Tangu nipatwe na Matatizo kazini, mke wangu amebadilika tabia

Mwanaume kama huna pesa usikae nyumbani bora kazurure hata maporini urudi usiku Ili kulinda heshima yako. Sometimes huwa hatuwambii tupitiayo makazini hawa viumbe Ili kulinda ndoa.
 
Kwenye ndoa kila mwanamke anacho kilichomvuta. Wengi pesa zako, Kazi yako, wengine heshima, wengine kuzaa watoto wote na mme mmoja, wengine ngono, nk.

So kile kilichomleta kwako akikikosa utajua tu. Huyo alifata pesa au Kazi yako thus havipo kabadilika,
 
Kuwa mpole man usimuache haya ni mapito tu Mungu kataka kukuonyesha tabia zake. Utaacha wangapi ukisikia ya wengine yako ni madogo mbona na watu wanavumilia tu huwezi pata mwanamke malaika bali jifunze kuwajua wanawake.

Wanawake wanamapungufu 360 muhimu jua jinsi ya kuishi nao kwa akili.
 
Kama huna pesa ni bora ondoka nyumbani uende hata mbali ukapambane muonane kwenye simu tu distance upunguza misuguano, ukiwa mbali wanaamini utatoka, huwezi mpa matumaini mwanamke ukiwa nae karibu na huna kitu. Mtaishia kuzozana tu kupigana na kuachana.
 
Mwanamke ameshakuzalau
 
It's all about fulfilling your family obligations as a man. Once you loose that majority of them won't take it lightly despite any reason or causes.
 
Pole sana mkuu. Sie tukitafta madem wasiopenda hela wanaojimudu huwa tunaonekana mandezi humu ila yajayo huwa yanafurahisha kama hivyo.
 
asante mkuu kwa ushauri, huu ni ukweli mchungu natakiwa kuumeza mimi bila kushauriwa na mtu kesho natoka hapa nyumbani nitakuwa natoa huduma za mtoto tuu ndoa imeshanishinda hii

Usiwe na haraka ya kuondoka nyumbani mkuu, wewe hata kama huna mishe ,amka asubuhi sana nenda kazunguke huko mjini wee tafuta mishe yeyote ya kufanya , ukikosa usirudi nyumbani pitia mida ya vijiweni kashinde kwenye kahawa, bao , draft, hata kama huna ela ya kahawa wewe piga tuu stori na masela japo ziwe za maana unajitengenezea connection, amka mapema sana kama unaenda job, jioni hakikisha yeye karudi ndio na wewe urudi nyumbani, pia usimwambie kama hujapata mishe nyingine kwenye ela ulio save unakua unaweka kidogo mfukoni kwa hesabu kali alafu unarudi nayo home hivyo hivyo, siku moja moja unapitia matunda hata ya buku unarudi na kamfuko mkononi.. jaribu hii ikishindikana safiri nenda kijijini jifanye kuna maswala ya ukoo huko ..huku unasoma hali ya hewa na huku unatafuta mishe za hapa na pale , usichague kazi mkuu

MWANAMKE UKIWA HUNA KAZI ANAKUONA WEWE NI TAKA TAKA TUU, JAPO SISI WAKIWA HAWANA HATA MISHE TUNAWAONA NI MALAIKA, MWANAMKE NI MBINAFSI SANA TAMBUA HILI
 
Shida inakuwa moja wanahangaika wee
Kisha wanarudi wenyewe uwe umefanikiwa au haujafanikiwa huwa wanarudi tu na MAJUTO
Shida inakuwa wanarudi na mtoto mwingine.

Kwangu ni ngumu na nlimuambia LIVE bila chenga kabisa. Yaani uniache mwenyewe kwenye NDOA uondoke Ukazini uzarishwe mtoto kisha urudi kwangu.

Hilo haliwezekani sahau
Kama PAPUCHI kaileta naichakata vizuri tu
 
mkuu huyo anakudharau na hil ni kwa wanawake wote yaani ukiona tu shida imekuja bado basi umekwisha, hapo kesho mambo yako ofisini yakikaa sawa lazima atabadilika kucheka cheka sana mbele zako.

NOTE Mwanamke ni mwanamke mbele ya mwanaume mwenye pesa ila mwanamke ni mwanaume mbele ya msaka tonge.
 

Habari,
Hapa ndo panahitaji ujasiri. Mke ni wako na wewe ndo mmewe, na maisha ni yenu na familia yako.
Pata muda na mwenzako:

1: Orodhesha mabaya na mazuri ya mkeo kwako na familia yako/watoto.

2: Mke wako aje na mabaya na mazuri yako kwake na kwa familia.

3: Kaeni wawili bila mihemko na kujadili pande zote kwa kusikilizana.

4: Amueni kulinganana kilichowafanya kuwa pamoja tangu mwanzo, je mabaya yenu kati yenu yamezidi mazuri?

5: Je kwenye mabaya na mazuri ni yapi yanaweza kubadilishwa au kuendelezwa na je inawezekana?

6: Kwa yasiyoweza kubadilishwa je yanatosha kuganya maamuzi mengine zaidi ya yale yaliyowaweka pamoja?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…