Tangazo la kifo cha Benjamin Mkapa, Kurungenzi ya Mawasiliano Ikulu lawamani. Inahitaji kusaidiwa kumsaidia Rais - Jicho Letu Ndani ya Habari

Idadi kubwa ya watu mida ile ya saa 6:30 usiku ninaamini wangekuwa wamelala vitandani mwao, sasa habari za msiba wangezipataje Chief barafuyamoto?
Ndotoni?
Ok...
Tusifanye wengi. Hao wachache bado wangekua wamepata na kutoa taarifa kabla ya serikali. Ingekuja debate tena serikali imetoa taarifa ambayo tayari watu walishaitoa!
Lakini mwisho wa siku hakijaharibika kitu, wangechelewa kutoa bado tungepata cha kusema kwa nini wamechelewa na wasingetoa hiyo hiyo usiku.
 
Uongozi wa Magufuli una taswira ya utoto sana na hili kaonyesha wazi hii taswira ya utoto.
 
Hata mimi niliona hilo, hakukuwa na haraka ya rais kutangaza msiba usiku na kutupa taarifa nusu nusu, Refer tangazo la Mkapa akitangaza msiba wa Mwalimu ilikuwa clear kabisa kila kitu kilisemwakea tangazo, kwenye dress code mmh, I reserve my comments
 
Katika uongozi hakuna shocking news yeye kama comforter in chief anapokuwa kwenye confusion hivyo sisi wananchi turakuwaje ?


Yaani unataka rais afarijiwe wakati yeye ni mfariji mkuu wa nchi ?

Kwanza kwanini katuficha chanzo cha kifo wakati anajua sheria inamtaka atoe taarifa ya chanzo cha kifo ?
 
Ndio maana ya kuwa na wasaidizi wake na ndio wanapaswa kubeba hizi lawama. Tusijisahaulishe kwamba Rais nae ni mwanadamu mwenye nafsi kama tulivyo. Yako mapungufu yake mengi tu lakini yako yanayokuwa nje ya uwezo wake pia hata kama "...mkiniambia ndo mmeharibu kabisa!!"
 
Mkapa ni wa tz na sisi tuko tanzania na taratibu za tz ndizo tunazotaka
 
Kuelekeza Ni rahisi sana ukiwa nje ya ulingo
Angetangaza saa 12 mngesema kwa nini kachelewa kutoa tangazo
Umeshasema Ni shocking news,Raise kaamshwa unataka atafute auto nyeusi usiku wa manane,acha Mambo yako Pasco
Msiba umetokea Raise yupo Dodoma,Pm yupo kusini,Vp Dar,ulitaka waitane ili tu watokee kwenye TV?
Tangazo limekidhi vigezo vyote,ugonjwa Ni Siri yamgonjwa na daktari
 
Ulitaka akae kimya ili Kigogo ndo atangulie kupost? Umefeli sana. Mambo ya dressing code tupa kule, hayawezi kumfufua marehemu. Honera sana JPM kwa uwazi.
 
Duh... kumbe.
Hivi huwa wakikosea wanakir kukosea au wanakazia makosa yao ili wasionekane wamechukua ushauri wa mtu mwingine?!

Anashaurika kweli?! Especially kama ikiwa ni covid-19?!
 
Kufuata sheria na protocol liko nje ya uwezo wa kibinadamu wa rais ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…