Mkuu Emanuel Tayari, kwanza asante kwa kutuletea nyaraka hizi.
1. La uhalali wa muungano halina ubishi, japo hakuna "ratification process" yoyote iliyofanyika upande wa Zanzibar, muungano umehalalishwa na kauli ya Karume, kuwaeleza Mabalozi kuwa BLM limeridhia!, na "performance" ya utekelezaji wa vifungu vya muungano ni uthibitisho wa kuridhia, ila kiukweli "ratification" ilifanywa upande mmoja tuu wa Muungano, huku kwetu Tanganyika, Zanzibar tuliwaburuza, na walijiingiza wenyewe kichwa kichwa kupitia Karume!.
2. Articles zile zimeeleza wazi namna ya kuongeza vipengele, jee uongezaji uliofanyika umefuata taratibu?. Jibu ni no, utaratibu haukufuatwa hivyo makubaliano ya muungano yalikiukwa!.
3. Ni kweli zile articles zimempa mamlaka rais wa muungano kufanya mabadiliko yoyote ya sheria za muungano ambazo zinazifuta sheria za Zanzibar zinazokwenda kinyume cha sheria za muungano, lakini ziliweka shuruti kwa rais wa Zanzibar kuwa consulted firs kabla sheria hizo hazijapitishwa!. Jee Zanzibar iliwahi kuwa consulted?. Jibu ni no Zanzibar was never consulted!.
Pamoja na yote hayo ukijumlisha na kero za muungano zisizoisha, dawa sasa ni serikali moja!.
Pasco.