TANGAZA UTALII TANZANIA: ATCL na TANAPA wana nini cha kuwapa wanafunzi 10 (bora) waliofanya vizuri Darasa la Saba 2020?

Havipo kisheria but TIME WILL TELL
 
Naona ni ssue ya watoto na wazazi wao, sijajuwa kwanini wizara na atcl wahusike kivile, kufaulu kwao ni faida ya watoto mbeleni na mtaji kwa wazazi.
Wee jamaa unakaa dunia gani? Yaaani kuwa na watoto bright kama hawa Top 10 bado hujaona kama ni faida kwa taifa? Au wewe ni mtani wangu Muhaya
 
Kama haujui hawa 10 bora wa darasa la saba ni mashujaa katika nini hapa Tanzania basi wewe sio mzalendo.
 
anza wewe n familia yako yaani wazoeshe watoto wako waone utalii ni sehemu ya maisha yao kila mwisho wa mwaka wapeleke hifadhi moja wapo hii itawajenga hata wakiwa wakubwa mwamko wa kutembelea vivutio vyetu utakua mkubwa.
Mimi na familia yangu kila baada ya miezi 6 ni lazima twende tukatembelee kivutio cha ndani kama sio Bagamoyo basi Tanga au Zanzibar...
 
Upande mwingine ni Tanapa pamoja na Serikali kuboresha miundo mbinu hasa barabara kufika hifadhini na malazi mazuri katika vivutio yaani hata mtu leo akifikiria kwenda Gombe National Park asianze kupata wasiwasi wa kufika na kulala.
Bila shaka wahusika watauona huu ushauri wako mzuri kisha wataufanyia kazi ipasavyo
 
Good idea
 
Wazo poa. Ngoja waje
 
Unaelewa maana ya kutangaza utalii, au ndiyo yale ya yule waziri wa zamani kupiga misele na madem na wahuni wanaojiita selebrite kutumbua mabilioni eti anatangaza utalii !!

Marketing... unakuwa unauza product flan, ukiwa na specific target audience, using specific strategies, ukitarajia au project returns flan.

Sasa jaza hapo mwenyewe...



 
Unaelewa maana ya kutangaza utalii, au ndiyo yale ya yule waziri wa zamani kupiga misele na madem na wahuni wanaojiita selebrite
Kwa hiyo unawaita celebrities wa Tanzania wahuni? Wangekuwa wa Marekani ungewaita super stars? Unahitaji ukombozi wa fikra
 
Marketing... unakuwa unauza product flan, ukiwa na specific target audience, using specific strategies, ukitarajia au project returns flan.

Sasa jaza hapo mwenyewe...
Ninaona umeamua kushusha notsi ulizokaririshwa na mwalimu wako darasani. Hongera sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…