Habari JF, Ukitaka kuliongoza taifa la Tanzania na kuliletea maendeleo ni lazima uwe in mtu mkali. maono na Mwenye msimamo. Tanzania ina asilimia kubwa ya watu wa aina 3:-
1. Wavivu - hawapendi kujituma kufanya kazi
2. Uwezo Mdogo wa kufikiri -Elimu kwa Tanzania haiwakomboi Uwezo wa alie prof ,PHD ,degree ukitoa aile kujua vitu vingi linapokuja suala la kufikiri hawatofautiana sana .
3. Wanapenda starehe sana
Sasa kuongoza watu wenye sifa hizo huhitaji sana kuwashirikisha ,unacho hitaji ni kuwaongoza njia sahihi .
Ukiachana na tuhuma alizopewa Hayati JPM ambazo hazina Ukweli wala ushahidi wowote alijitahidi sana .
Hivyo kuna haja ya kumpata mwingine Mwenye makali zaidi tuweze piga hatua zaidi .
Sema tu kifo ni nywila ya Mungu, lakini JPM angalifaa bado kuliongoza taifa mpaka mwisho wa muhula wake. Ilipaswa matamanio na ndoto zake zote kuhusu maendeleo ya taifa letu zipate kutimia.
Kama angalikuwepo hai yule jamaa hadi hii leo, hivi sasa tungalikuwa tunazungumza lugha nyingine kabisa katika yale aliyotamani kuyafaniskisha. Natumbua hakuwa na mzaha kabisa katika kusukuma maendeleo ya vitu, usimamizi thabiti wa rasilimali za nchi, uthubutu wa kufanya maamuzi magumu, na kurudisha nidhamu katika utumishi wa umma,
Lakini hakuwa malaika. Lakini ule upande wake wa pili ndiyo lilipokuwapo tatizo jingine. Ebu ungana na mimi kupitia mashairi ya wimbo ufuatao,
Ingekuwa vipi! X 3
Ingekuwa vipi kama JPM angekuwa hai, Je! Membe angalitakiwa kupewa fidia na Musiba!?
Ingekuwa vipi! X 3
Ingekuwa vipi kama JPM angekuwa hai, Je! Mtoto pendwa Sabaya angalitupwa kolokoloni !?
Ingekuwa vipi! X 3
Ingekuwa vipi kama JPM angekuwa hai, Je! Kesi ya ugaidi ya Mbowe ingalitupwa na yeye kuwa huru mtaani!?
Ingekuwa vipi! X 3
Ingekuwa vipi kama JPM angekuwa hai, Je! Vyama vya upinzani vingalikuwa huru kufanya mikutano yao halali ya kisiasa !?