Tanganyika and Zanzibar: Articles of Union and implementing legislation, with other evidences

Tanganyika and Zanzibar: Articles of Union and implementing legislation, with other evidences

Joined
Sep 20, 2010
Posts
86
Reaction score
67
Ndugu, wana Jamii forums,

Mjadala kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Umekuwa mzito sana, lakini ninadhani cha mhimu ni kuuweka ukweli hapa Jamii forums, yaani nyaraka halisi za Muungano huo pamoja na habari zingine za kijasusi.

Naomba baada ya kusoma Nyakara zote, then tuendelee na Mazungumzo.

Nyaraka nilizoziweka hapa zina prove mambo makuu manne.

1. Muungano huu ulikuwa halali na ulipitishwa na kuwa ratified na serekeli ya Mapinduzi ya Zanzibar.

2. Kuongezeka kwa vipengere vingine kwenye article of union ilikuwa na sababu kuu ya kulinda amani Zanzibar, na si kwamba Tanganyika ilikuwa na nia sana ya kuitawala Zanzibar.

3. Article of Union ilimpa Rais wa serekali ya Muungano madaraka, kufanya mabadiliko ya vipengere mbalimbali vya sheria ili kuweza kudumisha kusudio la Muungano.

4. Kumekuwa na mtizamo kwamba, wazanzibari wanadhurumiwa BOT, lakini ukisoma hizi nyaraka (Zanzibar historia na BOT DOC_0000126864, PAGE 11 utaona kwamba mnamo mwaka 1968 Bank ya Zanzibar ilikuwa imefirisika na ilikuwa haiwezi hata kulipa deni lake iliyokuwa inadaiwa na Bank kuu ya Tanzania.

Nimeongeza proof kutoka IMF, zinazoonyesha share za Zanzibar katika EACB kwamba zilikuwa asilimi 3.5%(Tatu na nusu). Ila kwa makusudi nadhani au kwa kutoelewa Zanzibar wamekuwa wanajumulisha na share za Aden, ambayo nayo ilikuwa EACB members, na share zake zilikuwa asilimia 11% na ukichanganya na zanzibar zilikuwa zinafika (15%). ( Adeni ilikuwa chini ya sulutani na alipoondoka alichukua chake) . Na baada ya Uhuru Zanzibar ilipowenda kuomba kujiunga na IMF 1964 iliuwa imebakiwa na share za 3.5% sulutani alishaondoka na chake.

Pia hizi document za IMF zinafanya assessment ya chumi zote za Tanganyika na Zanzibar wakati wa uhuru wao, hebu sasa tuamue wenyewe? kama kweli Zanzibar yenye Uchumi wa $ 2 , Ilikuwa inauwezo wa kuwekeza asilimia 11 kwenye uchumi wa Tanganyika wa $24 MILIONI
 

Attachments

  • Presentation1.png
    Presentation1.png
    71.4 KB · Views: 1,052
  • Proof of the Union of Tanganyika and Zanzibar.pdf
    Proof of the Union of Tanganyika and Zanzibar.pdf
    2.1 MB · Views: 399
  • More evidence zanzibar DOC_0000126866.pdf
    More evidence zanzibar DOC_0000126866.pdf
    37.1 KB · Views: 222
  • Zanzibar historia na BOT DOC_0000126864.pdf
    Zanzibar historia na BOT DOC_0000126864.pdf
    475.1 KB · Views: 264
  • zanzibar share IMF 1964.pdf
    zanzibar share IMF 1964.pdf
    619.4 KB · Views: 132
  • tanganyika IMF 1961.pdf
    tanganyika IMF 1961.pdf
    297.8 KB · Views: 112
Tunashukuru Mkuu; lakini unadhani wenzio wana tatizo basi na ushahidi wa Muungano?

Hata uwawekee video baraza la mapinduzi likikubali kuungana na Tanganyika bado watabisha.

Uhalali wa Muungano kwao siyo suala la kukosa legal legitimacy - bali kwa sababu hawataki Muungano.
 
Tunashukuru Mkuu; lakini unadhani wenzio wana tatizo basi na ushahidi wa Muungano? Hata uwawekee video baraza la mapinduzi likikubali kuungana na Tanganyika bado watabisha. Uhalali wa Muungano kwao siyo suala la kukosa legal legitimacy - bali kwa sababu hawataki Muungano.

... ni mithiri ya wanandoa kuchokana na kuonesha nia dhahiri ya kutarakiana, kisha anajitokeza mtu na kuwaambia - "si nyie mmevikana pete siku ya harusi, nawasihi msiachane bhana!!"
 
​
​
​
​
​
Tundu Lissu asema​
wakati umefika sasa kwaSerikali kuweka wazi nyaraka mbali mbali zinazohusu historia ya Muungano wetuna ‘mapito' yake​
​
MAPITO' YA MUUNGANO anasema kwamba kwa kuzingatia mazingira yakuanzishwa kwa Muungano na historia yake, "... kitu cha ajabu sio kwambaumekuwa na matatizo, bali ni kwamba umedumu (licha ya matatizo hayo); nakwenda kinyume na mwelekeo katika Afrika."Muungano ulidumu misuguano yamiaka ya mwanzo kati ya Mwalimu Nyerere na Sheikh Karume iliyohusu kuongezwakwa masuala ya fedha na sarafu katika orodha ya Mambo ya Muungano. Aidha,Muungano ulidumu mauaji ya viongozi waandamizi na wajumbe wa Baraza laMapinduzi la kwanza la Jamhuri ya Watu wa Zanzibar kama Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar Abdallah Kassim Hanga, Waziri wa Fedha Abdul AzizTwala, Othman Sharrif, Mdungi Ussi, Saleh Saadalla na wengine wengi. ​
​
Vile vile,Muungano ulidumu mauaji ya Sheikh Karume mwenyewe mwaka 1972 ‘kuchafuka kwahali ya hewa ya kisiasa' Zanzibar iliyopelekea kung'olewa madarakani kwa Rais Aboud Jumbe mwaka 1984; alichokiita Mwalimu Nyerere ‘udhaifu' wa Rais Mwinyi;​
Kwa bahati mbaya, Mheshimiwa Spika ‘mapito' haya ya Muungano yamekuwa yanafichwa fichwa, licha ya kauli zamara kwa mara za ‘kuelimisha umma juu ya Muungano.' ​
​
Kwa sababu hiyo, zaidi yatendo la kuchanganya udongo na matukio mengine yaliyofanyika hadharani,historia halisi ya Muungano wetu haifahamiki kwa wananchi walio wengi. KambiRasmi ya Upinzani Bungeni inapendekeza kwamba wakati umefika sasa kwa Serikalikuweka wazi nyaraka mbali mbali zinazohusu historia ya Muungano wetu ‘mapito' yake ili Watanzania waelewe masuala yote yaliyotokea yanayouhusu. Hii ni muhimu zaidi kwa kuzingatia ukweli kwamba mataifa ya magharibi kama vile Marekani na Uingereza yalikwishatoa hadharani nyaraka za mashirika yao ya kijasusi pamoja na balozi zao za Tanzania zinazoonyesha jinsiambavyo serikali za mataifa hayo zilihusika katika kuzaliwa kwa Muungano.​
​
Mheshimiwa Spika, Kuanikwa kwa nyaraka zilizoko katika mamlaka mbali mbali za Serikali kutasaidia kuthibitisha aukukanusha taarifa ambazo chanzo chake ni nyaraka za kidiplomasia na kijasusi zanchi hizo kwamba Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulitokana na njama za kibeberu za kudhibiti ushawishi wa siasa za kimapinduzi za Chama cha Umma naviongozi wake ndani ya Baraza la Mapinduzi Zanzibar la wakati huo. ​
​
Aidha, nyaraka hizo zitatoa mwanga juu ya kilichowasibu viongozi waandamizi wa chamahicho ambao bila uwepo wao kutambuliwa rasmi, historia ya Mapinduzi ya Zanzibar na ya Muunganoinabaki pungufu. Kwa maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, miaka karibu hamsini ya Muungano ni umri wa kutosha kwa taifa la Tanzania kuambiwa ukweli wote juuya kuzaliwa kwake na mapito ambayo limepitia katika kipindi hicho.​


UKIUKWAJIMAKUBALIANO/SHERIA YA MUUNGANO​

Mheshimiwa Spika, Makubaliano ya Muungano yatarehe 22 Aprili 1964 yalikuwa ni mkataba wa kimataifa kati ya nchi mbili huruzilizokubaliana kuunda ‘nchi moja huru', kwa mujibu wa ibara ya (i) ya Hati yaMuungano. Ili kutekeleza Makubaliano ya Muungano, Bunge la Jamhuri ya Tanganyika lilitunga Sheria ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar,1964, Sura ya 557 ya Sheria za Tanzania.

Kifungu cha 4 cha Sheria hiyo kilitangaza kuunganishwa kwa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na kuwa ‘Jamhuri moja huru itakayoitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.'

Kwa upande wa Zanzibar, Baraza la Mapinduzi ambalo ndio lilikuwa ‘Bunge' la Zanzibar wakati huo halikutunga sheria ya kuridhia Makubaliano ya Muungano.

Jambo hili limekuwa chanzo cha mjadala mkali katika duru za kitaaluma na kisheria juuya uhalali wa Muungano wenyewe. Kwa vyovyote vile, matokeo ya kusainiwaMakubaliano ya Muungano ni kwamba Jamhuri ya Tanganyikana Jamhuri ya Watu wa Zanzibar zilikufa na nchimoja iliyokuja baadae kuitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania -kuzaliwa

Mheshimiwa Spika, Kwa mujibu wa aya ya (iv) ya Makubaliano ya Muungano na kifungu cha 5(1) cha Sheria ya Muungano, Mambo yaMuungano yaliyokubaliwa kwenye Makubaliano ya Muungano yalikuwa kumi na moja.

Haya ni mambo yaliyoko katika vipengele vya 1 hadi 11 vya Nyongeza ya Kwanza ya Katiba ya Muungano.

Mheshimiwa Spika,
Mamboyote yaliyoongezwa katika orodha ya Mambo ya Muungano baada ya mwaka 1964 yalikuwa nje ya Makubaliano ya Muungano na nje ya Sheria ya Muungano na kwahiyo yalikuwa batili. Hii nikwa sababu Sheria ya Muungano na sio Katiba za Muda za 1964 au 1965 au yasasa -ndio Sheria Mama iliyozaa Muungano na kuweka mgawanyo wa madaraka kati yamamlaka za Jamhuri ya Muungano na mamlaka za Zanzibar. Sheria ya Muungano ilitungwa na Bunge la Katiba tofauti na sheria za kawaida.

Aidha, Katiba ya Muda, 1965iliyotawala Tanzania hadi1977 iliiweka Sheria hiyo kama Nyongeza ya Pili katika Katiba na kuwekamasharti kwamba Sheria hiyo haiwezi kurekebishwa bila marekebisho hayo kuungwamkono na theluthi mbili ya Wabunge wote wa Tanganyikana wale wa Zanzibar.Vile vile, Katiba ya Muunganoinataja, katika Orodha ya Kwanza yaNyongeza ya Pili, kwamba moja ya Sheria ambazo mabadiliko yake yahitaji kuungwamkono na theluthi mbili ya Wabunge wote ni "Sura ya 557 (Toleo la 1965),Sheria ya Kuthibitisha Mapatano ya Muungano wa Tanganyikana Zanzibar yamwaka 1964."Mheshimiwa Spika, Kifungu cha 5 cha Sheria yaMuungano, ambacho ndicho chenye misingi mikuu ya Muungano hakijawahikurekebishwa tangu Sheria yenyewe ilipotungwa mwaka 1964. Badala yake, Bungelimekuwa na tabia ya kukwepa kuigusa kabisa Sheria ya Muungano na badala yakelimekuwa likifanya marekebisho ya orodha ya Mambo ya Muungano iliyowekwa kwamara ya kwanza katika Katiba za Muda za mwaka 1964 na 1965 kwa kuongeza vipengelekatika orodha hiyo. Lengo la marekebisho haya, Mheshimiwa Spika, limekuwa marazote ni kuinyang'anya Zanzibarmamlaka yake chini ya Sheria ya Muungano. Ndio maana katika Mapendekezo yaHalmashauri Kuu ya CCM Kuhusu Marekebisho ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano naKatiba ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar yaliyotolewa tarehe 27 Januari,1983, CCM ilitamka kwamba "... msingi wa kuwa na orodha ya mambo ya muunganokatika Katiba ni kuonyesha mamlaka ya Serikali ya Zanzibar ambayo yalikabidhiwakwa Serikali ya Muungano; na msingi wa kuongeza mambo zaidi katika orodha yamambo ya muungano, kama ambavyo imefanyika mara kwa mara, ni kuhamisha mamlakazaidi ya Serikali ya Zanzibar kwenda kwa Serikali ya Muungano." Mheshimiwa Spika,
Profesa Shivji anasema -katika The Legal Foundations of the Union -kwamba Bunge la Jamhuri yaMuungano halikupewa mamlaka ya kuongeza Mambo ya Muungano bali lilipewa mamlakaya kutunga sheria zinazohusu Mambo ya Muungano kama yalivyofafanuliwa katikaSheria ya Muungano. Kwa maana hiyo, nyongeza zote zilizofanyika katika orodhaya Mambo ya Muungano tangu mwaka 1964 zilikiuka Makubaliano ya Muungano naSheria ya Muungano na ni batili. Ndio maana, kwa muda mrefu, Wazanzibariwamelalamikia masuala haya, hasa hasa masuala ya fedha, sarafu na mafuta nagesi asilia.
 
Kuongeza masuala ya Muungano kutoka 11 hadi 22 ni kuimeza Zanzibar, Wabara tuache ubishi - hatujui ni jinsi gani inavyouma kumezwa!
 
Jamani watanganyika tuwaache wazanzibar waende zao shida ipo wapi!! Akunyimae futari ya kunde kakupunguzia mashuzi, nchi letu kubwa linatushinda let them go and let us close the door for good.
 
Jamani watanganyika tuwaache wazanzibar waende zao shida ipo wapi!! Akunyimae futari ya kunde kakupunguzia mashuzi, nchi letu kubwa linatushinda let them go and let us close the door for good.

Wakiondokana na Tanganyika "TUNGULE" watapata wapi?
 
Ndugu, wana Jamii forums,

Mjadala kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Umekuwa mzito sana, lakini ninadhani cha mhimu ni kuuweka ukweli hapa Jamii forums, yaani nyaraka halisi za Muungano huo pamoja na habari zingine za kijasusi.

Naomba baada ya kusoma Nyakara zote, then tuendelee na Mazungumzo.

Nyaraka nilizoziweka hapa zina prove mambo makuu manne.

1. Muungano huu ulikuwa halali na ulipitishwa na kuwa ratified na serekeli ya Mapinduzi ya Zanzibar.

2. Kuongezeka kwa vipengere vingine kwenye article of union ilikuwa na sababu kuu ya kulinda amani Zanzibar, na si kwamba Tanganyika ilikuwa na nia sana ya kuitawala Zanzibar.

3. Article of Union ilimpa Rais wa serekali ya Muungano madaraka, kufanya mabadiliko ya vipengere mbalimbali vya sheria ili kuweza kudumisha kusudio la Muungano.
Mkuu Emanuel Tayari, kwanza asante kwa kutuletea nyaraka hizi.
1. La uhalali wa muungano halina ubishi, japo hakuna "ratification process" yoyote iliyofanyika upande wa Zanzibar, muungano umehalalishwa na kauli ya Karume, kuwaeleza Mabalozi kuwa BLM limeridhia!, na "performance" ya utekelezaji wa vifungu vya muungano ni uthibitisho wa kuridhia, ila kiukweli "ratification" ilifanywa upande mmoja tuu wa Muungano, huku kwetu Tanganyika, Zanzibar tuliwaburuza, na walijiingiza wenyewe kichwa kichwa kupitia Karume!.
2. Articles zile zimeeleza wazi namna ya kuongeza vipengele, jee uongezaji uliofanyika umefuata taratibu?. Jibu ni no, utaratibu haukufuatwa hivyo makubaliano ya muungano yalikiukwa!.
3. Ni kweli zile articles zimempa mamlaka rais wa muungano kufanya mabadiliko yoyote ya sheria za muungano ambazo zinazifuta sheria za Zanzibar zinazokwenda kinyume cha sheria za muungano, lakini ziliweka shuruti kwa rais wa Zanzibar kuwa consulted firs kabla sheria hizo hazijapitishwa!. Jee Zanzibar iliwahi kuwa consulted?. Jibu ni no Zanzibar was never consulted!.

Pamoja na yote hayo ukijumlisha na kero za muungano zisizoisha, dawa sasa ni serikali moja!.
Pasco.
 
Ndugu, wana Jamii forums,

Mjadala kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Umekuwa mzito sana, lakini ninadhani cha mhimu ni kuuweka ukweli hapa Jamii forums, yaani nyaraka halisi za Muungano huo pamoja na habari zingine za kijasusi.

Naomba baada ya kusoma Nyakara zote, then tuendelee na Mazungumzo.

Nyaraka nilizoziweka hapa zina prove mambo makuu manne.

1. Muungano huu ulikuwa halali na ulipitishwa na kuwa ratified na serekeli ya Mapinduzi ya Zanzibar.

2. Kuongezeka kwa vipengere vingine kwenye article of union ilikuwa na sababu kuu ya kulinda amani Zanzibar, na si kwamba Tanganyika ilikuwa na nia sana ya kuitawala Zanzibar.

3. Article of Union ilimpa Rais wa serekali ya Muungano madaraka, kufanya mabadiliko ya vipengere mbalimbali vya sheria ili kuweza kudumisha kusudio la Muungano.

4. Kumekuwa na mtizamo kwamba, wazanzibari wanadhurumiwa BOT, lakini ukisoma hizi nyaraka (Zanzibar historia na BOT DOC_0000126864, PAGE 11 utaona kwamba mnamo mwaka 1968 Bank ya Zanzibar ilikuwa imefirisika na ilikuwa haiwezi hata kuchangia sehemu yake ya mtaji kwenda Bank kuu ya Tanzania.


attachment.php

MM nafikiri wazanzibari wamerubuniwa na waarabu, wanadhani waarabu watawapa fedha za mafuta na mafuta bure, ningeshauri wajue hakuna kiu cha bure, kila kitu kina gharama zake
 
Tunashukuru Mkuu; lakini unadhani wenzio wana tatizo basi na ushahidi wa Muungano? Hata uwawekee video baraza la mapinduzi likikubali kuungana na Tanganyika bado watabisha. Uhalali wa Muungano kwao siyo suala la kukosa legal legitimacy - bali kwa sababu hawataki Muungano.
Mkuu Mzee Mwanakijiji, vikao vya BLM ni kama vikao vya Cabinet, vinaitishwa kwa maandishi na miniti zinarekodiwa kwa maandishi, hakuna kikao chochote cha BLM kilichoitishwa kuukubali muungano, ila Mwenyekiti wa BLM, aliwaita baadhi ya wajumbe na kuwaeleza kuwa BLM limeridhia!. Baadaye akawaita mabalozi na kuwaeleza vivyo hivyo kuwa BLM limeridhia!. Hakuna kikao, hakuna miniti wala kumbukumbu yoyote ya kuridhia!.

Ila pamoja na kutokuwepo ridhio hilo, utekelezaji wa muungano ni ridhio tosha kama ilivyo ukimpenda mwanamke, ukamuingilia kwa kumbaka, na mwanamke yule akapatwa ujauzito, kuliko aibu ya kujulikana ameingiliwa, akaamua kubaki kwako kama mke, japo haukuondolei hatia ya ubakaji, ila mke yule atahesabika aliridhia tangu kubakwa kule, hadi ndoa ya lazima, na alipoendelea na kaendelea kuzaa watoto wengine, kunahalalisha ule ubakaji kama ni moja ya njia halali za kujipatia mke!. Kwetu usukumani tunaita "Chagulaga".

Muungano Tanganyika ndiye mume, ilimbaka binti Zanzibar, mshenga ni Karume!, binti aliridhia kubakwa kule, mpaka leo miaka 49!, sasa hawezi tena kuja na kisingizio ati haitaki ndoa kwa sababu tuu pale mwanzo alibakwa!.
Muungano is there to stay, "vitimbakwiri" vitashughulikiwa kikamilifu!. Kama Jumbe aliyekuwa rais alishughulikiwa ipasavyo, nani mwingine atathubutu?!.

Tena sasa tuweke shinikizo kuelekea serikali moja!.
Pasco.
 
Pasco..baraza la mapinduzi la Zanzibar liliundwa kwa sheria gani na sheria hiyo ilitungwa na nani? Utendaji wa baraza la mapinduzi ulikuwa unaongozwa na taratibu zilizotungwa lini na nani? Ni nani aliitisha kikao cha kwanza cha baraza la mapinduzi na alipata madaraka ya kufanya hivyo wapi?
 
"Tuwaeleweshe" wanzibari kuelekea serikali moja.
Kwani muungano tuliwaelewesha?!. Hao Wazanzibari, sio waelewa hata kidogo!, ni watu wa kupelekwa pelekwa tuu kwa shuruti!

Hizi chokochoko za uamsho ni kufuatia kupata bwana wa kiarabu anayewazuzua!, tukishaamua ni serikali moja, ni serikali moja, asiyetaka na afungashe virago vyake, amfuate huyo bwana wao huko kwao Arabuni!.

Tena Watanganyika tunahuruma kuliko, huyo Sultan Seyyid Said, katoka kwao Oman na kuvamia vile visiwa vyetu as if havina mwenyewe!. Baada ya kuzaliana kwa muda mrefu, sasa wameota mapembe na kujisikia hapo ndio kwao!. Wasio kubali serikali moja, tutafukuzia mbali, wafungashe virago vyao, warudi kwa babu zao!, na watuachie visiwa vyetu tuvifanye ni mkoa wa Zanzibar wenye wilaya mbili za Uguja na Pemba!.
P.
 
Hakuna jipya hapo! hebu tupeni document ambazo walisaini nyerere na mh. karume
 
Kuwa na serikali moja ni kuimeza Zanzibar kikamilifu, hata Muasisi Mkuu wa Muungano aliliona hilo ndio maana akaona heri tuwe na Serikali 2 tu hadi pale tutakapoingia kwenye Muungano Mkubwa wa Afrika Mashariki ambapo tunaweza kuingia kama Serikali 1 au kila nchi ikaingia na Serikali yake bila shida maana utakuwa Muungano wa nchi nyingi na si nchi 2 tu!
 
Ndugu, wana Jamii forums,

Mjadala kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Umekuwa mzito sana, lakini ninadhani cha mhimu ni kuuweka ukweli hapa Jamii forums, yaani nyaraka halisi za Muungano huo pamoja na habari zingine za kijasusi.

Naomba baada ya kusoma Nyakara zote, then tuendelee na Mazungumzo.

Nyaraka nilizoziweka hapa zina prove mambo makuu manne.

1. Muungano huu ulikuwa halali na ulipitishwa na kuwa ratified na serekeli ya Mapinduzi ya Zanzibar.

2. Kuongezeka kwa vipengere vingine kwenye article of union ilikuwa na sababu kuu ya kulinda amani Zanzibar, na si kwamba Tanganyika ilikuwa na nia sana ya kuitawala Zanzibar.

3. Article of Union ilimpa Rais wa serekali ya Muungano madaraka, kufanya mabadiliko ya vipengere mbalimbali vya sheria ili kuweza kudumisha kusudio la Muungano.

4. Kumekuwa na mtizamo kwamba, wazanzibari wanadhurumiwa BOT, lakini ukisoma hizi nyaraka (Zanzibar historia na BOT DOC_0000126864, PAGE 11 utaona kwamba mnamo mwaka 1968 Bank ya Zanzibar ilikuwa imefirisika na ilikuwa haiwezi hata kuchangia sehemu yake ya mtaji kwenda Bank kuu ya Tanzania.


attachment.php

Mtumie na yule kiongozi wa UAMSHO kwani alikuwa analamika kwmba hajaziona. Ila zile za hapa kwangu anazo documents zote!
 





Tundu Lissu asema

wakati umefika sasa kwaSerikali kuweka wazi nyaraka mbali mbali zinazohusu historia ya Muungano wetuna ‘mapito' yake
MAPITO' YA MUUNGANO anasema kwamba kwa kuzingatia mazingira yakuanzishwa kwa Muungano na historia yake, "... kitu cha ajabu sio kwambaumekuwa na matatizo, bali ni kwamba umedumu (licha ya matatizo hayo) – nakwenda kinyume na mwelekeo katika Afrika."Muungano ulidumu misuguano yamiaka ya mwanzo kati ya Mwalimu Nyerere na Sheikh Karume iliyohusu kuongezwakwa masuala ya fedha na sarafu katika orodha ya Mambo ya Muungano. Aidha,Muungano ulidumu mauaji ya viongozi waandamizi na wajumbe wa Baraza laMapinduzi la kwanza la Jamhuri ya Watu wa Zanzibar kama Makamu wa Rais waJamhuri ya Watu wa Zanzibar Abdallah Kassim Hanga, Waziri wa Fedha Abdul AzizTwala, Othman Sharrif, Mdungi Ussi, Saleh Saadalla na wengine wengi. Vile vile,Muungano ulidumu mauaji ya Sheikh Karume mwenyewe mwaka 1972;‘kuchafuka kwahali ya hewa ya kisiasa' Zanzibariliyopelekea kung'olewa madarakani kwa Rais Aboud Jumbe mwaka 1984; alichokiitaMwalimu Nyerere ‘udhaifu'wa Rais Mwinyi;
Kwa bahati mbaya, MheshimiwaSpika,‘mapito' haya ya Muungano yamekuwa yanafichwa fichwa, licha ya kauli zamara kwa mara za ‘kuelimisha umma juu ya Muungano.' Kwa sababu hiyo, zaidi yatendo la kuchanganya udongo na matukio mengine yaliyofanyika hadharani,historia halisi ya Muungano wetu haifahamiki kwa wananchi walio wengi. KambiRasmi ya Upinzani Bungeni inapendekeza kwamba wakati umefika sasa kwa Serikalikuweka wazi nyaraka mbali mbali zinazohusu historia ya Muungano wetu na‘mapito' yake ili Watanzania waelewe masuala yote yaliyotokea yanayouhusu. Hiini muhimu zaidi kwa kuzingatia ukweli kwamba mataifa ya magharibi kama vileMarekani na Uingereza yalikwishatoa hadharani nyaraka za mashirika yao ya kijasusi pamoja na balozi zao za Tanzania zinazoonyesha jinsiambavyo serikali za mataifa hayo zilihusika katika kuzaliwa kwa Muungano.Mheshimiwa Spika, Kuanikwa kwa nyarakazilizoko katika mamlaka mbali mbali za Serikali kutasaidia kuthibitisha aukukanusha taarifa ambazo chanzo chake ni nyaraka za kidiplomasia na kijasusi zanchi hizo kwamba Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulitokana na njama zakibeberu za kudhibiti ushawishi wa siasa za kimapinduzi za Chama cha Umma naviongozi wake ndani ya Baraza la Mapinduzi Zanzibar la wakati huo. Aidha,nyaraka hizo zitatoa mwanga juu ya kilichowasibu viongozi waandamizi wa chamahicho ambao bila uwepo wao kutambuliwa rasmi, historia ya Mapinduzi ya Zanzibar na ya Muunganoinabaki pungufu. Kwa maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, miaka karibuhamsini ya Muungano ni umri wa kutosha kwa taifa la Tanzania kuambiwa ukweli wote juuya kuzaliwa kwake na mapito ambayo limepitia katika kipindi hicho.
​

UKIUKWAJIMAKUBALIANO/SHERIA YA MUUNGANO​
Mheshimiwa Spika, Makubaliano ya Muungano yatarehe 22 Aprili 1964 yalikuwa ni mkataba wa kimataifa kati ya nchi mbili huruzilizokubaliana kuunda ‘nchi moja huru', kwa mujibu wa ibara ya (i) ya Hati yaMuungano. Ili kutekeleza Makubaliano ya Muungano, Bunge la Jamhuri ya Tanganyika lilitunga Sheria ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar,1964, Sura ya 557 ya Sheria za Tanzania.Kifungu cha 4 cha Sheria hiyo kilitangaza kuunganishwa kwa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na kuwa ‘Jamhuri moja huru itakayoitwa Jamhuri yaMuungano wa Tanganyika na Zanzibar.' Kwa upande wa Zanzibar, Baraza la Mapinduzi – ambalondio lilikuwa ‘Bunge' la Zanzibarwakati huo – halikutunga sheria ya kuridhia Makubaliano ya Muungano. Jambohili limekuwa chanzo cha mjadala mkali katika duru za kitaaluma na kisheria juuya uhalali wa Muungano wenyewe. Kwa vyovyote vile, matokeo ya kusainiwaMakubaliano ya Muungano ni kwamba Jamhuri ya Tanganyikana Jamhuri ya Watu wa Zanzibar zilikufa na nchimoja – iliyokuja baadae kuitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania -kuzaliwaMheshimiwa Spika, Kwa mujibu wa aya ya (iv) yaMakubaliano ya Muungano na kifungu cha 5(1) cha Sheria ya Muungano, Mambo yaMuungano yaliyokubaliwa kwenye Makubaliano ya Muungano yalikuwa kumi na moja.Haya ni mambo yaliyoko katika vipengele vya 1 hadi 11 vya Nyongeza ya Kwanza ya Katiba ya Muungano.Mheshimiwa Spika, Mamboyote yaliyoongezwa katika orodha ya Mambo ya Muungano baada ya mwaka 1964yalikuwa nje ya Makubaliano ya Muungano na nje ya Sheria ya Muungano na kwahiyo yalikuwa batili. Hii nikwa sababu Sheria ya Muungano – na sio Katiba za Muda za 1964 au 1965 au yasasa -ndio Sheria Mama iliyozaa Muungano na kuweka mgawanyo wa madaraka kati yamamlaka za Jamhuri ya Muungano na mamlaka za Zanzibar. Sheria ya Muungano ilitungwa naBunge la Katiba tofauti na sheria za kawaida. Aidha, Katiba ya Muda, 1965iliyotawala Tanzania hadi1977 iliiweka Sheria hiyo kama Nyongeza ya Pili katika Katiba na kuwekamasharti kwamba Sheria hiyo haiwezi kurekebishwa bila marekebisho hayo kuungwamkono na theluthi mbili ya Wabunge wote wa Tanganyikana wale wa Zanzibar.Vile vile, Katiba ya Muunganoinataja, katika Orodha ya Kwanza yaNyongeza ya Pili, kwamba moja ya Sheria ambazo mabadiliko yake yahitaji kuungwamkono na theluthi mbili ya Wabunge wote ni "Sura ya 557 (Toleo la 1965),Sheria ya Kuthibitisha Mapatano ya Muungano wa Tanganyikana Zanzibar yamwaka 1964."Mheshimiwa Spika, Kifungu cha 5 cha Sheria yaMuungano, ambacho ndicho chenye misingi mikuu ya Muungano hakijawahikurekebishwa tangu Sheria yenyewe ilipotungwa mwaka 1964. Badala yake, Bungelimekuwa na tabia ya kukwepa kuigusa kabisa Sheria ya Muungano na badala yakelimekuwa likifanya marekebisho ya orodha ya Mambo ya Muungano iliyowekwa kwamara ya kwanza katika Katiba za Muda za mwaka 1964 na 1965 kwa kuongeza vipengelekatika orodha hiyo. Lengo la marekebisho haya, Mheshimiwa Spika, limekuwa marazote ni kuinyang'anya Zanzibarmamlaka yake chini ya Sheria ya Muungano. Ndio maana katika Mapendekezo yaHalmashauri Kuu ya CCM Kuhusu Marekebisho ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano naKatiba ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar yaliyotolewa tarehe 27 Januari,1983, CCM ilitamka kwamba "... msingi wa kuwa na orodha ya mambo ya muunganokatika Katiba ni kuonyesha mamlaka ya Serikali ya Zanzibar ambayo yalikabidhiwakwa Serikali ya Muungano; na msingi wa kuongeza mambo zaidi katika orodha yamambo ya muungano, kama ambavyo imefanyika mara kwa mara, ni kuhamisha mamlakazaidi ya Serikali ya Zanzibar kwenda kwa Serikali ya Muungano." Mheshimiwa Spika, Profesa Shivji anasema -katika The Legal Foundations of the Union -kwamba Bunge la Jamhuri yaMuungano halikupewa mamlaka ya kuongeza Mambo ya Muungano bali lilipewa mamlakaya kutunga sheria zinazohusu Mambo ya Muungano kama yalivyofafanuliwa katikaSheria ya Muungano. Kwa maana hiyo, nyongeza zote zilizofanyika katika orodhaya Mambo ya Muungano tangu mwaka 1964 zilikiuka Makubaliano ya Muungano naSheria ya Muungano na ni batili. Ndio maana, kwa muda mrefu, Wazanzibariwamelalamikia masuala haya, hasa hasa masuala ya fedha, sarafu na mafuta nagesi asilia.

Kuna mambo mengi nina disagree na Lissu kwasababu facts zionanesha otherwise.
 
Kuongeza masuala ya Muungano kutoka 11 hadi 22 ni kuimeza Zanzibar, Wabara tuache ubishi - hatujui ni jinsi gani inavyouma kumezwa!

Mambo yote 11 tuliyaongeza kwenye Muungano, hayakuwa mambo ya Makusudi, kila kipengere kiliashiria kushindwa kwa uongozi wa Zanzibar katika hizo nyanja, and since Mwalimu Nyerere alikuwa na nia ya kuhakikisha stability, then haya Mambo ndio maana yaliongezeka kwenye maswala ya muungano.Swali la msingi amabalo ndugu zetu wazanzbari inabidi wajiulize, ni kwanini yale mambo mengine 11 yaliongezwa? nyaraka zao za kiserekari zinaonesha nini kilikuwa kikitoea Zanzibar mpaka kufikia hataua ya kupunguziwa mambo ambayo wanaweza kujitawala wenyewe?
 
Back
Top Bottom