Tanga: Mjamzito adaiwa kufa baada ya kuwekewa damu kimakosa, Watano wasimamishwa kupisha uchunguzi

Kuna muda unampeleka mgonjwa wako hospital ila ukifika ule wakati daktari anakwambia hebu tupishe tumfanyie vipimo mgojwa unatamani umkatalie ubaki ukitazama ili ukiona walakini umuulize maswali ya msingi kwamba nini kinaendelea hapo, kwann unampa hiyo dawa, kwann unafanya hicho?

Maana madaktari na wauguzi wa sasa wamekuwa kama fundi shabani ukimuachia gari yako inakuwa ndio mwanzo wa magonjwa yasiyokuwa na mwisho.
 
M

Mkuu hata kama Una HIV huwezi kuwekewa damu ya mtu mwenye HIV
Zamani walikuwa wanaleta huo upuuzi ila siku hizi sababu umakini wa vipimo hizo kesi zimepungua. Ila hayakosekani majitu mazembe ambayo yanafanya kazi utadhani yalilazimishwa, anaweza pima damu juu juu au akachanganya vitendea kazi akakuchoma vyenye contamination ya virus.
 
Umakini mdogo sana, unachezaje na afya ya mtu aisee?
 
Selian ni hospitali nzuri na pia na shauri wkwa tanga ni ile ya mkoa wa jitahidi sana kuwa wasafi na ninzuri
 
Kuna madokta hawapo makini katika kazi zao, especially mikoani
I think Kosa sio La daktari Kosa ni umakini wa Manesi na kuchanganya Mafailu ya Wagonjwa..
Daktari anaandika but anayemuhudumia mgonjwa ni mwingine..

But hakukuwa na Njia yoyote ya kumsaidia hata kama wangetaka Reaction ikishaanza imeanza and hence Death
 
Duh nimeumia sana,Roho isiyo hatia imedhurumiwa,hawa matabibu wetu wanashida kubwa sana,unakuta anahudumia mgogwa utadhani wana ugomvi,hata askari magereza hawezi kuwa katili hivyo kwa mfungwa,sasa vipi hawa tabibu wetu?

Yaani hawako communicative kabisa,kumsaili mgonjwa,kumuuliza unasumbuliwa na nini ,vipi hali yako,hawawezi ,unafika ku kutundika drip ya damu bila usaili kwa mgonjwa wakati mgonjwa yuko katika hali nzuri ya kuzungumza.

Walaniwe wote waliohusika na uhuni huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…