Tangazo la Haki Elimu linadhalilisha kada ya Ualimu

Tangazo la Haki Elimu linadhalilisha kada ya Ualimu

Sasa kama Phd holders hawajui hapo mwl wa cheti unamlaumu nini. Tatizo lilianzia kwenye azimio la Arusha. Tuendelee kuongea matope tu.

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Wewe unashangaa nini hapo .
Magufuli na Ndalichako uliwahi kuwasikia kiingareza chao 😂😂😂😂
🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿
Ndali katisha sana, eti enzi zake alikuwa kipanga balaaaa, ana mi diploma, digrii, mastaz, dokta hadi uprofesa na yote hayo kayapata kwa kimombo
 
Huo ndio ukweli..walimu wengi ni vilaza..mana hata ualimu wanaoenda kusomea ni wale wenye division 3 na 4 za mwisho.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu sio suala la ukilaza, watu wamekimbilia mkopo na ajira za moja kwa moja. Wapo wenye division 1 hadi 3 kama ilivyo kwenye kada zingine.

Hilo la division 4 then uende ualimu huenda ulikuwa utaratibu wa zamani.
Na kama hadi sasa unatumika, basi hata kwenye kada zingine pia huwezi kuwakosa wenye hiyo division 4.

Na suala la changamoto za kuongea kingereza kilichonyooka sio kwa walimu tu hata kada zingine hili hawalikwepi.
 
Naweza sema nafuu Kada ya ualimu na medical ndipo kuna controll, kwingineko ni majanga tupu. D 1 au 2 anahiliwa certificate
 
Sasa home boy mbona unakanyaga cable na wewe.Hivi wanasema most teachers au most of teachers? Kingine hivi do we use a language or speak it?
hapo sasa! anamnanga asiyejua kwa kuonyesha alivyo empty kwenye jambo hilohilo. Asante kwa kichapo ulichompa.
 
Mwalimu yupo darasani anasema, which is talking? Wanafunzi wanaishia kushangaa.

Tangazo hili la haki elimu ni kama linadhalilisha kada ya ualimu. Je ni kweli walimu wengi hawajui Kiingereza? Sasa inakuaje mtu anafika hadi chuo kikuu hajui kimombo? Je kada nyingine nazo vipi kuhusu kujua kiingereza kwa watu wake?

My take:
Tangazo lile lipigwe stop asap!
hilo tangazo liko wapi sasa
 
Wewe unataka kukuza mada tu, kuna watu na digrii 3 wameshindwa na wakatetewa kwamba kiingereza siyo muhimu, halafu wewe unaongelea walimu?
Ni kweli, binafsi undergraduate nimefundishwa na lecturers wa chuo wenye Phd kabisa ila kingereza kina wapiga chenga
 
Mwalimu yupo darasani anasema, which is talking? Wanafunzi wanaishia kushangaa.

Tangazo hili la haki elimu ni kama linadhalilisha kada ya ualimu. Je ni kweli walimu wengi hawajui Kiingereza? Sasa inakuaje mtu anafika hadi chuo kikuu hajui kimombo? Je kada nyingine nazo vipi kuhusu kujua kiingereza kwa watu wake?

My take:
Tangazo lile lipigwe stop asap!
Huwezi compromise facts with hearsay!! sio walimu tu hata graduates wengi english ni tatizo
 
Hili tangazo nimelitafakari kwa muda na nilichoona haliko fair kwa Walimu wetu kwani linawaonesha kuwa hawajui wanachofanya.

Mwalimu: Okay, we are continued from where we stopping yesterday

Mwalimu: Quip quiet

Mwalimu: Which is talking?

(Wanafunzi wanamcheka Mwalimu wao)

With due respect, Hawa watu wa Hakielimu hawakutumia njia nzuri ya kufikisha ujumbe wao kwa Serikali kwa kuwaumbua Walimu wetu kiasi hiki.

Mimi ninawatoto wanasoma English medium schools na wanafundishwa na Walimu hawahawa wa Kitanzania. Na wako vizuri Sana kwenye hiyo lugha ngeni. Tunapoutangazia ulimwengu kuwa tuna Walimu wasiojiweza kwa lugha ya kiingereza kufundisha Ni kuwadharaulisha Walimu wetu na kuwatangazia soko Majirani zetu.

Sipingi kampeni ya ku promote kiswahili kuwa ndio lugha ya kufundishia na kujifunzia, ninachopinga Ni pale tunapo fanya promotion hiyo kwa kuumbua wengine Kama kwamba ndio sababu ya tatizo katika mfumo wetu wa Elimu.

Ieleweke hata huo ufundishaji wa kiswahili ukianza, hautakuwa mrahisi kwa jinsi tunavyodhania. Maandalizi mapana Ni muhimu kwa mfumo mpana na imara wa Elimu ya Nchi hii.

Walimu wetu waheshimiwe na wathaminiwe. Kazi wanayofanya kwa Nchi hii Ni kubwa na katika mazingira magumu. Tusiruhusu kampeni zinazo wadhalilisha kama tangazo hili la Hakielimu.
 
Hilo tangazo hata mimi sikulielewa.

Infact hata ufundishwaji wa shule za sekonari, Advance na vyuo kwa lugha ya kiswahili binafsi siungi mkono.

Tutakua local sana
 
Back
Top Bottom