 91.72%, na ni matarajio yetu mitambo yote itakuwa imefika nchini kabla ya mwisho wa mwezi Disemba 2023, na tutaanza kujaribu kupitisha maji kwenye mitambo mitatu ya kwanza mwezi Februari na tunategemea kupata Umeme wa kwanza mwezi Juni 2024 kama tulivyo ahidi.

Tunashukuru wananchi kwa kushirikiana nasi katika safari hii ya kujenga taifa letu, na hususan ufuatiliaji wa maendeleo ya mradi wetu huu mkubwa wenye manufaa makubwa kwa Taifa letu.

Imetolewa Na;
KURUGENZI YA MAWASILIANO NA UHUSIANO KWA UMMA TANESCO- MAKAO MAKUU.
DODOMA

Pia soma: Bwala la kufua umeme la Mwl. Nyerere, limeanza kutoa nyufa
India ndiyo nchi inayoaminika kuwa na wajua hesabu na mainjinia wazuri sana duniani, lakini kuna bwawa la umeme lililowahi kubomoka.
 
Magufuli alipoanzisha ujenzi wa lile bwawa unakumbuka alivyosema? "Haya,anzeni kujenga. Nataka kuuona uchawi wa Wamisri.!"
Uchawi"ndio neno lililotumika,na yule mtu alikuwa scientist,kwa nini aongee juu ya uchawi ?
 
hizo nyufa ni mapambo ya bwawa au ndio expansion joint ,
watoe ufafanuzi wa nyufa, hii taarifa ni mbambamba tu

biteko juzi kaona tatizo ,leo wanasema wapo vizuri
Kwa hiyo hawa 'Taa siko' wanambishia naibu waziri mkuu kuhusu uwepo wa nyufa? nchi ina mazongezonge sana hii..
 
Kwenye vichwa vyao team ya wataalamu inayosimamia mradi ni kila mfanyakazi wa TANESCO aliyeko site waliempeleka huko kupata uzoefu wa hiyo miradi.

Pili obvious contractor awezi ajiri kila mtu kutoka nje ya nchi so obvious kutakuwa na engineers wa TANESCO kwenye kazi za kila siku.

Team ya kitaalamu ina organisation structure yake mahususi wa mradi ambayo TANESCO imeiunda kutokana na skills mbali mbali. Na inaongozwa na project manager anaefahamika ambae wahusika waliochini yake wana report kwake.

Wao tazama hata viongozi wanapoenda tembelea mradi, yeyote alie-site mradi mfanyakazi wa TANESCO anageuka msemaji siku hiyo clearly hakuna team pale; otherwise project manager ndio angekuwa mtu wa kutoa ufafanuzi na anafahamika.

Hakikosena project manager siku hiyo, walau heads husika wa chini yake kwenye organisation structure kama ni issue za ujenzi basi designing/quality manager wa mradi.

Ni wazi hakuna team rasmi site based na waongeaji tofauti wanaojitokeza kila siku.

Halafu issue sio nyufa za kuta, issue ni uwezo wa maji over time kuweza pita chini ‘dam wall’ na kuufanya ukuta usiwe stable. Sasa hivi ndio wamestuka wanajenga support ya chini ya kuta kuzuia maji yasiweze penya chini. Hiyo kazi ilitakiwa kufanyika kabla ya kujaza maji knowing how weak the below surface (that’s why people learn fluid mechanics) apparently hayupo huyo mtaalamu kwenye team ya usimamizi kwenye ujenzi wa bwawa.

Halafu unasema mna team imara, ni watu wanaojifunza huo ujenzi tu huko, or else hayo ni makosa makubwa sana yanayotakana na uelewa mdogo wa usimamizi.

Inaonekana baada ya Mwarabu kulipua kazi huruma ukamjia na kuona umuhimu wa kuwekewa ukuta nguzo zaidi chini ya sakafu.

Management ya TANESCO imejaa watu wanaoropoka hawajui hata issue za mradi wao wenyewe.
 
Msijali Watanganyika, likibomoka ntawaletea Jenereta, naamini serikali itanifutia kodi ili nije kuwauzia kwa bei nafuu.
 
Back
Top Bottom