Tanga: Miili ya watu yaokotwa ikiwa kwenye Viroba

Tanga: Miili ya watu yaokotwa ikiwa kwenye Viroba

Sasa sababu mlizozipinga mwanzo iweje leo zionekana na maana wakati marukio yanajirudia bado?
Kutunza kumbukumbu, ni muhimu wengine "ushabiki" unawasahaulisha masuala ya msingi. Kabaya watu hao hawana Soni.
 

Waziri Masauni aagiza uchunguzi maiti zilizookotwa kwenye viroba​


masauni pic

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamadi Masauni akipata maelezo kutoka Kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omary Mgumba kuhusu tukio la miili ya watu wawili kuokotwa kwenye viroba.Picha na Raisa Said

Kilindi. Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, Hamadi Masauni ameliagiza Jeshi la Polisi kuhakikisha linafanya uchunguzi wa kina ili kubaini waliohusika na mauaji ya watu wawili na kuwatupa wakiwa kwenye viroba.

Maiti hizo ziliokotwa Agosti 11, 2022 zikiwa kwenye viroba katika kata ya Tunguli wilayani Kilindi mkoani Tanga na kupelekwa kuhifadhiwa Hospitali Teule ya Wilayani Kilindi.

Masauni ametoa agizo hilo leo Jumatano Agosti 17, 2022 baada ya kufika katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali Teule ya Wilayani Kilindi mkoani Tanga ilipohifadhiwa miili hiyo.

Waziri huyo amesema amesikitishwa na tukio hilo la mauaji lililotokea Wilayani humo na kuagiza Jeshi hilo lishirikiane na vyombo vingine vya usalama kuendeleza uchunguzi ili kuwakamata waliofanya mauaji hayo.

"Tukio hili ni la kinyama dhidi ya raia wenzetu wa Kitanzania, jambo hili halikubaliki kwa namna yoyote ile na sio utamaduni wetu. Kama Serikali tumelichukulia kwa uzito unaostahili na tutafanya kila linalowezekana ili vyombo vyetu vya usalama vinawabaini na kuwakamata wahusika," amesema Waziri huyo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omari Mgumba amesema watu waliofanya tukio hilo linaonyesha ni wazoefu sababu namna walivyo wakunja kwenye kiroba cha kilo 50 lakini utazani nikilo 20.
ADVERTISEMENT

Mgumba amesema kuwa dalili za awali zinaonyesha kuwa mauaji hayo hayajafanyika mkoa wa Tanga bali sehemu nyingine na kupeleka kutupa katika eneo hilo.

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga, Sofia Jongo amesema tayari Jeshi la Polisi nchini limeshaunda kamati kwaajili ya uchunguzi wa tukio hilo.

Mkuu wa Wilaya wa Wilaya, Abel Busalama amewataka wananchi wawe wanatoa taarifa wanapokuwa na mashaka na kitu chochote katika maeneo yao.

Mbunge wa Kilindi (CCM) Omari Kigua amesema tukio hilo linaweza kuwakimbiza wawekezaji wanaotaka kuwekeza huku akiliomba Jeshi la Polisi kuendelea na uchunguzi ili kuwabaini waliotekeleza tukio hilo la kinyama.
 
Mpakq taifa litakapokuwa na kanzi data iliyosheheni DNA za watu wake ndipo case kama hizi zitaanza kuchunguzwa kwa kina. Lakini kwa sasahivi unaweza kuambiwa tu ni miili kutoka nchi jirani.
 
Wametoka nchi za jirani zetu hao. Tanzania kwa Sasa ni shwari. Huo upuuzi ulikuwa unafanywa na Magufuli, lkn bahati nzuri Mungu aliamua kumtwaa ili kutuepushia shida Watanzania.
Unawajua Massiem au unawasikia tu? Hawa ni kawaida yao kuongoza nchi kwa ku-create fear in the society.
 
Kama Kipua mtekaji na mtesaji amekuwa mkuu wa makachero wa polisiccm mnategemea nini? Uzuri kesi ya mchongo ya Mbowe ilitisaidia kuwajua wasiojulikana
 
Wametoka nchi za jirani zetu hao. Tanzania kwa Sasa ni shwari. Huo upuuzi ulikuwa unafanywa na Magufuli, lkn bahati nzuri Mungu aliamua kumtwaa ili kutuepushia shida Watanzania.
Hapa umeongea kimihemko au chuki binafsi. Either utakuwa wa vyeti feki,shoga (ndo maana unajiita sexless) au ndo wake waliitwa vilaza. Sasa tuweke uchimba chumvi. Hoja ya kusema ni kutoka nchi jirani ndo hiyo hiyo ilitumika miaka ya Magufuli. Tukaipinga sisi wenye akili. Leo wasio na akili wanaitumia. Tuacheni Udini... Tujiulize hii tabia ya watu kuokotwa kwenye viroba kwa nini iwepo? Na kuna watu wanapotea. Mambo ya vyeti feki,dini na ushoga hayo tutayapinga tu sisi wengine ila ukweli tutasema. Kwa sababu chama cha mapinduzi kinatutaka tuseme ukweli.
 
Hivi hawa mbwa wanaofanya haya mauaji, wanadhani na wenyewe wataishi milele!! Kwa nini umuue binadamu mwenzako kirahisi tu!!

"Mashahidi waliona gari aina ya Landcruiser nyeupe ikipita katika maeneo yao"

Nani ni wamiliki wakuu wa magari ya aina hii?

Tukumbuke kuwa CCM ni ile ile na Serikali ni ile ile. Uzuri kesi ya Mbowe ilisaidia kuwatambua wasiojulikana na mtesaji mkuu amekuwa mkuu wa makachero wa polisiccm
 
Ben hakupotezwa na Dkt Magufuli na wala Lisu hakupigwa risasi na yeye bali ni wazandiki walifanya vile kwa ajili ya kumharibia.
Itakuchukua hata karne 3 kumtetea na kumuinua jangili jiwe lkn hutafanikiwa
 
Ben hakupotezwa na Dkt Magufuli na wala Lisu hakupigwa risasi na yeye bali ni wazandiki walifanya vile kwa ajili ya kumharibia.
Kwanini sasa nyuma ya pazia aliminya haki za tundulisu akibariki kazi za kishetani za job ndugai na genge lake?
 
Hoja ya kusema ni kutoka nchi jirani ndo hiyo hiyo ilitumika miaka ya Magufuli. Tukaipinga sisi wenye akili. Leo wasio na akili wanaitumia.
Enzi za jiwe ilikuwa kila mahala watu wanatoweka ama kutekwa na kikosi haramu alichoanzisha jiwe cha "watu wasiojulikana"

Tangu huyo mbwa atwaliwe kizembe kwa korona hata sisimizi hajatoweka wala kutekwa mitaani.

Kwahiyo, kama kwenye miji na mitaa ya nchi hii watu wote tupo Haiwezekani hizo maiti ziwe za nchi hii.
 
Raia hawanunuagi hawana hela ya kumiliki land cruiser jeupe so ni nani hawa kama siyo raia.
 
Back
Top Bottom