Sijui ndugu mwandishi unaongelea Tanga as mkoa au Tanga as mji, kwa Tanga as mji ni mji ulianza tangu mwaka 1890 wajerumani walipo ingia, Mji wa tanga ulipata hadhi ya kuwa manispaa tangu 1930, tokea hapo tanga ulikuwa mji kimbilio na namba moja kwa uchumi tanganyika mpka tunapata uhuru, mji wa tanga uliumbwa kwa mfumo wa capitalistic town, yaan walikuwepo watu na kampuni nyingi zenye nguvu ambazo ziliubeba uchumi, nani haikumbuki amboni na product zao kama ndoo za amboni na ndala za umoja? Uchumi wa kikapitalisti ulileta watu wengi tanga ili kufanya kazi, mji ulikuwa na mkoa ulikua miaka ya 70 mpka 80 sera za mwalimu nyerere ndio ziliua mji wa tanga na uchumi wake, azimio la arusha ndio lilimaliza kabisa uchumi wa pale, isingekuwa rahisi mji wenye uchumi wa mtu mmoja na makampuni ghafla ubadili upeo uwe mji wa kijamaa, walowezi wote waliikimbia tanga kwenda kenya, uingeleza na marekani, tanga kwa sasa uwekezaji una rudi taratibu, uchumi wa pale utakua, saivi wageni ni wengi, wenyeji siku zote huchelewa kujua kukimbizana na uchumi, ila soon uchumi wa kikapitalisti uta take over, sasa hivi wafanya biashara wenye asili ya ki asia wameanza jenga majengo marefu mjini, nina jamaa angu eng. Kwa mara ya kwanza ana tenda tanga ya kujenga jengo la orofa 10 pale mjini, jengo la wahindi, wale jamaa walinyang'anywa majengo yao yote mijini na sera ya kutaifisha, sekta ya ujenzi nayo huchangia uchumi