Tanzania bado ina uhitaji mkubwa wa kupata Rais kama Magufuli mwenye makali zaidi

Tanzania bado ina uhitaji mkubwa wa kupata Rais kama Magufuli mwenye makali zaidi

Unajua toka muanze kumuelezea huyo Magufuli na hiyo sifa ya uuwaji ni kwamba mmekuwa mnarudia kuwataja watu walewale tu kila siku ambao ndio mnadai kuwa aliwauwa kwa sababu ambazo hazina mashiko, nasema hivyo kwa sababu kwa jinsi ambavyo mnavyomkuza na hiyo sifa ya uuwaji kwa mtu ambaye ni kiongozi tena dikteta ni wazi kungekuwa na list ndefu ya watu aliyowauwa mbali na hao sijui maiti za kwenye viroba ambao ni watu wasiojulikana wala sababu za kuuliwa kwao.
Aliua hajaua?????
 
Hapana, Tanzania haihitaji rais aina ya hayati Magufuli. Yule alikuwa doa na unajisi kwa ardhi ya Tanzania; hususan jamii Watanzania wenye utu.

Kwa nini nasema hivyo?

1. Kama alikuwa "solution" hata kwa robo ya matatizo uliyotaja, na leo amekufa na yenyewe yapo - then he was, undeniably, a complete failure.

2. Kwa vile unakiri kuwepo kwa hayo matatizo na yeye hakuyamaliza na sasa hayupo wala hawezi kurudi tena; basi hata akija mwingine kama yeye ataishia kupata matokeo hayohayo, ni jina tu ndio litabadilika lakini kushindwa na matokeo vitakuwa vile vile. That's logic.

3. Lakini akija kiongozi wa ukweli, sio mtawala au dikteta kama hayati Magufuli, yeye ataweka Katiba nzuri, Sheria kali na za haki, mifumo thabiti na himilivu, mazingira na utashi - vitakavyosababisha mabadiliko ya fikra, utamaduni na matendo yenye faida, ufanisi na maendeleo ya kudumu kwa vizazi.
Huyu akiondoka mambo yataendelea vizuri, legacy itazidi kuimarika kwa vizazi vijavyo.
Wewe unazungumzia mabadiliko ya mfumo wakati mada inazungumzia aina ya kiongozi.
 
Taifa linahitaji mfumo dhabiti wa utawala wa nchi na si Rais. Mfumo utajengwa kwa kupitia Katiba bora inayoendana na wakati uliopo sasa.
 
UONGO mwingine huu unaojificha kwenye jina la USOMI.

Historia na Takwimu za nyumbani kwako, ukaambiwe na mgeni? UPUUZI. Kazaneni kupiga, mnajadili based on how mmevimbiwa sio?

Uchumi umekua ila hamkuvuka daraja, KIPINDI tulichovuka mstari MTASEMA ni juhudi za nyuma sio?

FACTS na EVIDENCES ni ripoti ya CAG, amesema, UBADHIRIFU huo, haujawahi tokea tangu ADAM na EVA waliumbwa
Tulia uandike vizuri hoja zako, maana umejichanganya mno hapo kwenye andiko lako.

Tambua tu kuwa "takwimu" zenu mnazopika na kuziamini ndio zimekufikisha hapo.
Hakuna mtu au taasisi yoyote yenye kuhodhi ukweli. Takwimu zozote zile huwa subject/open to criticism (good or bad, positive or negative); tawimu hupingwa na takwimu na vigezo vipo.
Sijui kama unaelewa.

Fikra zenu zimeharibiwa, ndio maana propganda mnaita Facts na Takwimu. Mnaishi kwa hisia na mihemko inayotokana na brainwashed education mliyopata. Ukibaki hapo utakufa na huo upumbavu, ukijinasua utakuwa na matumaini siku zijazo. Chagua mwenyewe.

Twende kazi.

1. Kama "takwimu" zenu za ndani zilikuwa za kweli sasa media censorship ilitoka wapi?

2. Kama mliyokuwa mnayafanya yalikuwa mazuri kwanini kusigina Katiba na sheria za nchi awamu ile ya 5? Hakuna bunge live, hakuna mikutano ya siasa, hakuna uhuru wa maoni wala kupata habari hurt (hofu ya kujua ukweli) nk vilitoka wapi?

3. Wakosoaji wa serikali na wa matendo yenu maovu kuitwa "wasaliti" nk- ilikuwa ni mwendo vitisho, ukatili na propaganda. Why?

Common sense tu inakataa huo uhuni wenu na legacy fake ya Mwendazake. Fact.
 
Awe kama magu lakini

1. asiwe muuaji.

2. mbambikiaji kesi watu,

3. anayetumia majambazi kuongoza (refer Sabaya),

4. Asiyeiba kura,

5. asiye piga watu risasi.
Akili kijiko cha chai inachangia ajenda kubwa. Chefuuuu!!
 
Aliua hajaua?????
Sina ushahidi mkuu kwamba aliuwa au hajauwa, na point yangu sio kuuwa tu maana hata kipindi cha Kikwete tuliona Ulimboka ilipangwa auliwe hilo wote tunajua hivyo hayo mambo yapo, ila Kikwete hajapewa sifa ya kiongozi muuwaji kama tunavyoona kwa Magufuli na hapo ndio hoja yangu ilipo kwamba kama Magufuli alikuwa na sifa ya kiongozi dikteta na muuwaji basi tungekuwa na list ndefu tu ya watu waliyouliwa na sio hivi tunaokoteza okoteza.
 
Mfumo ni nini?
Kingozi ni nini?

Hebu fafanua/nyambulisha zaidi hoja yako tafadhali
 
Duh! Kwahiyo hadi Akwilina nae kauliwa na Magufuli?
Ushahidi huu hapa
Ben sanane yupo wapi
Anzory gwanda yupo wapi
Watu waliuwawa KIBITI,MKURANGA, KISIJU NA MAFIA
Nani alimpiga risasi TL
Akwilin Akwilin Alipigwa risasi na nani kwa amri ya nani?
Mpaka uwe mpumbavu ndiyo utadai ushahidi dhidi ya serikali ile ya ki dictata
 
Duh! Kwahiyo hadi Akwilina nae kauliwa na Magufuli?
IGP huteuliwa na nani?
RPC huteuliwa na nani
Ocd huteuliwa na nani?
DED huteuliwa na nani?
Wote hawa ni chanzo cha kuuwa kwa AKWILINA kama hujui? Unafikiri kuua mpaka ufyatue risasi???
 
IGP huteuliwa na nani?
RPC huteuliwa na nani
Ocd huteuliwa na nani?
DED huteuliwa na nani?
Wote hawa ni chanzo cha kuuwa kwa AKWILINA kama hujui? Unafikiri kuua mpaka ufyatue risasi???
Sasa kama ni hivyo basi hakuna kiongozi asiyekatili na muuwaji.
 
Sina ushahidi mkuu kwamba aliuwa au hajauwa, na point yangu sio kuuwa tu maana hata kipindi cha Kikwete tuliona Ulimboka ilipangwa auliwe hilo wote tunajua hivyo hayo mambo yapo, ila Kikwete hajapewa sifa ya kiongozi muuwaji kama tunavyoona kwa Magufuli na hapo ndio hoja yangu ilipo kwamba kama Magufuli alikuwa na sifa ya kiongozi dikteta na muuwaji basi tungekuwa na list ndefu tu ya watu waliyouliwa na sio hivi tunaokoteza okoteza.
Ulikuwa wapi wakati wa ile operation ya MKIRU? unajua ni kiasi gani cha watu walipotea kule hadi leo hawajulikani walipo au unaongea tu kama upo bar?
 
Kwakifupi tu nimalize kwa kusema Mungu ni fundi...uwe na siku njema
 
Ila hapa tunataka kiongozi wa nchi, hakuna mfano wa rais shoga aliyefanya vizuri kwa sababu ni shoga?
Atal Behari Vajpayee na Hastings Kamuzu Banda walikuwa ni Makhanisi na walitawala vizuri.

Hayati Qaboos pia alikuwa ni mtawala asieuwa Wananchi wake.

James Buchanan Raisi wa 15 wa Amerika alikuwa Shoga mbobezi na alitawala vizuri.

I can go on and on...
 
Ulikuwa wapi wakati wa ile operation ya MKIRU? unajua ni kiasi gani cha watu walipotea kule hadi leo hawajulikani walipo au unaongea tu kama upo bar?
Ndio ueleze ufahamike usiishie kutoa tuhuma za jumla jumla tu sio kila mtu ana mtazamo sawa na wewe.
 
Tanzania haihitaji tena watawala Wachawi kama wa awamu ya 5.
 
Back
Top Bottom