Tangazo la kifo cha Benjamin Mkapa, Kurungenzi ya Mawasiliano Ikulu lawamani. Inahitaji kusaidiwa kumsaidia Rais - Jicho Letu Ndani ya Habari

Tangazo la kifo cha Benjamin Mkapa, Kurungenzi ya Mawasiliano Ikulu lawamani. Inahitaji kusaidiwa kumsaidia Rais - Jicho Letu Ndani ya Habari

Idadi kubwa ya watu mida ile ya saa 6:30 usiku ninaamini wangekuwa wamelala vitandani mwao, sasa habari za msiba wangezipataje Chief barafuyamoto?
Ndotoni?
Ok...
Tusifanye wengi. Hao wachache bado wangekua wamepata na kutoa taarifa kabla ya serikali. Ingekuja debate tena serikali imetoa taarifa ambayo tayari watu walishaitoa!
Lakini mwisho wa siku hakijaharibika kitu, wangechelewa kutoa bado tungepata cha kusema kwa nini wamechelewa na wasingetoa hiyo hiyo usiku.
 
Wangejifunza jinsi Mkapa alipotangaza kifo cha Mwalimu Nyerere

Kulia kwake alikuwepo Waziri mkuu ndugu Sumaye, Kushoto kwake alikuwepo Dr Omar Ali Juma na wote walivaa kimamlaka

Sasa Magufuli anavaa Shati la mchelemchele kututangazia kifo cha Raisi Mstaafu huku tukiwa tumelala usiku na yeye anaongea utafikiri alikuwa usingizini

Kisha anatoka hapo anaenda msibani huku amevaa shati la CCM

Nadhani Mkapa alimtendea haki sana Mwalimu Nyerere jinsi alivyohandle msiba wake kuliko jinsi yeye alivyotendewa na utawala huu
Uongozi wa Magufuli una taswira ya utoto sana na hili kaonyesha wazi hii taswira ya utoto.
 
Hata mimi niliona hilo, hakukuwa na haraka ya rais kutangaza msiba usiku na kutupa taarifa nusu nusu, Refer tangazo la Mkapa akitangaza msiba wa Mwalimu ilikuwa clear kabisa kila kitu kilisemwakea tangazo, kwenye dress code mmh, I reserve my comments
 
Simlaumu Mh. Rais katika hili, kwake ilikuwa ni shocking news alipaswa kufarijiwa kwanza na kuandaliwa vema kabla hajatangaza rasmi msiba huo mkubwa. Kwa tuliokwishafiwa watu muhimu ndani ya family tunalitambua vema hili.
Unaweza mpigia simu mtu wa mbali ukamsahau aliye jirani nawe.
Katika uongozi hakuna shocking news yeye kama comforter in chief anapokuwa kwenye confusion hivyo sisi wananchi turakuwaje ?

Yaani unataka rais afarijiwe wakati yeye ni mfariji mkuu wa nchi ?

Kwanza kwanini katuficha chanzo cha kifo wakati anajua sheria inamtaka atoe taarifa ya chanzo cha kifo ?
 
Ndio maana ya kuwa na wasaidizi wake na ndio wanapaswa kubeba hizi lawama. Tusijisahaulishe kwamba Rais nae ni mwanadamu mwenye nafsi kama tulivyo. Yako mapungufu yake mengi tu lakini yako yanayokuwa nje ya uwezo wake pia hata kama "...mkiniambia ndo mmeharibu kabisa!!"
 
Labda kwa sababu tumezoea ‘breaking news’ za JF sijui raisi ateuewa akina nani.

Raisi ni mtu mkubwa sana kwenye nchi anapotokea yeye mwenyewe usiku mnene kutangaza breaking news ya kitu chochote iwe tumevamiwa, kuna kiongozi kafa or whatever ‘symbolic’ inaashiria umuhimu wa tukio kwa taifa na habari yenyewe trustworthy 100%.

Unataka watu watangaze habari za kifo na press conference sijui na kuvaa nguo sahihi; mambo mengine only in Tanzania, wapi kwengine wanafanya ivyo.

Tangazo la kifo cha Mandela au Nkuranziza likikuwa na press conference?
Mkapa ni wa tz na sisi tuko tanzania na taratibu za tz ndizo tunazotaka
 
Kuelekeza Ni rahisi sana ukiwa nje ya ulingo
Angetangaza saa 12 mngesema kwa nini kachelewa kutoa tangazo
Umeshasema Ni shocking news,Raise kaamshwa unataka atafute auto nyeusi usiku wa manane,acha Mambo yako Pasco
Msiba umetokea Raise yupo Dodoma,Pm yupo kusini,Vp Dar,ulitaka waitane ili tu watokee kwenye TV?
Tangazo limekidhi vigezo vyote,ugonjwa Ni Siri yamgonjwa na daktari
 
Ulitaka akae kimya ili Kigogo ndo atangulie kupost? Umefeli sana. Mambo ya dressing code tupa kule, hayawezi kumfufua marehemu. Honera sana JPM kwa uwazi.
 
Duh... kumbe.
Hivi huwa wakikosea wanakir kukosea au wanakazia makosa yao ili wasionekane wamechukua ushauri wa mtu mwingine?!

Anashaurika kweli?! Especially kama ikiwa ni covid-19?!
 
Ndio maana ya kuwa na wasaidizi wake na ndio wanapaswa kubeba hizi lawama. Tusijisahaulishe kwamba Rais nae ni mwanadamu mwenye nafsi kama tulivyo. Yako mapungufu yake mengi tu lakini yako yanayokuwa nje ya uwezo wake pia hata kama "...mkiniambia ndo mmeharibu kabisa!!"
Kufuata sheria na protocol liko nje ya uwezo wa kibinadamu wa rais ?
 
Back
Top Bottom