Hapana, Tanzania haihitaji rais aina ya hayati Magufuli. Yule alikuwa doa na unajisi kwa ardhi ya Tanzania; hususan jamii Watanzania wenye utu.
Kwa nini nasema hivyo?
1. Kama alikuwa "solution" hata kwa robo ya matatizo uliyotaja, na leo amekufa na yenyewe yapo - then he was, undeniably, a complete failure.
2. Kwa vile unakiri kuwepo kwa hayo matatizo na yeye hakuyamaliza na sasa hayupo wala hawezi kurudi tena; basi hata akija mwingine kama yeye ataishia kupata matokeo hayohayo, ni jina tu ndio litabadilika lakini kushindwa na matokeo vitakuwa vile vile. That's logic.
3. Lakini akija kiongozi wa ukweli, sio mtawala au dikteta kama hayati Magufuli, yeye ataweka Katiba nzuri, Sheria kali na za haki, mifumo thabiti na himilivu, mazingira na utashi - vitakavyosababisha mabadiliko ya fikra, utamaduni na matendo yenye faida, ufanisi na maendeleo ya kudumu kwa vizazi.
Huyu akiondoka mambo yaraendelea vizuri, legacy itazidi kuimarika kwa vizazi vijavyo.