Huo mzigo lazima aubebe, mataifa mengine wapo wasiotaka chanjo lakini hawakuwa na support ya kiongozi wao mkuu, leo hii asilimia kubwa kama sio asilimia 100 ya wale wanaoikataa chanjo nchini wanamnukuu yeye, alikuwa anauwezo wa kipekee kuongea na mwananchi wa kawaida na akamsikiliza... conspiracy theories zipo kila sehemu ila kama watu maarufu ama wenye nguvu wakiziongelea basi raia wengi zaidi wanaweza kuziamini. Utoaji elimu utakuwa ni mgumu sana na hatuwezi kukwepa kwamba uongozi wa awamu ya tano umeaminisha wengi misingi iliyo kinyume na zoezi serikali hii ya awamu ya sita inajaribu kufanya.