Tanganyika and Zanzibar: Articles of Union and implementing legislation, with other evidences

Tanganyika and Zanzibar: Articles of Union and implementing legislation, with other evidences

Kwanini Wolfgang Dourado aliwekwa ndani baada kusema kweli kuwa muungano haukuridhiwa na wananchi wa Zanzibar kupitia bunge lao? Hizo zingine umeweka porojo tu.
Alihifadhiwa mahala salama kwasababu ya kutaka kuhatarisha usalama wa taifa. Enzi za Nyerere, kuwaza tuu kuuvunja muungano, ni uhaini.
P
 
Mkuu Emanuel Tayari, kwanza asante kwa kutuletea nyaraka hizi.
1. La uhalali wa muungano halina ubishi, japo hakuna "ratification process" yoyote iliyofanyika upande wa Zanzibar, muungano umehalalishwa na kauli ya Karume, kuwaeleza Mabalozi kuwa BLM limeridhia!, na "performance" ya utekelezaji wa vifungu vya muungano ni uthibitisho wa kuridhia, ila kiukweli "ratification" ilifanywa upande mmoja tuu wa Muungano, huku kwetu Tanganyika, Zanzibar tuliwaburuza, na walijiingiza wenyewe kichwa kichwa kupitia Karume!.
2. Articles zile zimeeleza wazi namna ya kuongeza vipengele, jee uongezaji uliofanyika umefuata taratibu?. Jibu ni no, utaratibu haukufuatwa hivyo makubaliano ya muungano yalikiukwa!.
3. Ni kweli zile articles zimempa mamlaka rais wa muungano kufanya mabadiliko yoyote ya sheria za muungano ambazo zinazifuta sheria za Zanzibar zinazokwenda kinyume cha sheria za muungano, lakini ziliweka shuruti kwa rais wa Zanzibar kuwa consulted firs kabla sheria hizo hazijapitishwa!. Jee Zanzibar iliwahi kuwa consulted?. Jibu ni no Zanzibar was never consulted!.

Pamoja na yote hayo ukijumlisha na kero za muungano zisizoisha, dawa sasa ni serikali moja!.
Pasco.
Idea ilikuwa serikali moja, Karume alitaka waungane moja kwa moja na iwe nchi moja lakini Nyerere alikataa makusudi ingawa naye alitaka muungano wa taifa moja.
Alijua wakiungama serikali moja baadae Zanzibar watalalamika kumezwa maana watapoteza utambulisho wao kama Tanganyika ilivyopoteza. Lakini Nyerere alifikiri kizazi cha nne cha wazanzibar baada ya kuona faida za muungano wangedai serikali moja.
Badala yake tumeona mambo mengibyakibadilishwa au kuongezwa bila kufata utaratibi, rasilimali za Tanganyika ndizo zinagharamia muungano.
Kwa kifupi Tanganyika inapata hasara kubwa kupitia muungano huu na ni wakati wa kuwa na serikali inayosimamia mambo yake nje ya muungano.
 
Back
Top Bottom