TANU na ASP vilikutana na vikwazo kama hivi kutoka kwa wakoloni

TANU na ASP vilikutana na vikwazo kama hivi kutoka kwa wakoloni

Wakoloni walivizuia vyama vya TANU na ASP kushinda chaguzi kwa mbinu kama hizi zinazotumika sasa hivi kuzuia vyama vingine kushinda chaguzi.

Kila mtu anajua na anaona kama uwanja wa uchaguzi hauko sawa kwa vyama vyote. Uwanja haukuwa sawa waziwazi wakati wa akina Nyerere na Karume wakidai Uhuru wa nchi zao na hauko huru leo wakati wa utawala wa watu weusi wenyewe. Mbinu na mitego ni ileile kama iliyokuwa ikitumiwa na wakoloni, tofauti yake ni rangi ya wategaji mitego hiyo.

Madaraka yalikuwa matamu kwa wakoloni na ni matamu kwa watawala wa leo. Mbinu zilizotumiwa na weupe sio za kificho na zinazotumiwa na weusi sio za kificho pia.

Swali hapa ni je, akina Nyerere na Karume walitumia njia zipi kuvishinda vikwazo na wapinzani wa sasa wanatumia njia zipi kuvishanda vikwazo?

Je, mbinu walizotumia akina Nyerere bado zinafaa katika zama hizi?
Shida uzao wa hao jamaa ulikua sio wa ma keyboard warriors, wao viongozi wakipanga jambo jamii inatenda,,,ila kwa sasa zimejaa siasa za ma keyboard warriors tu, kiongozi atajitoa hata jela ataenda ila waambie hao wafuasi waje tu kuliamsha wote wataufyata kwenye simu zao wakitegeana nani aende,,,,,,,nchi ingekua ya kukombolewa kwa mambo yalipofikia sasa watu wangeamka , shida huu ni uzao wa makeyboard warriors, kiongozi wao wa ndani akishindwa utaanza kusikia wazungu watasaidia...........uzuri CCM wameshawajua watapiga tu makelele mwisho wa siku mambo yanaenda, propaganda za wazungu zimewajenga vibaya side B
 
Back
Top Bottom