Tanganyika and Zanzibar: Articles of Union and implementing legislation, with other evidences

Tanganyika and Zanzibar: Articles of Union and implementing legislation, with other evidences

Mkuu Emanuel Tayari, kwanza asante kwa kutuletea nyaraka hizi.
1. La uhalali wa muungano halina ubishi, japo hakuna "ratification process" yoyote iliyofanyika upande wa Zanzibar, muungano umehalalishwa na kauli ya Karume, kuwaeleza Mabalozi kuwa BLM limeridhia!, na "performance" ya utekelezaji wa vifungu vya muungano ni uthibitisho wa kuridhia, ila kiukweli "ratification" ilifanywa upande mmoja tuu wa Muungano, huku kwetu Tanganyika, Zanzibar tuliwaburuza, na walijiingiza wenyewe kichwa kichwa kupitia Karume!.
2. Articles zile zimeeleza wazi namna ya kuongeza vipengele, jee uongezaji uliofanyika umefuata taratibu?. Jibu ni no, utaratibu haukufuatwa hivyo makubaliano ya muungano yalikiukwa!.
3. Ni kweli zile articles zimempa mamlaka rais wa muungano kufanya mabadiliko yoyote ya sheria za muungano ambazo zinazifuta sheria za Zanzibar zinazokwenda kinyume cha sheria za muungano, lakini ziliweka shuruti kwa rais wa Zanzibar kuwa consulted firs kabla sheria hizo hazijapitishwa!. Jee Zanzibar iliwahi kuwa consulted?. Jibu ni no Zanzibar was never consulted!.

Pamoja na yote hayo ukijumlisha na kero za muungano zisizoisha, dawa sasa ni serikali moja!.
Pasco.

Pasco, Nadhani unachanganya kati ya taratibu zilizowekwa chini ya katiba ya Tanzania 1977 Section 98 (1) (b) Inayaotaka kuongezwa kwa mambo kwenye list ya Muungano lazima iwe approved by two thirds of Members of Parliament from Tanzania Mainlandand two thirds of Members of Parliament from Tanzania Zanzibar. Lakini the fact ni kwamba mambo mengi yaliongezwa kwenye list ya Muungano, yalifanyika kabla ya 1977, na hicho kipengere cha sheria hakikuwepo.Mwongozo wa kuongeza Idadi ya Mambo ya Muungano uliongozwa na The Interim Constitution 1964.

Maswali ya msingi ni yale yale, Kama Zanzibar ingekuwa stable kisiasa haya mambo yangeongezwaje kwenye list ya Muungano??? kwahiyo ushahidi unatuonesha kwamba kulikuwa na nia Njema ya kuongeza haya Mambo kwenye issue za Muungano ili tuepushe Vita na Vurugu Zanzibar.
 
Kuwa na serikali moja ni kuimeza Zanzibar kikamilifu, hata Muasisi Mkuu wa Muungano aliliona hilo ndio maana akaona heri tuwe na Serikali 2 tu hadi pale tutakapoingia kwenye Muungano Mkubwa wa Afrika Mashariki ambapo tunaweza kuingia kama Serikali 1 au kila nchi ikaingia na Serikali yake bila shida maana utakuwa Muungano wa nchi nyingi na si nchi 2 tu!

Ninakubariana na wewe, kwamba serekali moja haifai, Ila ili hii debate iwe yenye tija, inabidi ile dhana inayosema kwamba tunawaonea wazanzibari ibadilike, Kuna vitu vingi tu kwenye list ya maswala ya Muungano tunaweza kuwarudishia, hasa hasa isuues related to domestic matters.
 
Mambo yote 11 tuliyaongeza kwenye Muungano, hayakuwa mambo ya Makusudi, kila kipengere kiliashiria kushindwa kwa uongozi wa Zanzibar katika hizo nyanja, and since Mwalimu Nyerere alikuwa na nia ya kuhakikisha stability, then haya Mambo ndio maana yaliongezeka kwenye maswala ya muungano.Swali la msingi amabalo ndugu zetu wazanzbari inabidi wajiulize, ni kwanini yale mambo mengine 11 yaliongezwa? nyaraka zao za kiserekari zinaonesha nini kilikuwa kikitoea Zanzibar mpaka kufikia hataua ya kupunguziwa mambo ambayo wanaweza kujitawala wenyewe?

Wazanzibari waliwaambia kuwa wameshindwa hivyo muongeze masuala 11? Kama suala la kushindwa lilikuwa wazi kwa nini masuala hayo yaliongezwa kinyemela? Hivi nani kawapa mamlaka ya kikoloni/kidikteta ya kuwapunguzia watu wengine uhuru wa kujitawala wenyewe?
 
Hayo mambo hayakuongezwa kinyemela, ukisoma article of Union, na Interm constitition kipengele hadi kipengele ilikuwa inampa madaraka makubwa sana raisi wa Tanzania katika kuongeza mambo ya Muungano. Katiba ya Tanzania 1977 Section 98 (1) (b) ndio ilibadiri hili swala la namana gani mambo yanaweza kuongezwa kwenye list ya Muungano , i.e (laizma iwe approved by two thirds of Members of Parliament from Tanzania Mainlandand two thirds of Members of Parliament from Tanzania Zanzibar). Lakini the fact ni kwamba mambo mengi yaliongezwa kwenye list ya Muungano, yalifanyika kabla ya 1977, na hicho kipengere cha sheria hakikuwepo. Kwahiyo kusema ilifanyika kinyemera unakosea sana.
 
One Sovereign Republiz.jpg

Hapo ndipo nashangaa serikali za CCM zimenyamaza toka 1964. Hii ni hatari tunavurugana kwa upuuzi wa watawala wapuuzi
 
Attachments

  • One Sovereign Republiz.jpg
    One Sovereign Republiz.jpg
    6.1 KB · Views: 38
Hayo mambo hayakuongezwa kinyemela, ukisoma article of Union, na Interm constitition kipengele hadi kipengele ilikuwa inampa madaraka makubwa sana raisi wa Tanzania katika kuongeza mambo ya Muungano. Katiba ya Tanzania 1977 Section 98 (1) (b) ndio ilibadiri hili swala la namana gani mambo yanaweza kuongezwa kwenye list ya Muungano , i.e (laizma iwe approved by two thirds of Members of Parliament from Tanzania Mainlandand two thirds of Members of Parliament from Tanzania Zanzibar). Lakini the fact ni kwamba mambo mengi yaliongezwa kwenye list ya Muungano, yalifanyika kabla ya 1977, na hicho kipengere cha sheria hakikuwepo. Kwahiyo kusema ilifanyika kinyemera unakosea sana.

Haya, hapo kwenye kinyemela weka neno 'kiimla'
 
Sasa mbona "mwenyekiti kivuli" wa UAMSHO anadai bila hata kupepesa macho kuwa hajawahi kuona articles of Union?!
Mimi ninakubaliana na wale wanaodai kuwa Muungano huu ni kama ndoa. Baadhi ya ndoa hufika pahala wanandoa wakachokana na kufikia hatua ya kutalakiana. Kwa kawaida huwa ni mmoja ya wanandoa amabye huanza chokochoko ili kuwepo na mgogoro ambao hatimaye hufikia talaka kutolewa ama kwa amani au kwa vitimbi. Tukubali ndoa yetu imefikia hatua ya kutalakiana. Tunachohitaji ni kutumia busara na kufanya mchakato wa talaka uwe wa amani ili hata baada ya talaka tundelee kutembeleana na kushirikiana "kulea watoto". Ninaunga hoja ya muungano kuvunjwa lakini iwe kwa amani.
 
Mkuu Emanuel Tayari, kwanza asante kwa kutuletea nyaraka hizi.
1. La uhalali wa muungano halina ubishi, japo hakuna "ratification process" yoyote iliyofanyika upande wa Zanzibar, muungano umehalalishwa na kauli ya Karume, kuwaeleza Mabalozi kuwa BLM limeridhia!, na "performance" ya utekelezaji wa vifungu vya muungano ni uthibitisho wa kuridhia, ila kiukweli "ratification" ilifanywa upande mmoja tuu wa Muungano, huku kwetu Tanganyika, Zanzibar tuliwaburuza, na walijiingiza wenyewe kichwa kichwa kupitia Karume!.
2. Articles zile zimeeleza wazi namna ya kuongeza vipengele, jee uongezaji uliofanyika umefuata taratibu?. Jibu ni no, utaratibu haukufuatwa hivyo makubaliano ya muungano yalikiukwa!.
3. Ni kweli zile articles zimempa mamlaka rais wa muungano kufanya mabadiliko yoyote ya sheria za muungano ambazo zinazifuta sheria za Zanzibar zinazokwenda kinyume cha sheria za muungano, lakini ziliweka shuruti kwa rais wa Zanzibar kuwa consulted firs kabla sheria hizo hazijapitishwa!. Jee Zanzibar iliwahi kuwa consulted?. Jibu ni no Zanzibar was never consulted!.

Pamoja na yote hayo ukijumlisha na kero za muungano zisizoisha, dawa sasa ni serikali moja!.
Pasco.

Pasco

Hii yako kiboko!

Umeorodhesha mtiririko wa utumiaji nguvu/uburuzaji ambao tumeufanya dhidi ya Zanzibar na umeona hiyo haitoshi
unapendekeza serikali moja.

Je serikali moja itakuwa dawa au sumu?

Maelezo yako mengi yanalingana na ya mtoa mada hii link https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/334649-tundu-lissu-na-kiini-macho-cha-muungano.html lakini yeye amekuja na pendekezo jengine la jinsi ya kutatua "kero" za muungano zisizoisha.

Hata Mzanzibari,Dr. Bilal ambaye anatumikia "tumbo lake" ametoa mapendekezo yake juu ya muungano na anataka zibaki serikali mbili. Huyu Dr. Bilal haelewi kuwa dawa ni serikali moja?

Dr. Bilal ndie anayeongoza vikao vya kutatua kero na changamoto za muungano. Wameshindwa kufikiria hili la "dawa ya kero za muungano ni kuunda serikali moja"?
 
Ninakubariana na wewe, kwamba serekali moja haifai, Ila ili hii debate iwe yenye tija, inabidi ile dhana inayosema kwamba tunawaonea wazanzibari ibadilike, Kuna vitu vingi tu kwenye list ya maswala ya Muungano tunaweza kuwarudishia, hasa hasa isuues related to domestic matters.

Pasco anatumia neno "tuliwaburuza" "tuliiburuza Zanzibar" kama hili kweli lilifanyika sio sahihi kubadilisha dhana ya kuwa tuliwaonea au inaruhusika kuiburuza nchi nyengine kwa sababu tunaipenda?

Hata unaposema "kuna vitu tunanaweza kuwarudishia", huoni hii kauli inaashiria hiyo ya kuwaonea? wao hawana maamuzi katika kuondoa vitu katika list ya mambo ya muungano?
 
Haya, hapo kwenye kinyemela weka neno 'kiimla'

Maamuzi ya serekari ya Tanzania hayakuwa yaki totalitarian(kiimla) bali yaliuwa constitutional , kwasababu the government didn’t make decisions which violated any aspect of the constitution of the time. Kama hukubaliani na katiba ya mda ya mwaka 1964, hilo ni swali lingine.
 
Pasco, Nadhani unachanganya kati ya taratibu zilizowekwa chini ya katiba ya Tanzania 1977 Section 98 (1) (b) Inayaotaka kuongezwa kwa mambo kwenye list ya Muungano lazima iwe approved by two thirds of Members of Parliament from Tanzania Mainlandand two thirds of Members of Parliament from Tanzania Zanzibar. Lakini the fact ni kwamba mambo mengi yaliongezwa kwenye list ya Muungano, yalifanyika kabla ya 1977, na hicho kipengere cha sheria hakikuwepo.Mwongozo wa kuongeza Idadi ya Mambo ya Muungano uliongozwa na The Interim Constitution 1964.

Mkuu Emanuel Tayari, hebu kwanza turudi nyuma kabla hata ya katiba hii iliyopo ya 1977, hati za Muungano zilisema wazi kuwa mara baada ya muungano, iliundwa katiba ya muda, ile 1964 kwa maelekezo "very specific" kuwa ndani ya mwaka mmoja, Rais wa Tanganyika kwa mashauriano na rais wa Zanzibar, wataunda katiba ya kudumu ambayo ndio ingeeleza kuhusu utaratibu wa kuongeza mambo ya muungano.

(vii) The President of the united Republic: in agreement with the Vice-President who is head of the Executive in Zanzibar shall-
(a) Appoint a Commission to make proposals for a Constitution for the united Republic.
(b) Summon a Constituent Assembly composed of Representatives from Tanganyika and from Zanzibar in such numbers as they may determine to meet within one year of the commencement of the union for the purpose of considering the proposals of the Commission aforesaid and to adopt a Constitution for the united Republic.
(viii) These Articles shall be subject to the enactment of laws by the Parliament of Tanganyika and by the Revolutionary Council of the Peoples' Republic of Zanzibar in conjunction with the Cabinet of Ministers thereof, ratifying the same and providing for the Government of the united Republic and of Zanzibar in accordance therewith.
IN WITNESS WHERE Julius K. Nyerere, the President of the Republic of Tanganyika, and Abeid Karume the President of the Peoples' Republic of Zanzibar have signed these Articles, in duplicate, at Zanzibar, on this twenty-second day of April, 1964.
Passed in the National Assembly on the twenty-fifth day of April, 1964.

Kulikuwa na sababu gani ya kutoundwa hiyo constitituent assembly ndani ya mwaka mmoja na badala yake, ikaundwa 1977 ndani ya miaka 13!.

Msingi mkuu wa madaraka ya muungano ni (vii) The President of the united Republic: in agreement with the Vice-President who is head of the Executive in Zanzibar shall- Wakati wa miaka hiyo 13, Tanganyika ilipata wapi mamlaka ya kubadili zile articles za union bila kumshirikisha rais wa Zanzibar na hivyo kuongeza idadi ya mambo ya muungano?!.

Katiba ya JMT ya 1977, inapata powers zake kutoka hati za muungano, hivyo kabla hata taratibu zilizowekwa chini ya katiba ya Tanzania 1977 Section 98 (1) (b) Inayaotaka kuongezwa kwa mambo kwenye list ya Muungano lazima iwe approved by two thirds of Members of Parliament from Tanzania Mainlandand two thirds of Members of Parliament from Tanzania Zanzibar, ile hoja tuu ya kuongezwa jambo lolote, ilipaswa kutanguliwa na mashauriano kati ya rais wa Tanganyika na yule wa Wazibar ndipo muswada upelekwe bungeni kupigiwa kura na hizo two third majority. Mamlaya ya upande mmoja kufanya mabadiliko bila kushirikisha upande mwingine, tuliyapata wapi?.

Maadamu tumekuwa tukiuendesha huu muungano kibabe, sasa bora tumalize kazi rasmi kwa kwenda kwenye serikali moja itakuwa ni heshima, adabu na chokochoko zote zitakwisha!.
Pasco.
 
Pasco anatumia neno "tuliwaburuza" "tuliiburuza Zanzibar" kama hili kweli lilifanyika sio sahihi kubadilisha dhana ya kuwa tuliwaonea au inaruhusika kuiburuza nchi nyengine kwa sababu tunaipenda?

Hata unaposema "kuna vitu tunanaweza kuwarudishia", huoni hii kauli inaashiria hiyo ya kuwaonea? wao hawana maamuzi katika kuondoa vitu katika list ya mambo ya muungano?

Sikubaliani na huo msemo wa kwamba tuliwaburuza,Hii issue ya Muungano ilikuwa win to win situation, kuliuwa na faction zaidi ya tatu ndani ya zanzibar ilipopata uhuru, na hizi faction zote ziliuwa zinataka kungo'a faction nyingine. Tusingeingilia kungeuwa na civil war ya mda mrefu ambayo iliuwa inatishia stability yetu pia.
 
Ndugu, wana Jamii forums,

Nyaraka nilizoziweka hapa zina prove mambo makuu manne.

4. Kumekuwa na mtizamo kwamba, wazanzibari wanadhurumiwa BOT, lakini ukisoma hizi nyaraka (Zanzibar historia na BOT DOC_0000126864, PAGE 11 utaona kwamba mnamo mwaka 1968 Bank ya Zanzibar ilikuwa imefirisika na ilikuwa haiwezi hata kuchangia sehemu yake ya mtaji kwenda Bank kuu ya Tanzania.
Hili Mzee Mtei anaweza kuweka ukweli hapa.

BoT iliundwa lini?

Je BoT iliundwa kwa mtaji upi? Ulitoka wapi?

Umewahi kusikia kuwa kulikuwa na East African Currency Board?
 
Kwa miaka mingi watanzania tumekuwa tukijadili mengi juu ya Muungano, lakini hatukupata fursa pana ya kuujadili Mkataba wa Muungano huo yaani (Articles of Union) uliosainiwa na Mwalimu J.K Nyerere na ndugu Abeid A.Karume.

Haijapita miaka mitatu tangu baadhi ya wazanzibar walipoadhimia kuupata mkataba huu wakaambiwa hauonekani, na nadhani wakajaribu waupate kule United Nations ila sikumbuki- waliambiwaje huko.

Tundu Lissu mwaka jana 2011 alipowasilisha Hotuba ya Kambi ya Upinzani alielezea dai la Serikali ya Tanganyika lakini akatamka wazi kuwa “hatutaki kuona picha za Nyerere na Karume wakichanganya udongo, tunataka Mkataba wa Muungano”.

Leo tena, nawaletea Mkataba wa Muungano yaani Articles of Union. Wapo wanaosema Mkataba huu ndiyo mama wa katiba zetu mbili yaani ya Muungano na ya Zanzibar. Wapo wanaosema yale mambo 11 ya Muungano yameongezwa kadhaa. Sasa mkataba huu tuuone ukweli wake.

Ni nafasi yetu leo wanamang’amuzi, tuendelee kuoyesha kuwa sisi ni- alama ya machipuko ya fikra huru na hata vilivyojificha nyuma ya ukinza wa maovu, tuna uwezo wa kuvifurumua vikawekwa hadharani.

Mkataba:

MKATABA WA MUUNGANO BAINA YA JAMHURI YA TANGANYIKA NA JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR

Kwa kuwa Serikali ya Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar zinafahamu uhusiano wa muda mrefu watu wake na mshikamano na kukuza uhusiano huo na kuimarisha mshikamano na kukuza umoja wa watu wa Afrika, zimekutana na kutafakari Muungano wa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar.

Na kwa kuwa Serikali za Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar, zinapendelea ya kwamba Jamhuri hizi mbili ziungane kuwa Jamhuri moja huru moja kwa amasharti ya makubaliano yafuatayo:

Kwa hiyo IMEKUBALIWA baina ya Serikali ya Jamhuri ya Tanganyika na ya Jamhuri ya watu wa Zanzibar kama ifuatavyo:-

I) Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar zitaungana na kuwa Jamhuri huru moja.

II) Katika kipindi cha kuanza kwa Muungano mpaka Baraza la Kutunga katiba lililotajwa katika ibara ya (vii) litakapokutana na kupitisha katiba ya Jamhuri ya Muungano (Kuanzia hapa kitaitwa kipindi cha mpito), Jamhuri ya Muungano itaongozwa kwa masharti ya ibara ya (iii) mpaka ya (vi).

III) Katika kipindi cha mpito katiba ya Jamhuri ya Muungano itakuwa katiba ya Tanganyika iliyorekebishwa ili kuweka:

a) Chombo tofauti cha kutunga sheria na Serikali kwa ajili ya Zanzibar kwa mujibu wa sheria zilizopo za Zanzibar na vitakuwa na mamlaka ya mwisho katika Zanzibar kwa mambo yote isipokuwa yale tu yaliyo chini ya bunge na Serikali ya Jamhuri ya Muungano

b) Nafasi ya makamo wawili wa Rais mmoja kati yao akiwa ni mkaazi wa Zanzibar atakuwa ndiye kiongozi wa Serikali iliyotajwa kwa ajili ya Zanzibar na atakuwa ndiye msaidizi mkuu wa rais wa Jamhuri ya Muungano katika utekelezaji wa kazi za Serikali kwa upande wa Zanzibar.

c) Uwakilishi wa Zanzibar katika bunge la Jamhuri ya Muungano.

d) Mambo mengine yatayofaa au kuhitajika ili kuipa nguvu Jamhuri ya Muungano na mkataba huu.

IV) Mambo yafuatayo yatakuwa chini ya bunge na Serikali ya Jamhuri ya Muungano:-

1) Katiba na Serikali ya Jamhuri ya Muungano
2) Mambo ya nchi za nje
3) Ulinzi
4) Polisi
5) Mamlaka yanayohusika na hali ya hatari
6) Uraia
7) Uhamiaji
8) Mikopo na biashara ya nchi za nje
9) Utumishi katika Jamhuri ya Muungano.
10) Kodi ya mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika, ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa nchini na kusimamiwa na idara ya forodha
11) Bandari, mambo yanayohusu usafiri wa anga, Posta na Simu

V) Bunge na Serikali vilivyotajwa vitakuwa na mamlaka ya mwisho juu ya mambo yote yahusuyo Jamhuri ya Muungano na kuongezea mamlaka juu ya mambo yote yahusuyo Tanganyika.

Sheria zote zilizopo za Tanganyika na za Zanzibar zitaendelea kutumika katika maeneo yao bila kuathiri:-

a) Masharti yoyote yatakayowekwa na chombo chenye mamlaka ya kutunga sheria.

b) Masharti yatakayowekwa kwa amri ya Rais wa Zanzibar juu ya sheria yoyote inayohusu jambo lolote lililotajwa kwenye ibara ya (iv), na kufuta sheria yoyote inayolingana Zanzibar.

c) Mabadiliko yoyote kama yataonekana yanafaa au kuhitajika ili kufanikisha Muungano na mkataba huu.

a) Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano atakuwa ni Mwalimu J. K. Nyerere na ataongoza Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa kufuata masharti ya mkataba hu na kwa kusaidiwa na maofisa wengine atakaowateuwa toka Tanganyika na Zanzibar na watumishi wa Serikali zao.

b) Makamo wa kwanza wa Rais kutoka Zanzibar aliyeteuliwa kwa kufuata marekebisho kama yalivyoelezwa na ibara ya 3, atakuwa Sheikh Abeid Karume.

VI) Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa kukubaliana na Makamo wa Rais ambaye ni kiongozi wa serikali ya Zanzibar

a) Atateua tume kwa ajili ya kutoa mapendekezo kwa ajili ya katiba ya Jamhuri ya Muungano.
b) Ataitisha Baraza la kutunga katiba ikiwa na wawakilishi kutoka Tanganyika na Zanzibar katika idadi itakayoamuliwa likutane katika kipindi cha mwaka mmoja tokea kuanza kwa muungano kwa madhumuni ya kutafakarimapendekezo ya tume iliyotajwa juu na kupitisha katiba ya Jamhuri ya Muungano.

VII) Mkataba huu utahitaji kuthibitishwa kwa kutungiwa sheria na Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi la Jamhuri ya Watu wa Zanzibar kwa kushirikiana na Baraza lake la Mawaziri, na mkataba kupitishwa na kuundwa kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano na ya Zanzibar kwa kufuata masharti yaliyokubaliwa.

KWA KUSHUHUDIA HAPA Julius K. Nyerere, Rais wa Jamhuri ya Tanganyika na abeid Karume, Rais wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, wametia saini nakala mbili za mkataba huu, hapa Zanzibar siku ya tarehe Ishirini na mbili ya mwezi Aprili, 1964.

……………………………………………………………………………… …………………….
Umepitishwa na Bunge siku ya tarehe Ishirini na Tano ya Aprili, 1964.

……………………………………………………………………………… …………………….
Pius Msekwa, Karani wa Bunge

……………………………………………………………………………… …………………….
Adam Sapi Mkwawa, Spika
25 Aprili 1964

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
SOURCE:

1: {THE PATNERSHIP, ISBN: 9789987880553, pg. 156, Author: Aboud Jumbe, }

2: {Zanzibar hadi mwaka 2000: ISBN: 9789987898015, pg. 201, Author: Ali Shaaban Juma}

-

MAMBO 11 YANAYOTAJWA KUONGEZWA MIAKA YA KARIBUNI KINYEMELA NI:

12.Mambo yote yanayohusika na sarafu na fedha kwa ajili ya
malipo yote halali (pamoja na noti); mabenki (pamoja
mabenki ya kuweka akiba) na shughuli zote za mabenki;
fedha za kigeni na usimamizi juu ya mambo yanayohusika
na fedha za kigeni.
13. Leseni ya viwanda na takwimu.

14. Elimu ya juu.

15. Maliasili ya mafuta, pamoja na mafuta yasiyochujwa ya
motokaa na mafuata ya aina ya petroli na aina nyinginezo za
mafuta au bidhaa, na gesi asilia.

16.Baraza la Taifa la Mitihani la Tanzania na mambo yote
yanayohusika na kazi za Baraza hilo.

17.Usafiri na usafirishaji wa anga.

18.Utafiti.

19.Utafiti wa hali ya hewa.

20.Takwimu.

21.Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano.

22.Uandikishaji wa Vyama vya siasa na Mambo mengine
yanayohusiana navyo.
 
Pasco

Hii yako kiboko!

Umeorodhesha mtiririko wa utumiaji nguvu/uburuzaji ambao tumeufanya dhidi ya Zanzibar na umeona hiyo haitoshi
unapendekeza serikali moja.

Je serikali moja itakuwa dawa au sumu?

Maelezo yako mengi yanalingana na ya mtoa mada hii link https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/334649-tundu-lissu-na-kiini-macho-cha-muungano.html lakini yeye amekuja na pendekezo jengine la jinsi ya kutatua "kero" za muungano zisizoisha.

Hata Mzanzibari,Dr. Bilal ambaye anatumikia "tumbo lake" ametoa mapendekezo yake juu ya muungano na anataka zibaki serikali mbili. Huyu Dr. Bilal haelewi kuwa dawa ni serikali moja?

Dr. Bilal ndie anayeongoza vikao vya kutatua kero na changamoto za muungano. Wameshindwa kufikiria hili la "dawa ya kero za muungano ni kuunda serikali moja"?
Mkuu Nonda, kwenye muungano kumefanyika sacrifices, Tanganyika tumefuta jina letu, tumefuta nchi yetu, tumefuta utaifa wetu for the sake of Muungano, Zanzibar wao wanataka "to eat their cake and still have it!", you can't eat your cake and have it!. Huwezi kuingia kwenye muungano wa nchi moja na bado ukaendelea ku claim your soverenity!. Its high time sasa, Wazanzibar nao waka lipa the same price Tanganyika tuliogharimia, tuwe Taifa moja, Nchi moja na serikali moja!.

Mkuu Pasco

Baada ya ukusanyaji maoni ya kuandika katiba mpya, hasa unapozingatia maoni yaliyotolewa Zanzibar, unafikiri kuna uhalisia wa kuleta serikali moja, nchi moja na taifa moja? Au tutawaburuza tena?

Hivi nani alileta "uwendawazimu" wa kuifuta Tanganyika?
Ile sherehe tunayofanya kusherehekea uhuru wa "wadanganyika"/Tanzania bara ina maana yoyote?

Kama tuliifuta Tanganyika kwa nini hatusherehekei siku ya kuzaliwa jina Tanzania tu?
 
Kwa miaka mingi watanzania tumekuwa tukijadili mengi juu ya Muungano, lakini hatukupata fursa pana ya kuujadili Mkataba wa Muungano huo yaani (Articles of Union) uliosainiwa na Mwalimu J.K Nyerere na ndugu Abeid A.Karume.

Haijapita miaka mitatu tangu baadhi ya wazanzibar walipoadhimia kuupata mkataba huu wakaambiwa hauonekani, na nadhani wakajaribu waupate kule United Nations ila sikumbuki- waliambiwaje huko.

Tundu Lissu mwaka jana 2011 alipowasilisha Hotuba ya Kambi ya Upinzani alielezea dai la Serikali ya Tanganyika lakini akatamka wazi kuwa "hatutaki kuona picha za Nyerere na Karume wakichanganya udongo, tunataka Mkataba wa Muungano".

Leo tena, nawaletea Mkataba wa Muungano yaani Articles of Union. Wapo wanaosema Mkataba huu ndiyo mama wa katiba zetu mbili yaani ya Muungano na ya Zanzibar. Wapo wanaosema yale mambo 11 ya Muungano yameongezwa kadhaa. Sasa mkataba huu tuuone ukweli wake.

.
Mkuu
Umeweka sheria iliyopitishwa na bunge la Tanganyika na sio mkataba wa muungano.

Mkataba wa muungano utakuwa umebeba sahihi za Karume na Nyerere.

Wale wanaodai mkataba halisi wana sababu zao za msingi na sisi wadanganyika tunaochukulia masuala ya muungano kimchezo mchezo tuna sababu zetu kuleta sheria zilizopitishwa na bunge letu/bunge la Tanganyika. Tunadanganyika kirahisi.
 
Mkuu Pasco

Baada ya ukusanyaji maoni ya kuandika katiba mpya, hasa unapozingatia maoni yaliyotolewa Zanzibar, unafikiri kuna uhalisia wa kuleta serikali moja, nchi moja na taifa moja? Au tutawaburuza tena?

Hivi nani alileta "uwendawazimu" wa kuifuta Tanganyika?
Ile sherehe tunayofanya kusherehekea uhuru wa "wadanganyika"/Tanzania bara ina maana yoyote?

Kama tuliifuta Tanganyika kwa nini hatusherehekei siku ya kuzaliwa jina Tanzania tu?
Mkuu Nonda,
Wanzanzibari wanaitaka nchi yao leo kesho!. Hata hao wanaopigia upatu serikali mbili, kimoyo moyo bado wanataka nchi yao huku wakihitaji kuendelea kuinyonya Tanganyika, dawa ni kuwaburuza tuu!.
Pasco.
 
Back
Top Bottom