TANU na ASP vilikutana na vikwazo kama hivi kutoka kwa wakoloni

TANU na ASP vilikutana na vikwazo kama hivi kutoka kwa wakoloni

I
Zanzibar inatakiwa iwe ni Mkoa kama ilivyo Kigoma au Manyara, na Mwinyi anatakiwa awe Mkuu wa Mkoa
Inafikirisha sana kusikia zanzibar yenye watu 1.2M inaleta bunge la bara wabunge 50, ina mikoa 5, wilaya sijui ngapi. achilia mbali mbali tarafa na shehia. Wabunge wa muungano ni wengi kuliko wawakilishi
 
Wakoloni walivizuia vyama vya TANU na ASP kushinda chaguzi kwa mbinu kama hizi zinazotumika sasa hivi kuzuia vyama vingine kushinda chaguzi.

Kila mtu anajua na anaona kama uwanja wa uchaguzi hauko sawa kwa vyama vyote. Uwanja haukuwa sawa waziwazi wakati wa akina Nyerere na Karume wakidai Uhuru wa nchi zao na hauko huru leo wakati wa utawala wa watu weusi wenyewe. Mbinu na mitego ni ileile kama iliyokuwa ikitumiwa na wakoloni, tofauti yake ni rangi ya wategaji mitego hiyo.

Madaraka yalikuwa matamu kwa wakoloni na ni matamu kwa watawala wa leo. Mbinu zilizotumiwa na weupe sio za kificho na zinazotumiwa na weusi sio za kificho pia.

Swali hapa ni je, akina Nyerere na Karume walitumia njia zipi kuvishinda vikwazo na wapinzani wa sasa wanatumia njia zipi kuvishanda vikwazo?

Je, mbinu walizotumia akina Nyerere bado zinafaa katika zama hizi?
Nyerere na Karume walipokutana na vikwazo hawakususa mapambano. Walipambana Hadi ushindi.
Sasa unapomwachia mzanzibar ashindane na Spunda huo Ni usaliti kwa watanganyika.
 
Wakoloni walivizuia vyama vya TANU na ASP kushinda chaguzi kwa mbinu kama hizi zinazotumika sasa hivi kuzuia vyama vingine kushinda chaguzi.

Kila mtu anajua na anaona kama uwanja wa uchaguzi hauko sawa kwa vyama vyote. Uwanja haukuwa sawa waziwazi wakati wa akina Nyerere na Karume wakidai Uhuru wa nchi zao na hauko huru leo wakati wa utawala wa watu weusi wenyewe. Mbinu na mitego ni ileile kama iliyokuwa ikitumiwa na wakoloni, tofauti yake ni rangi ya wategaji mitego hiyo.

Madaraka yalikuwa matamu kwa wakoloni na ni matamu kwa watawala wa leo. Mbinu zilizotumiwa na weupe sio za kificho na zinazotumiwa na weusi sio za kificho pia.

Swali hapa ni je, akina Nyerere na Karume walitumia njia zipi kuvishinda vikwazo na wapinzani wa sasa wanatumia njia zipi kuvishanda vikwazo?

Je, mbinu walizotumia akina Nyerere bado zinafaa katika zama hizi?
Karume aliingia msituni ,nyerere alikaa mezani kwa makunaliano maalumu
 
Hi
Karume aliingia msituni ,nyerere alikaa mezani kwa makunaliano maalumu
Hivi ni kweli Nyerere na Lissu walikuwa tayari kutawala, au walihitaji muda zaidi wa kukomaa?
 
I

Inafikirisha sana kusikia zanzibar yenye watu 1.2M inaleta bunge la bara wabunge 50, ina mikoa 5, wilaya sijui ngapi. achilia mbali mbali tarafa na shehia. Wabunge wa muungano ni wengi kuliko wawakilishi
Ni mambo ya kihuni sn, hapo bado viti maalumu
 
Ni mambo ya kihuni sn, hapo bado viti maalumu
Jambo la kusikitisha ni kwamba, akina Lissu na watanganyika badala ya kumlaum Nyerere na rafiki zake akina Pius na John kwa kuifuta Tanganyika na kutuandikia katiba yenye Tume ya uchaguzi kama hii tunaelekeza shutuma na lawama kwa Samia na wazanzibar ambao wao walikataa kuifuta zanzibar yao. Ukweli tunatakiwa tujilaumu wenyewe na kuwalaumu wazee wetu kwa kutuachia Katiba kama hii na muungano kama huu. Wengi wao walikuwa wachunga ng'ombe wasiokuwa na exposure wala uelewa mpana kama wenzao wa Zanzibar ambao walierevuka miaka mingi iliyopita kutokana na mwingiliano na wageni kutoka mabara mengine. Wazanzibar walijua kusoma na kuandika kabla yetu. Walianza kuabudu mumgu mmoja kabla yetu. Wana hofu ya mungu kuliko sisi. Ustaarabu uliingia mapema zanzibar kabla ya tanganyika. Nyerere alikuwa akitua ujanjaujanja tu kuwarubuni watu wa Pwani akina Sykes kuwa vile alivyokuwa.
 
Sijui utakuwa na umri mdogo? Jikumbushe Karume alivyopata uhuru kutoka kwa sultani! Damu ilimwagika!
Na isivyokuwa bahati watanganyika tumeacha kuwalaumu akina Nyerere kwa Katiba, muungano na tume hii. Ni wao sio samia wala wazanzibar
 
Makubaliano maalumu yapi hayo?
Kwamba ukoloni utaendelea kwa njia ya indirect/mamboleo malkia ataendelea kuwa mkuu wa serikali kwa mlango wa nyuma,mifumo ileile ya kikoloni itabaki kwa kubalidisha rangi tu kiwa nyeusi badala ya ile nyeupe
 
Hiyo inafahamika karibu kwa kila mtu, kinachokosekana ni viongozi wenye akili na maarifa kama akina Nyerere na Karume. Wapinzani wa sasa hawana busara wala hekima pia. Akina Nyerere na Karume walikuwa wanavieneza vyao vyao hadi vijijini na kila sehemu. Wakati akina Nyerere wakidai uhuru hawakusema kuwa kama watapata uhuru watataifisha mali za wageni wote na kuwafukuza wakoloni. Wao walikuwa wapole wakati wanadai uhuru na kuwa wakali baada ya kuupata uhuru. Hawa akina Lissu wanakuwa wakali kwa katiba, viongozi, muungano na kila kitu cha CCM hata kabla ya kuingia Ikulu, nani akupe IKulu?

Wapinzani wangeendelea kujenga ofisi za vyama vyao kila kijiji ili kuonyesha ukubwa na utayari wao wa kushika dola, wangeikubali hali ilivyo sasa hadi hapo watakapokuwa wameingia Ikulu. Mfano, hata kule marekani kama kikitokea chama kikatangaza kuvunja muungano wa USA na kuyapa uhuru majimbo bila shaka chama hivyo kitafutiliwa mbali na chama tawala.
Viongozi wa chama tawala hawawezi kukubali mabadiliko yanayoweka uwanja sawa kwa wote kwa kuwa wao na vizazi vyao na vya marafiki zao wanataka kutawala milele. Wamejazana serikali kuu, halmashauri, idara mbalimbali, taasisi, mashirika ya uma na majeshi. Ndiyo asili ya jeuri yao kuwa hakuna kitakacho badilishwa kwa sababu wao ndiyo wenye maamuzi ya mwisho. Hata mabadiliko wanayodai wadau mwisho wa siku watakaozuia ni watawala kwa kura za hapana maana wapo wengi katika sehemu nyeti.
 
Kwamba ukoloni utaendelea kwa njia ya indirect/mamboleo malkia ataendelea kuwa mkuu wa serikali kwa mlango wa nyuma,mifumo ileile ya kikoloni itabaki kwa kubalidisha rangi tu kiwa nyeusi badala ya ile nyeupe
Kwahiyo lile Azimio la Arusha la nyerere lilitoka wapi?
 
Viongozi wa chama tawala hawawezi kukubali mabadiliko yanayoweka uwanja sawa kwa wote kwa kuwa wao na vizazi vyao na vya marafiki zao wanataka kutawala milele. Wamejazana serikali kuu, halmashauri, idara mbalimbali, taasisi, mashirika ya uma na majeshi. Ndiyo asili ya jeuri yao kuwa hakuna kitakacho badilishwa kwa sababu wao ndiyo wenye maamuzi ya mwisho. Hata mabadiliko wanayodai wadau mwisho wa siku watakaozuia ni watawala kwa kura za hapana maana wapo wengi katika sehemu nyeti.
Mbona wanaoimba iyenaiyena ni watoto wa wwtu wa kawaida tu? Wanafaiika na nini?
 
Mbona wanaoimba iyenaiyena ni watoto wa wwtu wa kawaida tu? Wanafaiika na nini?
Wanafuata mkumbo tu. Wengi wao wamekuwa 'brain washed' hawajitambui. Lakini wanaofaidika ni wale niliowataja hapo juu.
 
Wanafuata mkumbo tu. Wengi wao wamekuwa 'brain washed' hawajitambui. Lakini wanaofaidika ni wale niliowataja hapo juu.
Yaani unaongelea watoto, wakwe. Wake na wajukuu wa akina Nyerere, Malecela, pius, mongela, mwiny1, Mkap, Kikwet3. Magufuli, bul3mbo, sokoine, Kawawq, Mnauye. Sapi, Jumbe. Thabiti. Karume. Nk. Nchi ni kama urithi wqo binafsi.
 
Naamini ndivyo ilivyo.
Ukijaza vinasaba wengi kwenye serikali tegemea kuona viongozi wanaosifu tu wanaosubiri maagizo kutoka juu ya nn wafanye na wasifanye.
 
Back
Top Bottom