Tanganyika iiombe radhi Zanzibar?

Tanganyika hatuna la kupoteza muungano ukivunjika ila Zanzibar watapoteza bajeti, nafasi tele za uteuzi, biashara, ajira nyingi, na mali nyingi ikiwemo ardhi wanazomiliki huku bara.
Wazanzibar washalalmika sana kuwa Watanganyika wanawazibia vingi!

1. Nafasi za ubalozi

2. Uhuru wa kukopa

3. Haki ya kujiunga katika taasisi na jumuia za kimataifa kama OIC

Kwa kiasi kikubwa, Zanzibar inaiona Tanganyika kama kikwazo kikubwa sana kwa ustawi wake.
 
Ni kinyume na hayo. Zanzibar wamekuwa kupe mkubwa kwenye mgongo wa Tanganyika. Mwisho wa ukupe huo ufike sasa.
 
Ni kinyume na hayo. Zanzibar wamekuwa kupe mkubwa kwenye mgongo wa Tanganyika. Mwisho wa ukupe huo ufike sasa.
Lakini ujue wanaoulinda Muungano kwa nguvu ni Watanganyika walio kwenye nafasi za uongozi.
 
Yawezekana hata hapo ulipo upo bara muungano ndio dili kubwa kwa wanzanzibari chungeni usivunjike.
Mimi sipo "bara", nipo Tanganyika.

Mimi ni Mtanganyika Halisi. Hata Zanzibar kwenyewe nilishaenda mara Moja tu.

Mimi ni Mtanganyika ninayeidai Tanganyika yangu.

Nawapenda Wazanzibar kwa sababu ni ndugu zetu, lakini turudishiwe Tanganyika yetu!
 
NA HILO NENDENI MKALITAZAMEEEE..... 😄😄😄😄
 
Tanganyika hatuna la kupoteza muungano ukivunjika ila Zanzibar watapoteza bajeti, nafasi tele za uteuzi, biashara, ajira nyingi, na mali nyingi ikiwemo ardhi wanazomiliki huku bara.
Lakini pamoja na yote hayo, hawatuthamini kabisa. Wanatuona mabwege mtozeni tu. Hawataki kabisa nasaba na sisi. Angalau kwa maswahiba wao wa pwani.

Hivyo inayumkinika kabisa kwamba Tanganyika ndiyo inayolazimisha muungano huu. Nyerere was shortsighted on this strategic blunder. Sijui lengo lake lilikuwa nini hasa kulazimisha muungano wa aina hii - lopsided (muungano wa serikali mbili?)
 
Honestly speaking, tuache unafiki na ubabaifu. Huo muungano hauna kero yoyote; bali ni MBOVU, period. Zaidi ya kujadiliana (to negotiate) kuwa na serikali moja tu, mengine yote ni UBATILI mtupu.

Aidha, muungano lazima uwe na lengo la kimkakati. Miaka yote 60 lengo la muungano huu “halijadiliki”; ni “siri”; ni “nyeti”; limefunikwa na kivuli cha kutisha na kufisha cha Mwalimu JKN kinacholindwa na wakuu wa CCM wasio na maadili. Ukweli ni kuwa maradhi hayafichiki milele. Tusubiri kilio tu. Na bado.
 
Kwamba kuunganisha nchi na nyerere kubakia kuwa Rais ndo kulizui manowari za uingereza kuivamia Zanzibar?
 
Wakianza kuudai bara wanaenda kuwakamata wahusika
Umesahau masheikh wa uamsho?
Si bara iliwafunga kisa kudai Zanzibar huru?
 
Hahahahajaj inashangaza kweli, hawasemi ila ukweli ni kwamba mwingereza alikua stand by kusaidia iwapo zanzibar wangekataa au marafiki wangesaidia kukataa muungano
Zanzibar ilikuwa Hadi na Sarafu yake
Leo hi iko wapi?
Aah au Basi mengine ni machungu hata kuyasema .
 
Hivi ni ajali raia wa nchi jirani kuongoza nchi ya Tanganyika badala ya kubaki kiti cha umakamu madhali znz wana serikali kamili isiohusu nchi ya Tanganyika?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…